Ni nini kiliwashinda UKAWA kwenda mahakani?

Huu ndiyo mtaji wa Ccm siku zote,anachokiandika hakijui na hatakijua daima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mahakama kuu ya Kenya imeonesha Ulimwengu kuwa ipo huru,na ni Mahakama yenye wasomi wanaojitambua kuacha hawa wakwetu wanaowalamba wakubwa miguu kias cha kuinajisi taaluma yao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unazungumzia mahakama ipi labda kwa mfano? Kama ni hii iliyozuia kubomolewa kwa nyumba kimara halafu ikapuuzwa unategemea nini??!
 
Katiba ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania hairuhusu uhalali wa kuhoji matokeo ya urais mahakamani ndio maana punde tu baada ya uchaguzi kuisha na matokeo kutangazwa rais mteule huapishwa na mchezo unaishia hapo.

Tofauti na wenzetu Wakenya katiba yao inaruhusu kuhoji matokeo. Mara tu baada ya uchaguzi na matokeo kutangazwa katiba ya Kenya inasema rais mteule hawezi kula kiapo au kuapishwa ndani ya wiki tatu ili kama kutakuwepo na malalamishi yoyote basi wahusika ambao ni walalamishi kimsingi waweze kwenda MAHAKAMANI na kuhoji matokeo

Na hicho ndicho kimefanyika hadi kufikia matokeo yaliyompa Uhuru ushindi kubatilishwa.

Mkuu jifunze kutofautisha kati ya msalaba na kujumlisha
 
Unaelewa ulicho kiandika lakini?
 
Uliyeleta post elimu ya uraia una,soma katiba vizuri na pia tafiti ujue kwanini watu walidai katiba mpya,kwa Kenya wameweza kwani walibadili katiba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
akili yako na wewe,hujui kupinga matokeo ya urais mahakamani inaelezwa kwenye katiba ya kenya,katiba yetu imezuia haki hiyo!!!!jiongeze na wewe
Mfafanulie tu kwamba kenya matokeo hupingwa mahakamani ambako ni huru na tume ni huru tofauti kabisa na hapa tz wooooote wanahusika kwenye mahakama aunkwenye tume ni wateure Wa ccm serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Tatizo siyo usawa wa majaji waliotangaza ushindi.

Elewa kwamba:-

Tanzania ni nchi mbili tofauti katika Africa Mashariki.

Katiba ya Kenya inasimamia demokrasia. katiba ya Tanzania inasimamia udikteta kwamba tume ikishamtangaza raisi katika uchaguzi, hakuna mahakama yoyote duniani inahaki ya kuhoji ushindi. Katika hali hiyo ulitegemea wafanye nini?

Bila shaka utaelewa Watanzania wazalendo wanapodai katiba mpya wana maanisha nini.

Bila shaka unaelewa wazalendo wanaotaka raisi apunguziwe hiyari za uteuzi kwa kuwa anaowateua lazima wawe puppets. Lazima watangaze utashi wake hata kama ni kinyume cha haki. Umeelewa?

Kwa kuwa umeelewa, mishale yako peleka ccm kwa kuua taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…