Ni nyimbo gani kila ukiiskiliza inakukumbusha mbali??

HBC 2000 na nyimbo za bendi zote zilipendwa (Msondo,DDC mlimani park, Kimulimuli jaz band,Tankati almasi,urafiki jazz,Kilimanjaro band,)
 
Na nikisikia ile ya Ndoa Ndoano ya Msondo Ngoma inanikumbusha mbali sana.
 
Au nikisikia Chungwa Special ya African Revolution wana Tam Tam nakumbuka mbali kweli.
 
Kuna wimbo sijui in wa les wanyika unaitwa Pamela..nakumbuka 1998 muda kidogo baada ya mama kufariki baba akiumba kwa kufuatilzia unavyoimbwa kwenye radio huku ananilisha chakula ili nile chakula cha kutosha. Mpaka Leo nikiusikia nakumbuka hicho kipindi
 
Wimbo wa manfongo "zamu ya Nani" nakumbuka baba enzi za uhai wake akishautwika akifika maeneo ya home anaanza kuimba icho Kipande Cha zamu ya Nani leo ataimba mpaka anaingia ndani.

Kuna wimbo wa richi mavoko "kokoro" nao alikua akiutwika lazima acheze kile kipande Cha aaaahh atacheza Hadi chini na mjuu wake tulikua tunaenjoy Sana..R.i.p Dady

Wimbo wa TI "whatever you like" unanikumbusha ex wangu mmoja alikua anapenda Sana kuniimbia hapo nimevaa t-shirt yake na kofia anaimba tunafurahi ...Rest in peace Monte
 
Tausi ndege wangu, ndege wangu wa fahari, ndege umekwisha mali, sasa watafakari.
wapita watu wawili, wameleta uramali, sasa tuko mbali mbali, sasa tuko mbali mbali.

Nimeandika sababu nimekumbuka mbali[emoji4][emoji4][emoji4]
 
[emoji45]
 
Masudi amekua jambazi. Nakumbuka long time mshua ananifundisha jinsi ya kupiga pasi nguo siku za j2 na mida hiyo ya mchana RFA ndo wanapiga zilipendwa. Rest in peace fella, ulinifunza mengi.
 
Elimu Dunia - Daz
Washikaji walikuwa wakija nigongea Night kali...

Kamanda amka twende tukausake UTAJIRI...

Hata kwa njia zile ambazo sio halali...

Nikakubali, nikawa silali...

Nafanya vile AKILI yangu ilivyonituma...

Navunja Mlango hata kwa jiwe FATUMA...

Yoyote alioleta ubishi kutoa MALI alitolewa UHAI...

Nilichokuwa nkikitaka kwake kwanza ni MASILAHI...

Maasi yangu mwisho yakaongezeka...

Habari kwenye Vyombo vya DOLA kote zikafika...

Matangazo kwenye MAGAZETI sasa yakaandikwa...

Jambazi MUHALIFU anatafutwa...

Na DONGE NONO litatolewa endapo atakamatwa...

Huwezi kuamini kweli AROBAINI zake MWIZI...

Siku hiyo kwenye KAZI nimenasa KITANZI...

Naishia GEREZANI...
 
Daaaah Aisee hili pini daaah. Maisha ni safari. Mungu asante
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…