Ni nini kimeifanya CCM kushindwa kabisa kufanya lolote juu ya Mipango Miji?

Ni nini kimeifanya CCM kushindwa kabisa kufanya lolote juu ya Mipango Miji?

Nitakualika mitaani kwetu baada ya tarehe moja nije nikuonyeshe open spaces
Kinondoni pachoto open space imekuwa garage
Biafra uwanja wa michezo kuna garage na parking ya malori ...
Hiyo mifano michache tu nakupa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mtawalaumu CCM hadi kiama. Swala la mipango miji ni la halmashauri za mikoa pamoja na wilaya. Je, humo ndani wanaoshiriki ni kina nani? Je, sera za miji kwenye hizo halmashauri zinapitishwa na kina nani?

Mtapiga kelele mpendavyo lakini siku ya mwisho wenye lawama ni halmashauri na siyo chama cha siasa. Piganeni ingieni huko kwenye halmashauri za mikoa/wilaya mpiganie haki zenu kupiga kelele mitandaoni bila kuhesabiwa kwa vitendo ni uzandiki tu.
 
Kinondoni pachoto open space imekuwa garage
Biafra uwanja wa michezo kuna garage na parking ya malori ...
Hiyo mifano michache tu nakupa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Sasa kama viwanja vipo vya kutosha na havijaanza kutumika sawasawa kuna kitu kinaharibika kwa kuwa parking, mikutano au soko kwa muda?

Sababu matumizi hayajabadilishwa bado hivyo ni viwanja
 
Mtawalaumu CCM hadi kiama. Swala la mipango miji ni la halmashauri za mikoa pamoja na wilaya. Je, humo ndani wanaoshiriki ni kina nani? Je, sera za miji kwenye hizo halmashauri zinapitishwa na kina nani? Mtapiga kelele mpendavyo lakini siku ya mwisho wenye lawama ni halmashauri na siyo chama cha siasa. Piganeni ingieni huko kwenye halmashauri za mikoa/wilaya mpiganie haki zenu kupiga kelele mitandaoni bila kuhesabiwa kwa vitendo ni uzandiki tu.
Halmashauri asilimia kubwa nchi hii ziko chini ya Chama gani?
 
Hili linahitaji uongozi wa wizara utakaotambua kuwa ni tatizo. Process ya kupimi viwanja na kupata hati ilikuwa ngumu na bado ngumu sana japokuwa Toka awamu ya tano imeingia kidogo kuna uafadhali japo ni gharama kubwa.

Tunasikitika sana tukiona nchi za waafrika wenzetu jinsi zilivyopangwa vizuri eneo kama Goba lingepangwa vizuri na ile milima kungependeza sana. Madale sijui kwa nini palishindikana kupangwa, kisauke, boko cha simba, bunju sehemu kubwa haijapangwa, kiaraka, kerege hata huko baobab.

Temeke sijui walifeli wapi kupaacha watu waharibu mipango miji, mbande, ubungo yote kuanzia kwa gwajima mpaka maramaba mawili serikali ilikuwapo lakini wakaacha sagulasagula ya maeneo.

Inatia aibu kwa kweli, eneo kama kawe ilikuwaje lugalo ipimwe ipangwe vizuri kawe wakaicha chaguchagu. Au oysterbay ipangwe msasani kujae panya.
 
naona jengo la chadema linalamikiwa ,dah kweli chadema mwiba wa samaki halafu show ya safari ya kibabe yaani mbowe hata haongeeii wananchi wameachiwa waisome namba kwa raha zao,yaani sasa hivi unaweza kulalamikia mzunguko wa hela mdogo utasikia ufipa,haaa hahaha
 
Hili linahitaji uongozi wa wizara utakaotambua kuwa ni tatizo. Process ya kupimi viwanja na kupata hati ilikuwa ngumu na bado ngumu sana japokuwa Toka awamu ya tano imeingia kidogo kuna uafadhali japo ni gharama kubwa...
Inasemekana sababu ya yote uliyosema ni chadema mkuu,wanazi wa lumumba wanakuambia malalamiko ya nini mbona jengo la mtaa wa ufipa wa chadema halijapangwa,ndo maana mwenyekiti wao huwaga anasubiri usajili kutoka ufipa awape vyeo siyo kwa akili hizi humu ndani
 
Chadema wenyewe wamepanga makao yao makuu kwenye makazi holela midimbwi kibao nyumba utafikiri Choo cha city
Hii hoja ni nzito..kama huiwezi ni bora ukakaa kimya.
Wakati mwingine tupunguze mizaha kwenye mambo ya msingi.

