Elimu inadharauliwa kwasababu watanzania wengi wanasaka ukombozi wa kiuchumi kuliko ukombozi wa kifikra.
Hii ni kutokana na changamoto za kiuchumi tu mkuu, mtu anaona haina maana kusoma na kusota mtaani wakati kuna deals ndogondogo anaweza akafanya akaendesha maisha ya kila siku.
Njaa ikizidi sana,watu watashindwa kuvumilia tu mkuu.
Kuna kijana Mtunisia Mohamed Bouaziz alijichoma moto kisa maisha magumu amesoma na hana ajira, Hii iliwaamsha unemployed wengi Tunisia watu waliandamana ,barabara zilifungwa. So Ni suala la Mda mtu akitokea wa kujitoa muhanga mmoja tu. Sera zibadilishwe