Naona comments nyingi za kupeana moyo ; tena kutoka kwa waandishi wa habari wakubwa.
Watu wanaandika magazeti na story za half lela ulela . Hii yote ni kwa sababu tunajua kuwa tuna poor investment and poor scouting. Ndio maana tunatumia maneno mengi sana.
Nimeshawahi kusema hapa kuwa Mpira ni Investment, sio matangazo au blah blah . Lakini siku zote hatujifunzi. Sababu ya Kaizer kututoa last time , was an investment and poor scouting( scouting za kitapeli).
Mabadiliko ya Yanga kwa sasa ni kutokana na Investment, hata kama ni ndogo, na kama Yanga akifanya Investment zaid na Club ikawa na long term plan basi ndani ya miaka 3 ijayo anakwenda kuwa Bingwa wa Africa kama hii consistency ya uwekezaji usio na kelele za kizaramo kama kwa mwafulani zikiendelea.
Simba haina Investment ya kuitoa Wydad , na kudhani kuwa Simba ataitoa Wydad ni moja ya tatizo la afya ya akili ( Poor Mental Health)
Mpira sio kujaza watu au kutoa motivation words kama tupo vitani. Wakati watu wanatumia nguvu nyingi kufanya Investment, wengine wanashinda mitandaoni na kupiga kelele kuwa anapata Hasara, haya ndiyo madhara ya utajiri wa kurith. Kama unapata hasara mbona bado upo, ni another form of UTAPELI wa Mwafulani.
Well, alichofanya Raja ndiyo atakachofanya Wydad. Mark my Words. Hakuna mambo ya Sugar Coat , au mambo ya Inshallah inshallah. Kwanza Wydad kafurahi kuwa na Simba, njia ya kusonga kwake ni kama kutoa unywele kwenye maziwa.
Washabiki wa SSC tujiandae kisaikolojia, hatuna uwezo wa kuitoa Wydad , kama tunawaza kuitoa Wydad kwa uwepo wa Chama, imekula kwetu.
Investment matters a lot , Ahly
Ilikuwa kidogo isiende robo fainali, Investment kati ya Hilal na Ahly na quality ya wachezaji ndiyo iliyoamua wa kwenda robo fainali.
Mpira haujengwi kwa kusumbua watu mitaani na matarumbeta, it's all about investment and scouting ya kibabe.
Yanga anayo nafasi kwenda Nusu fainali kwa asilimia 60%, ni muda wa Yanga, tukubali hizi Timing and let's cherish for their success.
Huu mwaka Yanga anakwenda kuonesha utofauti wa investment and process. Simba mara zote anafika robo fainali, kombe la maluza au Klabu Bingwa: katika Miaka 5 mfululizo, safari yake inaishia robo fainali and yule Muhindi anatuaminisha hayo ndiyo mafanikio. It's awkward kama kila mara unaishia hatua hiyo hiyo; that means you are not learning and huna growth path and long term goals.
It's OVER now , Tanzaania kupitia Dar es salaam Young Africans (Yanga ) anakwenda kuvunja huu mwiko na kutinga nusu fainali ambapo SSC ameshindwa kuvuka for the past 5 years.
Nawatakia kila heri Simba kwenye game yao na Wydad next two weeks , but in truth , ninajua simba haina madhara kwa Wydad kwa namna yoyote ile. Yaani sio game ambayo ninashauku ya kuiona, kwa sababu matokeo yapo wazi.
Game ya Rivers na Yanga, inatia hamasa kwa sababu hata investment zao zinalingana na uwezo pia wa players hawajaachana sana. Anything can happen.
Kuna mdau kauliza Yanga kama kawekeza mbona hajaweza hata kuwafunga Vipers? Yanga kama kawekeza yuko namba 9 kwa viwango vya CAF? Yanga kama kawekeza anashiriki Mashindano gani ya CAF?
Yanga ameifunga Mazembe ambyo ni team mbovu msimu huu na kwa mwaka huu team zote za Congo zimeburuza mkia. Je Yanga kama kawekeza anaweza kuifunga Raja? Waydad je? Mtoa mada jibu hayo maswali, usilete porojo!