Ni nini chanzo cha vijana wengi kuwa na tamaa

Ni nini chanzo cha vijana wengi kuwa na tamaa

Massawejr

Member
Joined
Jul 22, 2022
Posts
19
Reaction score
23
Muda mwingi nimekuwa nikikaa na kuwaza kuhusu hili swala la vijana wengi kuwa na tamaa. Tumekuta vijana wengi wakiwa wanaingia katika wimbi kubwa la majanga na hasa ni tamaa,

Tamaa imefanya vina wengi wakumbwe na majanga mbalimbali kama magonjwa na wengine tunaona wakiwa wanapoteza maisha kwasababu ya tamaa.

Mimi nadhani ni muda sahihi kwa vijana kuacha kutamani/tamaa kwa ujumla kwa maana hakuna kitu kinakuja kiurahisi na wala maisha hayana shortcut.
 
Tamaa inaweza sababishwa na kuiga maisha ambayo huwezi kuyaishi hali inayopelekea kufanya vitu vinavyoweza ku~risk,afya au maisha kiujumla kikiwemo na kifo
NAWASILISHA
 
Chanzo kikubwa cha tamaa ya vijana ni maisha wanaoyaona mitandaoni, wao huamini kile wakionacho hata kama hakina uhalisia. Hii imechangia pakubwa mmomonyoko wa maadili katika jamii zetu hapa nchini.

Vijana wajue kuwa maisha ya mitandaoni mengi ni maigizo, no mengine yana uchafu mwingi nyuma yake, wajifunze kulidhika na maisha yao na kujitahidi kuongeza bidii kufikia mafanikio wanayo yatamani. Hakuna short cut katika mchakato wa mafanikio.
 
Kwanza hueleweki tamaa ipi? Kijana yupi kafa kwa sababu ya tamaa? Fafanua
 
Tunaishi kwenye jamii ya watu waliojaa wivu sana.
Na ukisikiliza maneno ya watu malengo yako yatabaki kuwa ndoto.

Kuna watu wana wivu kwa sababu akiangalia umri wake na uchumi alionao haviendani hata kidogo.
 
Back
Top Bottom