Miji ya Tanzania imeachwa ijiendee holela kama moto wa nyikani.
Hii ni hatari na aibu kwa taifa.
 
Hili linahitaji uongozi wa wizara utakaotambua kuwa ni tatizo. Process ya kupimi viwanja na kupata hati ilikuwa ngumu na bado ngumu sana japokuwa Toka awamu ya tano imeingia kidogo kuna uafadhali japo ni gharama kubwa...
Mie hadi Kuna kipindi najisemeaga kimoyo moyo kuwa inawezekana hawa wenzetu labda walinyimwa bongo kama sisi. Hii nchi kusema kweli ukichukua case study ya Dar tu unaweza lia.

Ni kama hakuna serikali au waliopo serikalini wote ni mazumbukuku. Umetoa mifano mizuri sana. Kwa nini mzungu alizipanga oysterbay, Upanga na Masaki na sie tukashindwa kupanga sehemu zingine na juzi simamia?

Maeneo mapya kama kivule, chanika, kinyerezi, kibamba, madale, makabe, msakuzi, Goba, Bunju na Mbagala huko kwa nini serikali wameshindwa kuyapanga. Basi kama hawakuwa na hela kwa nini hata hawakutoa mwongozo jinsi ya mpangilio wa ujenzi Yaani watu wajenge kwa mfumo fulani na lazima wahakikishe Kuna barabara za mitaani kwenye kila mtaaa?

Mie bado naomba wana Ccm watujibu humu. Sio kwamba tunawaandama bure, waseme hata kama hela hawana za kupima, imekuwaje wao na serikali zao kushindwa kutoa hata miongozo na kuelekeza juu ya usimamizi kwa serikali za mitaa ili kuhakikisha watu wanajenga vizuri kwa mpangilio na maeneo yanapendeza?
 
Hii hoja ni nzito..kama huiwezi ni bora ukakaa kimya.
Wakati mwingine tupunguze mizaha kwenye mambo ya msingi.

Miji ya Tanzania imeachwa ijiendee holela kama moto wa nyikani.
Hii mi hatari na aibu kwa taifa.
Wao Kil muda ni kuleta masikhara tu. No wonder hii nchi ni vituko kila kona
 
Solution yake inaanzia waizarani kulete mpango kazi ambao mpaka mwenyekiti, mtendaji na mjumbe wa kaya anafahamishwa jinsi viwanja au maneno yanavyotakiwa kuendelezwa.

Ilikuwa rahisi tuu mjumbe wa shina amuonye mangi fulani anayejenga mpaka nje ya mawe pale mabibo opposite NIT. Au aple sinza queen of sheebah lakini mjumbe na mtendaji siku hizi wamekurupuka kukusanya fedha za kibali cha ujenzi halafu wanaminya matumboni mwao. Wala hawajishughulishi kuangalia mipaka, barabara zinapata nafasi.
 
Shida ni usimamizi wa sheria za mipango miji
Utakuta serikali za mitaa wanatoa vibali vya ujenzi holela mpaka watu wanaziba chochoro
Alafu viongozi wa juu wanafungia macho tu

Ova
 
Sasa kama viwanja vipo vya kutosha na havijaanza kutumika sawasawa kuna kitu kinaharibika kwa kuwa parking, mikutano au soko kwa muda?

Sababu matumizi hayajabadilishwa bado hivyo ni viwanja
Maeneo mengi kwanza TANU/CCM walipewa na watu kama kuwaunga mkono hivi unalijua hilo!

Ova
 
Mie hadi Kuna kipindi najisemeaga kimoyo moyo kuwa inawezekana hawa wenzetu labda walinyimwa bongo kama sisi. Hii nchi kusema kweli ukichukua case study ya Dar tu unaweza lia.

Ni kama hakuna serikali au waliopo serikalini wote ni mazumbukuku. Umetoa mifano mizuri sana. Kwa nini mzungu alizipanga oysterbay, Upanga na Masaki na sie tukashindwa kupanga sehemu zingine na juzi simamia?

