Tomaa Mireni
JF-Expert Member
- Sep 8, 2015
- 2,395
- 2,391
- Thread starter
- #21
Hio nchi masikini yenye mipango mizuri ni ipi?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hio nchi masikini yenye mipango mizuri ni ipi?
Hivi hili linahitaji picha za Juu ,huoni huko mitaani kwenu kama uko Bongo hii?Ungeweka sasa na aerial photograph ya bongo ili hoja yako iwe na mashiko zaidi.
Shida sio kitengo bali utashi wa kisiasa,pesaKitengo cha mipango miji kipo tuu kwenye makaratasi but in reality ni sifuri kabisa.
MalawiHio nchi masikini yenye mipango mizuri ni ipi?
Siyo Watanzania wote wanaishi maeneo ya misongamano! Mfano mimi niko Kijijini huku Milimani! Hatuna huo utaratibu wa Mipango Miji.Hivi hili linahitaji picha za Juu ,huoni huko mitaani kwenu kama uko Bongo hii?
Watu wanajenga milimani na serikali inaona haichukui hatua na maeneo tambarare yapo hayapimwi wagawiwe viwanja. Inashangaza sanaDah umenikumbusha juzi nimepita Babati Mjini yani watu wamejenga juu ya mlima wanahatibu kabisa uoto wa mlima ule mzuri unatoa ukingu.
🤣🤣🤣Hata Google wanapata tabu sana kujua na kuonyesha mitaaMji wetu pendwa huu nenda kaulize bei za nyumba sasa ndio utajua kachumbali ni mboga sasa hapo ngoja mvua inyesha ni hatari tu.View attachment 1791572View attachment 1791575View attachment 1791576
Huyo kazungumzia migogoro hakuna mpango wa kupima wala niniNaona Katibu Mkuu wa CCM ameanza kulifanyia kazi suala la ardhi. Hii imeriporiwa na gazeti la Mwananchi la Leo
Agizo la CCM kwa Wizara ya Ardhi
THURSDAY MAY 20 2021
Dar es Salaam. Katibu mkuu wa CCM, Daniel Chongolo ameitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuongeza kasi ya utatuzi wa migogoro ya ardhi inayosababisha malalamiko kwa wananchi.
Ameyasema hayo leo Alhamisi Mei 20, 2021 katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dodoma huku akirejea ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020/25 inayoeleza kasi ya umilikishaji wa ardhi kwa wananchi.
"Hatua hii itawafanya wananchi wawe na usalama zaidi wa maeneo yao na ni muhimu. CCM italifuatilia kwa karibu kuona utekelezaji wake," amesema Chongolo.
Amesema kwa sasa ni wananchi wachache wanaomiliki ardhi kisheria, huku asilimia kubwa wakimiliki kiasili au bila utaratibu wa kisheria, ambapo mtu ananunua ardhi na kujenga nyumba ya thamani kuwa na umiliki halali wa kiwanja hicho.
Aidha, Chongolo amesema chama hicho kinaelekeza kufanyika kwa uthaminishaji na fidia kwa wananchi waliotwaliwa maeneo yao kwa shughuli za umma pamoja na uimarishwaji wa mfuko wa fidia.
"Viongozi wote wa Serikali kuanzia ngazi za vijiji na mitaa mpaka wizara wanapaswa kuhakikisha wanatatua na kuandaa siku mahsusi za kutatua migogoro ya ardhi kwa haraka na wakati.”
"Chama kinaelekeza kumaliza migogoro ya ardhi katika Wilaya za Kondoa, Kitero, Kongwa, Morogoro, Kilombero na pembezoni mwa hifadhi mbalimbali ambayo imekuwepo kwa muda mrefu na kuwasumbua wananchi," amesema.