Ni pesa gani huwa unazikumbuka ukifulia?

Hamsini hamsini na Mia nilizokua nanunulia ice cream za maziwa.
 
Nilipiga dili halali kazini nikapata kama laki tatu hivi ilikuwa jumamosi, sikurudi nyumbani nikapitia club moja kuna live band inapiga muda huo. Kuna wimbo wao huwa naupenda sana, nikamwita mwanamuziki mmoja kumuomba waupige. Akaniambia mmoja wa waimbaji wa wimbo huo hakuja anaumwa na hakuna mwimbaji mwingine aliefanyia mazoezi kipande chake hivyo hawatoweza kuupiga.
Sijui nilipanda na mzuka gani nikamwambia nitawapa kila mwanamuziki elfu kumi, lineup ya bendi nzima ilikuwa na wanamuziki 12. Yule mwanamuziki akamuita kiongozi wake wakaa chemba wanateta huku wakiniangalia mimi. Baada ya muda nasikia wimbo wangu unapigwa ila kile kipande cha mwanamuziki asiekuwepo kiliwasumbua ila walitumia uzoefu tu. Ikabidi nijumuike jukwaani kutimiza ahadi yangu. Ilinitoka kama 120,000/=. Ile pesa naikumbuka mpaka kesho ingawa sikuipatia tabu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu hii pesa hata mimi sitaisahau japo sijaitoa mimi
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu ulikuwa umelewa nini
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Ulijiona papaa ghafla
 
2016 Nilipiga finger kwa wallet ya hubby! 200k! Yaan unaiba huku una hasira hatari moyo umejaa balaa.. nikaimbiza yoote kwa kikoba..sikuambulia chochote..kifup nami nikadhulumika! Sitak Tena kuiba hela mie!
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mkuu hii pesa hata mimi sitaisahau japo sijaitoa mimi
Kila zinapofika tarehe dume zile tarehe ngumu kwa mfanyakazi huwa nakumbuka sana ile pesa. [emoji3][emoji3]
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mkuu ulikuwa umelewa nini
Hapana wala sikupiga gambe ila sijui ni mzuka gani ulinipata. Nadhani ni ile hela ambayo sikuitegemea kupata kwa siku ile tena nilifanya dili nyepesi sana na dili halali.
 
[emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] Ulijiona papaa ghafla
Toka siku hiyo nikawa nafahamika na wanamuziki wa ile bendi, kila nikihudhuria show zao wananifuata wanipige mzinga. Hawakujua kama ile ilikuwa ni zali lao tu, nikaacha kwenda kwenye live show za bendi hiyo bendi ilikuepuka usumbufu.
 
1.Nilijichanga nikanunua bodaboda ya biashara ile hela japo niliuza lakini najutia mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…