Wanabodi,
Nimekutana na hii kitu, nimeisoma, sio tuu nimeshangaa, bali nimechoka, imeniacha hoi, ukisoma ukaona jinsi tunavyoibiwa rasilimali zetu, na wanaofanya tuibiwe, ni wenzetu tuliowapa dhamana ya kutuongoza, mtu unaweza kupata wazimu, ukarukwa na akili, ukikamata SMG, unaweza kuwamiminia risasi Watanzania wenzetu wanaoiuza nchi yetu na maliasili zake kwa bei ya bure kwa wageni kwa jina la wawekezaji kwa kisingizio kuwa sisi hatuna uwezo wa kuwekeza ili kuvuna rasilimali hizo zitufaidie!.
Mpaka hapa tulipo, Tanzania tumesha ibiwa sana kwenye madini kutokana na mikataba mibovu ya kinyonyaji na mpaka sasa ninapoandika haya, bado tunaendelea kuibiwa kwa mikataba hiyo hiyo mibovu iliyoingiwa na wenzetu. Sasa Mwenyeenzi Mungu katupa gesi asili angalau ituokoe kutoka katika hili lindi la umasikini uliotopea...lakini kumbe..., masikini Watanzania!, sijui nani katuloga!, maana na huku kwenye gesi asili, Watanzania tunaendelea kuibiwa mchana kweupee! huku wenyewe na hawa makuwadi tunaowaita ni viongozi wetu, tukiangalia tuu kama mazuzu!. Nchi hatuna sera ya gesi, hatuna sheria ya gesi!, hatuna lolote tulijualo kuhusu uchumi wa gesi, lakini ndio bado tunashadadia kugawa vitalu vya gesi kama njugu!.
Hadi hapa ninapopandisha uzi huu, mwaka huu wa 2012, nchi yetu hatuna sera ya gesi wala sheria ya gesi lakini tumeingia mikataba 23 ya PSA ambayo in reality, we are getting almost nothing!, nil!. Hii ni "day light Robbery!" na inafanywa na viongozi hawa hawa tulio nao tukidhani ni wenzetu lakini kumbe. ..
Sijui ni nani aliyetuloga!.
Mungu Ibariki Tanzania!.
Paskali