Ni nani motivational speaker mkali hapa bongo?

Ni nani motivational speaker mkali hapa bongo?

Kwa mliowai kuwasikia au kuwaona watoa mada au waongeaji kwenye majukwaa ya hamasa kwenye angle tofauti naamini kuna watu walikuvutia kwa umahiri wao, story zao halisi za maisha au kukupa nguvu fulani hivi.

Mimi namkubali sana Masudi Kipanya na kuna mtu nilimuona jukwaa fulani anaitwa James.

Namkubali Kipanya sababu atengenezi hadithi na ana facts.

Wewe unaesoma hapa unamkubali nani?


Nafikiri Magufuli ndiyo kiboko yao.
 
Bila kumsahau mzee wangu maneno yake ukiyapuuzia lazima ujute
 
Ni Eric Shigongo pekee ndiye anayaishi anayo yafundisha na kidogo unaweza ukawa na mifano ya kuona hasa anapo ongelea biashara na ujasiriamali lakini wengine walio baki ni wapiga story na wasoma vitabu tuuuu.
Huyuhuyu ninayemjua au ndugu yake.
Huyu ametajirika kwa umbea na uchonganishi. Na hiyo dhambi ndiyo kwanza imeanza kumtafuna.
 
Dr Elie Waminian Huyu MTU hana mpinzani Barani Africa.. Ni mtanzania
 
Kiukweli mimi hiki kitu kinaitwaga kusikiliza motivation speaker hakijawai niingia akilini labda wenzangu eti nisikilize story za mtu ndio na mimi nifanikiwe, naonaga ni upotezaji wa mda tu na watu kupiga hela za maboya motivation lazima itoke kwako sio kwa story za wapiga dili. Period
 
David Mbaga,Mark Walwa Marekana And Geoffrey Mbwana My church Pastor
 
Sijawahi kumsikiliza yeyote wakati akiongea as Motivational Speaker lakini kama ningekuwa nimefanya hivyo basi huenda ningekuwa convinced na watu wenye elimu ndogo kama akina Masoud Kipanya au Shigongo kuliko wenye elimu kubwa kama akina Chris Mauki!!!

Watu dizaini ya Kipanya wanakuwa real... na wataongea mambo waliyo na uzoefu nayo wakati watu aina ya Mauki wanakuwa too theoretical! Mara nyingi huwa wanahubiri yale wasiyoyafanyia kazi... more often than not, they preach what they don't practice!
 
Back
Top Bottom