mngony
JF-Expert Member
- Jul 27, 2012
- 5,555
- 6,972
Akizungumza na mwanablog Magendela kupitia SALMA MADAI IT ANAYETEMBEA NA NDOTO ZA RAIS DKT SAMIA
Novemba, 2023, mdada mrembo wa sura na umbo, ameelezea ndoto za kuwa Rais wa Tanzania siku baadae.
Salma ambaye amekuwa akijiita Salama wa Samia Suluh katika mtandao instagram, amedai kuwa na asili ya kutoka Manyoni,Singida kwa sasa ni Mwenyekiti wa UWT CCM tawi la Mbezi na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM Mkoa wa Dar Es Salaam.
Vilevile amejitanabaisha kama mwanaharakati wa kutetea usawa na haki za jinsia ambaye ni mwenyekiti wa Taasisi ya DMI Foundation na pia ni makamu mwenyekiti wa Jumuiya ya kupiga ukatili wa wanawake SMAUJATA na Mkuu wa Idara ya wanawake Taifa wa TK Movement.
Akiongea na Bloger amesema alipata elimu ya Shule ya Msingi Utemini kuanzia mwaka 1992 hadi 1998 na Sekondari ya Salmin Amour 1999 hadi 2002.
Kada huyo wa CCM anasema taaluma yake ya IT ( ambayo hakumuelezea aliipata wapi) hajaitumikia kwa muda mrefu, kwani ndoto yake ilikuwa ni kufanya biashara na shughuli za kijamii.
Anasema amefanya biashara ya kuuza viatu na nguo kwa takribani miaka 12 na baadae biashara ya kuuza virutubisho vya lishe.
"Biashara hii ya virutubisho vya tiba lishe nauza Tanzania, Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Zambia na kwingineko ambapo anakira kuwa elimu yake ya IT imekuwa msaada kwake zaidi" alieleza
Anasema anatumia mawakala na teknolojia za mitandaoni zimekuwa chachu ya yeye kufanikiwa katika biashara hiyo ambayo anazalisha bidhaa zote kwa kutumia kiwanda kidogo anachomiliki
baadae aliamua kujikita katika siasa ambayo anafanya hadi sasa kupitia CCM.
Kada amekuwa akifanana na Mbunge wa Segerea Bonna Kamoli kwa muonekano , kimo, umbo na hata wote kuwa wanasiasa wanawake wenye utaalamu wa IT ma wenye ndoto za kuwa Marais wa Tanzania hapo mbele.