Kama ningekuwa na uwezo wa kuwashauri UKAWA, ningewashari wakubali matokeo. Huwezi kuoa siku hiyo hiyo na kutarajia kupata mtoto siku hiyo hiyo na kumwandikisha shule siku hiyo hiyo. Hata Mbuyu ulianza kama Mchicha, EL amewasaidia kuongeza idadi ya % ya kura za Urais huenda hata wabunge wa viti maalum wataongezeka, hiki sio kitendo cha kubezwa, ndege aliyeko mkononi ni bora zaidi aliyeko juu ya mti. Kitendo cha UKAWA kuungana katika uchaguzi huu kimewapatia nguvu na wamefanya vizuri sana ikilinganishwa na chaguzi zilizopita. Hata hivyo, imeshuhudiwa muungano huu kutoheshimiwa miongoni mwao wenyewe kiasi cha kusimamisha wagombea wawili kutoka vyama shirika kitu ambacho kimewachanganya baadhi ya wapiga kura kutoamini kama kweli ni muungano wenye tija, na wengine kuchanganya kura na kusababisha wagombea kushindwa; Katika hali kama hii, UKAWA wanapaswa kuchukua changamoto zilizojitokeza na kuanza kuzifanyia kazi kuanzia leo ikiwa ni pamoja na kuimarisha Muungano wao kwa malengo maalum. Kitendo cha kugomea matokeo hakitakuwa na tija kwa sababu Rais akishatangazwa ataanza kutumia ngivu zake za Urais nao kuendelea kulalamika bila kuhudumia wapiga kaura wao kama ilivyotokea mwaka 2010 walivyogoma kutomtambua Mhe. JK, lakini mbona JK amekuwa Rai hadi leo.
Aidha, wahakikishe Chama kinakua na taswira ya Kitaifa ili Watanzania wote wajione kama sehemu ya Chama ingawa kiuhalisia inaweza isiwe hivyo. Hebu fikiria kuhusu CCM Meneja Kampeni Alhaji Bulembo - kutoka Mara; Katibu wa Itikadi na Uenezi - Mtwara; Katibu Mkuu wa Chama - Arusha; Mwenyekiti wa Chama - Pwani, Makamu Mwenyekiti - Iringa. Katika hali kama hii watu wengi wanajiona kama sehemu ya chama kwa mfano wakiwa na mkutano wa Kampeni Musoma, Wanamusoma wakimwona Bulembo wanajiona kama sehemu ya Chama hata kama kiuhalisi sio hivyo. Sasa Angalia kwa CDM - Mwenyekiti - Arusha; Meneje wa Kampeni - Arusha, Mkurugenzi wa Fedha - A, Komu; huko huko !!! Hata kama ni kwa nia nzuri hiyo inajenga taswira gani kwa jamii ya Tanzania ambayo asilimia kubwa inahitaji elimu, elimu, elimu sio ya darasani tu hata ya kuchanganua mambo.