Maeneo mapya kama kivule, chanika, kinyerezi, kibamba, madale, makabe, msakuzi, Goba, Bunju na Mbagala huko kwa nini serikali wameshindwa kuyapanga. Basi kama hawakuwa na hela kwa nini hata hawakutoa mwongozo jinsi ya mpangilio wa ujenzi Yaani watu wajenge kwa mfumo fulani na lazima wahakikishe Kuna barabara za mitaani kwenye kila mtaaa?

Mie bado naomba wana Ccm watujibu humu. Sio kwamba tunawaandama bure, waseme hata kama hela hawana za kupima, imekuwaje wao na serikali zao kushindwa kutoa hata miongozo na kuelekeza juu ya usimamizi kwa serikali za mitaa ili kuhakikisha watu wanajenga vizuri kwa mpangilio na maeneo yanapendeza?
Wapuuzi tu hao maccm wanaakili za hovyo hakuna wanacjoweza fanya,huoni Rais wao anateua watu kutoka nje ya lichama lao na kuwapa madaraka au ananunua wapinzani na kuwapa ofisi anajua huko yamejaa nambulula na matokeo yake ndio haya sasa Kila kitu wamefeli hili la makazi holela kwa sababu linaonekana wazi
 
Binafsi nakwera na Tabia ya Halmashauri kuuza viwa ja nje ya mji wkt katikati ya mji kina viwanja vingi havijajengwa tangu miska ya 80 huko. Kwa nini hii Sharia isibadilishwe ili MTU skishindwa kujenga na kuishi ndani ya Mipaka 5 Uwanja au msingi uuzwe tu? Wengi kujenga msingi na kuiacha eti anatunza kiwanja. Kumbe uchafu tu
 
Mipango miji duniani kote hutegemea uwezo wa kipato wa jamiii husika

Usiite ujenzi holela kuna maenro ya wenye nazo mipango miji iko vizuri kaishi huko kama uwezo sababu huko nyumba kujenga ramani tu yaweza kugharimu hata milioni kumi sababu nyumba unatakiwa kujenga kwa specific specification na kunakuwa na maeneo ya supermarkets sio magenge au duka la mang au mpemba l na kunakuwa na hotels sio mama nitilie

Ukikomaa copy and paste sio rahisi

Nchi ili duniani ya dunia ya tatu isiyp na makazi holela?taja hata moja tu
Jibu la kijinga kabisa.

Mimi nimetembelea nchi nyingi maskini, miongoni mwa hizo nchi, licha ya umaskini wake, wana mipangilio mizuri sana ya miji yao.

Hivi nchi kama Mali, inaizidi nini Tanzania? Mali, kwenye miji yake yote, hakuna mahali ambapo watu wanajenga kabla ya kupimwa. Sehemu zote, wapimaji wametangulia, wanaojenga wanafuata. Tanzania, wanaojenga wanatangulia, wapimaji wanafuata nyuma.

Mimi sijasomea mipango miji, nina utaalam wa hali ya juu kwenye mambo mengine pamoja na surveying, hakika nikiambiwa nisimamie mpangilio na upimaji wa makazi yote Tanzania, nitafanya vizuri zaidi maradufu ya hawa wataalam uchwara wa Tanzania.

Kutetea mpangilio wa hovyo wa makazi Tanzania, ni uwendawazimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mipango miji ipo ramani zipo tatizo utekelezaji na usimamizi wa serikali

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
Hizo ramani zinazoonesha upana wa barabara za mitaa mita 6, nazo unaita ni ramani za miji?

Nadhani kati ya taaluma ambazo huenda zinachukua watu ambao ni very low IQ, nadhani mojawapo ni hiyo ya mipango miji.

Wanaona kabisa, mipango yao ya hovyo ilivyoharibu miji lakini wanaendelea na specifications zile zile miaka yote. Hata hivyo viramani vya hovyo, wanavificha ficha kwenye ofisi zao utadhani ni tunguli za kichawi badala ya kutawanya kwenye ofisi za ngazi za chini ili watu waweze kuzifikia kiurahisi, na yote hiyo ili kila wakiulizwa wapate kulipwa vihela kidogo kwa madai wakakutazamie kwenye ramani kama vile ni kazi ngumu sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom