Ni njia zipi unaweza tumia kuepuka, kupunguza na kuondoa kabisa msongo wa mawazo 'stress'

Ni njia zipi unaweza tumia kuepuka, kupunguza na kuondoa kabisa msongo wa mawazo 'stress'

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Ni aina ipi ya stress unapitia kiasi kwamba imekua ni changamoto inayo tatiza baadhi ya mafanikio katika kazi, biashara, masomo, familia na majukumu yako mbalimbali mengine.

Ladies and gentlemen, kama hutojali, unaweza kushirikisha familia hii pana ya JF mbinu mbadala na namna ambavyo unajikwamua na kasumba hii inayotrendi sana miongoni mwa watu wengi tu nchini...
 
ni aina ipi ya stress unapitia kiasi kwamba imekua ni changamoto inayo tatiza baadhi ya mafanikio katika kazi, biashara, masomo, familia na majukumu yako mbalimbali mengine...

ladies and gentlemen, kama hutojali,
unaweza kushirikisha familia hii pana ya JF mbinu mbadala na namna ambavyo unajikwamua na kasumba hii inayotrendi sana miongoni mwa watu wengi tu nchini...
Umesomesha kwa kuuza hadi mashamba na watoto hawana ajira na una Zeeka kwa kasi halafu unasikia ufisadi toka kwa viongozi ukimwagwa hadharani na Mpina!

Kwanini usife kwa sonona!!? future ya watoto haielweki!!?
 
Silaha muhimu za kuepukana au kupunguza stress maishani mwako:-
1. Jifunze kushukuru kwa kila jambo
- hii itakupa Tumaini hata katika changamoto.
2. Epuka kuwa na haraka ya vitu, mali au mambo yaliyo nje ya uwezo wako. Tumia mchakato na muda kuvifikia.

3. Maisha ni "Leo" hivyo jaza Leo Yako kwa furaha na shukrani🙏
4. Anza kuondoa au kujiepusha na vyanzo vya stress zako mfano, mpira wa miguu, kamali, ngono, ulevi n.k

5. Kauli hii ikae kichwani mwako "HILI NALO LITAPITA"
- Hii ndiyo nguvu yangu inipayo Tumaini na tahadhari. Ukiwa katika majonzi tambua kuwa yatapita vivyo hivyo ukiwa katika furaha tambua nayo itapita maana ni ya kitambo tu!
 
Stress ni mawazo, na akili ya mtu haiwezi kukaa bila kuwaza hata kwa sekunde moja tu, hivyo njia sahihi ni kuingiza mawazo mapya ambayo hayawezi kukufanya uwe katika hali ya kukosa utulivu na amani.

Mfano kuwaza mambo mazuri ambayo umefanya au unataka kufanya, hiyo itasababisha mawazo mabaya kupotea akilini. Hakuna njia nyingine ya kuondoa stress zaidi ya kubadilisha mawazo kutoka negative na kuhamia Positive.
 
Binafsi hua najichanganya sehemu zilizochangamka, Ila jaribu hizi huenda zikakusogeza.
 

Attachments

  • Screenshot_20240619-213613_1.jpg
    Screenshot_20240619-213613_1.jpg
    30.8 KB · Views: 6
Back
Top Bottom