Ni nini hatma ya yote haya?

Ni nini hatma ya yote haya?

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
221
Reaction score
197
Hakika katika migogoro inayoendelea ni dhahiri kuwa watu wengi tumekuwa tukitamani kuona nini mwisho wa yote yanayoendelea kutokea hivi sasa.

Mpaka sasa Urusi inaendelea na kile inachokiita kuwa ni "oparesheni ya kijeshi" katika taifa la Ukraine. Watu wengi tunatamani kuona mwisho wake.

China inaendelea kuweka tishio la kivita juu ya kisiwa kidogo kilichojitenga cha Taiwan Huku Marekani ikiendelea na ziara zake nchini humo kitendo ambacho kinazidi kuchukiza taifa la china.

Korea kaskazini chini ya Kim Jong Un bado inaendelea na vitisho vyake vya majaribio ya silaha za nyuklia kitendo ambacho kimekuwa kikikwaza mataifa kama Marekani na Korea kusini.

Israeli bado nayo ikiendelea kutopatana kwa kina dhidi ya jirani yake Palestina kutokana na migogoro ya muda mrefu juu ya mji wa Jerusalem.

Ikumbukwe kuwa, mwaka 1914 vita kuu ya kwanza ilitokea ikihusisha mataifa yaliyogawanyika pande mbili yaani Triple Alliance (Ujerumani, Italia, USSR) dhidi ya Triple Entete( Uingereza, na mataifa mengine) lakini vita hii ilimalizika mwaka 1918 baada ya Triple Alliance kuchakazwa.

Lakini mnamo mwaka 1939 ndipo, Vita hii ilianza upya huku Japani akionekana kuongeza nguvu katika upande wa Mjerumani.

Ndipo mwaka 1945, vita hii ilimalizika mara baada ya Marekani kutupa bomu la nyuklia katika miji ya Yeroshima na Nagasaki nchini Japani. Na ndipo lilipoundwa shirika la amani duniani chini ya Marekani kupiga marufuku matumizi ya silaha za nyuklia kutokana na madhara yalioachwa nchini Japani
hadi leo.

Je! Unahisi vita vitakavyotokea katika karne hii vitasababisha madhara kiasi gani kwani ikumbukwe kuwa mpaka sasa kuna mataifa zaidi ya 15 yanayojulikana kuwa na silaha za silaha za nyuklia.

Tuendelee kumuomba Mungu atunusuru dhidi ya majanga ambayo yanaweza kutokea endapo kutakuwa na machafuko ya kidunia.

Ikumbukwe pia, Urusi waliwahi kutengeneza bomu aina ya Tsars~bomb ambalo lilionekana kuwa ni bomu hatari zaidi kuliko mabomu yaliyowahi kutumika hata yale ya Yeroshima na Nagasaki. Hivyo hatuna uhakika kama bomu hili liliachwavkuendelea kutengenezwa au la.

Pia, Korea ya Kaskazini anaendelea kutengeneza mabomu ya masafa marefu yanayoweza kuvuka bara moja hadi lingine. (Intercontinental missiles) kwa wakati huo huo mataifa haya yana uhasama mkubwa dhidi ya taifa la Marekani ambalo ndilo limeonekana kuchukua jukumu la kusimamia amani ya dunia.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ibariki Afrika na dunia kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom