Bennie 369
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 713
- 534
JE UNAMFAHAMU?Hebu nikuulize swali ni nani aliyeiumba dunia hii na vyoye vilivyomo?
Kama ukimjua aliyeiumba dunia hii basi ndiye mmiliki maana ameweza kuiumba na anaweza kuibomoa..hiyo peke yake ni hati miliki.
Kwaio aliyeiumba ndiye mmiliki.
Mfinyanzi siku zote anaweza kukifinyanga kitu na kikatokea...kama apendavyo.
Na wakati huohuo anaweza akakibomoa.
Fundi mbujifu anaweza akabuni mashine jinsi awezavyo na anaweza akaiharbu kama atakavyo na mtu yeyote asiweze kuitengeneza...huyo ni mmiliki.
Aliyeweza kukupa pumzi na kuiondoa huyo ndiye anayekumiliki wewe.
Kuondoa pumzi ni wakati wowote kama jinsi apendavyo haitaji ushauri..
Huyo anakumiliki..
Vivyo hivyo kwa dunia.