Ni ngumu sana kumpata Mwanamke kama Tulia Ackson. Ana uwezo mkubwa, anafaa kuwa Rais

Tumeshuhudia ubora wa utawala wa mwanamke Samia, nashawishika kuanza sala na maombi, kwa kuwa uongozi unatoka kwa Mungu ikimpendeza akitoka samia aingie Tulia Akson

Ni mapema mno lakini wazo hili limweke kwenye hadhara watu wachambua strength na weekness zake mapema ili nuru ikiangaza juu yake lisiwe ni jambo ya kubahatisha. Anatufaa sana baada ya Samia.
 
Naona Tulia anajitahidi kulipa chawa wampigie promo humu mitandaoni vibaya sana. Uwezo huo Hana, labda kwenye siasa za kiburi Cha madaraka.
 
Kwa nini isiwe wewe?
 
Hatutaki tena mwanamke, ni dhaifu...maamuzi karibu yote yanafanywa na wanaume tena kwa maslahi yao binafsi ye (huyo mwanamke rais) anakuwa kama boya tu...hiyo hatutaki ijirudie tena!.
 
Umelipwa shilingi ngapi mkuu?
 
Kama mpango huu wa kwenye mitandao ni wake basi anajihalibia na nikama hajakomaa kisiasa. Na kama ni mapenzi yenu tu ya kumtangaza hivyo basi mjue mnamuhalibia kabisaa.
 
Ni kweli kabisa. 100%
 
Kuuuuuuuuuuule,hakujawahi kuwa na watoto wenye akili sta kidogo.Ila kumejaa watoto wanaochekana Kwa Kamasi zao kukaukiana kwenye pua na mashavu Yao.
Hawaambiani Wala kushauliana wakanawe uso,rahasha Kila mmoja anamwona mwenzake Kamasi zimemganda bila kujua nae zimemganda.

Tutafanya mchakato kuwapelekea KIOO angalau waweze kujitizama kibinafsi,japo Kuna wasiwasi kuwa Kuna mwenzao anaweza kukimbizia chumbani Kwa mama yake ili tu awe anajiona mwenyewe Kwa wenzake hapana.

Wanasahau kuwa nyumba ile ni ya wao wote,tofauti ni mama zao ila baba ni mmoja.

Ila Kila mama mtu ana chumba,hivyo mtoto kuona kama chumba Cha mama yake ni rahisi yeye kuingia anavotaka afu wa Kiume😂😂😂😂.
Msisahau kuweka no zenu za Simu.
 
Kwa hiyo Samia hafai sindiyo?
 
Kibongo bongo baada ya huyu tulie nae itachukua muda sana kuja kuwa na raisi wa jinsia ya Tulia.
Sio itachukua muda mrefu, bali haitokuja kutokea tena! Hata Magu angejua kama hatamaliza muda wake kuwa Rais, asingeteua mgombea Mwenza wa jinsia ya kike nina uhakika!. Haitokuja kutokea, kama ambavyo haitokuja kutokea tena kwa Marekani kumuweka Rais mwenye asili ya Black

Sent from my SM-A042F using JamiiForums mobile app
 
Hakika inaweza kuwa hivyo.
 
Sawa chawa ila eti Mbeya wanamtaka Sugu 😆😆😆
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…