Ni njia gani wanaweza kutumia chadema kuzuia tume kutangaza matokeo ya raisi

Ni njia gani wanaweza kutumia chadema kuzuia tume kutangaza matokeo ya raisi

jonas255

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
225
Reaction score
110
Mambo vp wanasheria wenzangu...

Kulingana na kichwa cha habari na hali tulio nayo sasahivi ninaitaji kujua yafuatayo:

Je kuna njia gani chadema wanaweza ku apply mahakamani ili tume hisimtangaze raisi (prerogative order)?

Kutokana na usitishwaji wa matokeo ya zanzibar kua batili na haramu kwa wapiga kura feki kupiga kura je uchaguzi wetu unaweza kurudiwa kutokana na kura zilizopigwa uko zanzibar kwa raisi wa jamuhuri wa muungano wa tanzania?
 
wasione aibu wakubali tu wameshindwa. Huwezi kupata majimbo hata 50 hayajafika then upotoshe kwamba umeshinda uraisi hizo no ndoto za mchana.
 
Kutokana na uchaguzi zanzibar kua feki kwa kua na watu waliopiga kura bila vitambulisho na idadi ya wapiga kura kuzidi hili swala kisheria naona lina affect hadi uchaguzi wetu wa bara kwa sababu wazanzibar wale wale walimteua raisi wa jamuhuri wa muungano wa tanzania

hiyo inamaanisha katika kura za uraisi kwetu kuna kura za wale watu feki wa zanzibar waliopiga kura..

Je kuna njia gani chadema wanaweza ku convince mahakama isitishe uapishwaji wa raisi atakae shinda siku ya leo
 
NEC walisimamia wenyewe uchaguzi wao wa jamhuri...

ZEC nao walisimamia wenyenyewe pia

Walichokuja kushare ni wino tu ila sio wote waliwachagua marais wazanzibar walichagua marais wa jamhuri na kinyume chake...

So chadema walichobakiwa nacho ni kukubali tu kuwa walitumia njia ya mkato kwenda ikulu ambayo pia ilihadaiwa na wale wananchi wa Mwanza waliokesha viwanjani na wale wa Musoma waliodeki barabara kumbe ilikuwa danganya toto tu....
 
But swali limuulizwa kwenye mrengwa Wa kisheria sion haya ya kujibu usicho kijua...
 
Kama ningekuwa na uwezo wa kuwashauri UKAWA, ningewashari wakubali matokeo. Huwezi kuoa siku hiyo hiyo na kutarajia kupata mtoto siku hiyo hiyo na kumwandikisha shule siku hiyo hiyo. Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha, EL amewasaidia kuongeza idadi ya % ya kura za Urais huenda hata wabunge wa viti maalum wataongezeka, hiki sio kitendo cha kubezwa, ndege aliyeko mkononi ni bora zaidi aliyeko juu ya mti. Kitendo cha UKAWA kuungana katika uchaguzi huu kimewapatia nguvu na wamefanya vizuri sana ikilinganishwa na chaguzi zilizopita. Hata hivyo, imeshuhudiwa muungano huu kutoheshimiwa miongoni mwao wenyewe kiasi cha kusimamisha wagombea wawili kutoka vyama shirika kitu ambacho kimewachanganya baadhi ya wapiga kura kutoamini kama kweli ni muungano wenye tija, na wengine kuchanganya kura na kusababisha wagombea kushindwa; Katika hali kama hii, UKAWA wanapaswa kuchukua changamoto zilizojitokeza na kuanza kuzifanyia kazi kuanzia leo ikiwa ni pamoja na kuimarisha Muungano wao kwa malengo maalum. Kitendo cha kugomea matokeo hakitakuwa na tija kwa sababu Rais akishatangazwa ataanza kutumia ngivu zake za Urais nao kuendelea kulalamika bila kuhudumia wapiga kaura wao kama ilivyotokea mwaka 2010 walivyogoma kutomtambua Mhe. JK, lakini mbona JK amekuwa Rai hadi leo.

Aidha, wahakikishe Chama kinakua na taswira ya Kitaifa ili Watanzania wote wajione kama sehemu ya Chama ingawa kiuhalisia inaweza isiwe hivyo. Hebu fikiria kuhusu CCM Meneja Kampeni Alhaji Bulembo - kutoka Mara; Katibu wa Itikadi na Uenezi - Mtwara; Katibu Mkuu wa Chama - Arusha; Mwenyekiti wa Chama - Pwani, Makamu Mwenyekiti - Iringa. Katika hali kama hii watu wengi wanajiona kama sehemu ya chama kwa mfano wakiwa na mkutano wa Kampeni Musoma, Wanamusoma wakimwona Bulembo wanajiona kama sehemu ya Chama hata kama kiuhalisi sio hivyo. Sasa Angalia kwa CDM - Mwenyekiti - Arusha; Meneje wa Kampeni - Arusha, Mkurugenzi wa Fedha - A, Komu; huko huko !!! Hata kama ni kwa nia nzuri hiyo inajenga taswira gani kwa jamii ya Tanzania ambayo asilimia kubwa inahitaji elimu, elimu, elimu sio ya darasani tu hata ya kuchanganua mambo.
 
Back
Top Bottom