Ni ngumu sana kumpata Mwanamke kama Tulia Ackson. Ana uwezo mkubwa, anafaa kuwa Rais

Ni ngumu sana kumpata Mwanamke kama Tulia Ackson. Ana uwezo mkubwa, anafaa kuwa Rais

Hamna kitu hapo. Watu mnasifia ujinga tu sijui mumelipwa Shillingi ngapi? Huyo Tulia bila LIFT ya Magufuli asingefika hapo alipofika. Alimfanyia nini Magufuli hadi akampa u Naibu Spika, ni siri yao

Kwenye duru za sheria wala siyo nguli kihivyo, nenda kaulize UDSM uone kama ana machapisho. Ukikuta ana machapisho nenda kayatest kwa Plagiarism application ndiyo uje hapa.

Watu eti wanamsifia kushinda kesi ya muta 200 mwaka 2015. Ile kesi hata mwanafunzi wa first year Law School angeshinda tu kwa kuwa tayari Jaji wa High Court alikuwa na maelekezo.
Exactly. Yaani Mimi kwa hapa kwetu mtu akishakuwa na madaraka, hasa yanayopatikana kwa kusimamia hila, inakuwa ngumu kuona uwezo wake halisi.
 
Nashukuruuu Sanaaaa kwa kuliona hilo ambalo wengine tulishaliona tangia muda mrefu sana na kuandika sana humu jukwaani kwa kurudia rudia sana ,katika kueleza uwezo mkubwa wa kiakili na kiuongozi alio nao Mheshimiwa Dkt Tulia Acksoni Mwansasu Dada wa Taifa na Nguli wa sheria kuwahi kutokea nyanda za juu kusini. Bora wewe umejisemea ukweli maana mimi nikiandika naambiwa kuwa namtetea na kumpamba sana.ok ngoja nisiandike sana leo.
Rippti ya CAG ndo kipimo chake kama Spika, je amekiweza?
 
Habari za Sabato!

Sijawahi kumfahamu Mwanamke yeyote kwa hapa Tanzania mwenye uwezo kama Tulia Akson. Sisemi ili wengine wamuonee Wivu, wala sisemi ili yeye awe na Kiburi. Ila naongea kila ambacho ninaokiona Kwa Tulia mwenyewe.

Kama utapata Nafasi ya Kumsikia Tulia Akson akizungumza iwe kwa kuhojiwa au kuhutubia, utagundua kuwa hana tofauti na kina Kamala Harris au kina Hilary Clinton.

Utulivu!
Kujiamini!
Umahiri!
Hoja!
Ubobevu!,

Nimeona Watu wengi wanapokutana na Tulia katika mijadala wakimshindwa kwa Hoja. Unapozungumzia hoja Unazungumzia uwezo wa akili ya mtu kujenga mantiki, yaani kitu kieleweke. Wakati mwingine kwa lugha rahisi.

Tulia sijawahi kumsikia akijali uanamke wake au maumbile yake kama sehemu 6a kikwazo katika kazi zake.
Tena yeye hupendelea changamoto anapokutana na sisi wanaume.

Tulia hatajali kama wewe ni Waziri au Mheshimiwa, ukiwa bungeni kama ataona kuna jambo hujalitolea maelezo yaliyonyooka au hakuna hoja anauthubutu wa kukukosoa au kutaka kukuweka Sawa.
Kujadiliana na Tulia Akson itakupasa uwe na uwezo mkubwa kama yeye au umzidi ili usije ukaaibika.

Kwa mwanaume mwenye upeo mdogo lazima amwone Tulia kama Mjuaji, hasa pale atakaposhindwa kwa Hoja.

Tunaposema Wanawake wapewe nafasi tunahitaji wanawake wa mfano wa Tulia Akson. Wanawake wenye uwezo.

Sio Mwanamke anayelalamika hajapewa haki yake. Tunahitaji Wanawake wenye uwezo wa kudai haki zao wenyewe bila kusaidiwa. Hao ndio watakuwa na uwezo wa kuongoza.

Tulia Akson anauwezo wa kushika nafasi ya Urais katika nchi yetu na sio hivyo tuu hata kuongoza Nchi yoyote hapa Duniani. Kwa sababu anasifa za level za kimataifa.

Nimemaliza
Machadomo watabisha watakuita wewe chawa.

Mwisho Mbeya haiwezi kumpoteza mtu kama Dk.Tulia eti at the expenses of Sugu 😂😂
 
Mwisho, Dk.Tulia ni mwanasheria kitaaluma. Je, ametumia wanasheria wake kwa manufaa ya watawala, au kwa manufaa ya wanyonge? Je, Dk.Tulia ni mwanasheria mtafuta ngawira na vyeo, au mwanasheria mtetezi wa haki?
Ni mtetezi wa haki!
P
 
Shida ninayoona anayo, ni kuna muda anafanyaga mambo kukomoa yani ni kwamba utafanya nini sasa nimefanya.
Hana tofauti sana na ndungai.
Yani kama hakupendi basi atakukomoa hata kama anajua anachofanya si sahihi.

..uwezo wa kielimu anao, na ndio maana akafaulu vizuri na kufikia ngazi ya PhD.

..tatizo linakuja ktk jinsi watawala walivyomtumia, na jinsi Dk.Tulia alivyowatumikia mabosi wake.
 
..uwezo wa kielimu anao, na ndio maana akafaulu vizuri na kufikia ngazi ya PhD.

..tatizo linakuja kwa jinsi watawala walivyomtumia, na jinsi Dk.Tulia alivyowatumikia mabosi wake.
Basi anaweza kutumiwa na mafisadi na walowezi, na madonors maana kumbe ana udhaifu wa kutumika.
 
🤣🤣kwahiyo kizmkaz Hana uwezo?
Haupigi mwingi tena?
Usimwaribie shangazi yangu msomi,mwenye udaktare wake wa kukaa darasani,sio kupewa bure India,huku ulitaga form foo🤣🤣🤣
 
Nafasi ya Urais imemzidi uwezo.
Kwa Urais ninaoujua mimi hata wengi walikuwa tu MaRais kwasababu ndio hivyo tuko Tanzania.

Hili neno Rais huku kwetu inabidi tulipe jina lingine ili tusisharibu maana na kuwadhallilisha watu kama akina Putin, Stalin, Churchill, Truman, Roosevart, Bush, nk.
 
Back
Top Bottom