Ni ngumu sana jambo lisilo na Goli la Mkono kwa Tanzania (Watanzania) kuleta ushindi

Ni ngumu sana jambo lisilo na Goli la Mkono kwa Tanzania (Watanzania) kuleta ushindi

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Ukifatilia katika mambo mengi hapa Tanzania iwe kwenye siasa, michezo, uchumi au hata mahakama au kesi, katika kila jambo ambalo Mtanzania yumo kama hilo jambo halitoi mwanya wa Rushwa, Upendeleo au kwa lugha ya Mh. Nape Goli la Mkono basi hilo jambo ni ngumu sana kufanikiwa.

Nakumbuka enzi za Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alitoa sana sapoti kwa team zetu za Taifa za Kiume na Kike lakini kila mashindano waliishia kumvunja moyo Hayati Magufuli.

Unakuja kuona tena suala la Yanga jinsi Dkt. Samia Suluhu Hassani alivyojitoa kwa hali na mali ili kuwapa hamasa vijana walete ushindi kwa Heshima ya Taifa lakini wakaenda kinyume na matarajio.

Simba follows same trends.

Shida ni nini?
 
Siasa imevuka mipaka yaake na rushwa nayo inachangia kufanya watu kuwa wavivu wa kufikiri.
 
Ukifatilia ktk mambo mengi hapa Tanzania iwe kwenye siasa, michezo, uchumi au hata mahakama au kesi.

Ktk kila jambo ambalo Mtanzania yumo kama hilo jambo halitoi mwanya wa Rushwa , upendeleo au kwa lugha ya Mh Nape Goli la Mkono basi hilo jambo ni ngumu sana kufanikiwa.

Nakumbuka enzi za Hayati Dkt. John Pombe Magufuli alitoa sana sapoti kwa team zetu za Taifa za Kiume na Kike lakini kila mashindano waliishia kumvunja moyo hayati Magufuli.

Unakuja kuona tena suala la Yanga jinsi Dkt. Samia Suluhu Hassani alivyojitoa kwa hali na mali ili kuwapa hamasa vijana walete ushindi kwa Heshima ya Taifa lakini wakaenda kinyume na matarajio.

Simba follows same Trends.

Shida ni nini?
Yanga ipi, ile iliyoshika nafasi ya pili? Haudhani nafasi ya pili ni ushindi!
 
Back
Top Bottom