Ni pesa gani huwa unazikumbuka ukifulia?

Ni pesa gani huwa unazikumbuka ukifulia?

Nilipiga dili halali kazini nikapata kama laki tatu hivi ilikuwa jumamosi, sikurudi nyumbani nikapitia club moja kuna live band inapiga muda huo. Kuna wimbo wao huwa naupenda sana, nikamwita mwanamuziki mmoja kumuomba waupige. Akaniambia mmoja wa waimbaji wa wimbo huo hakuja anaumwa na hakuna mwimbaji mwingine aliefanyia mazoezi kipande chake hivyo hawatoweza kuupiga.
Sijui nilipanda na mzuka gani nikamwambia nitawapa kila mwanamuziki elfu kumi, lineup ya bendi nzima ilikuwa na wanamuziki 12. Yule mwanamuziki akamuita kiongozi wake wakaa chemba wanateta huku wakiniangalia mimi. Baada ya muda nasikia wimbo wangu unapigwa ila kile kipande cha mwanamuziki asiekuwepo kiliwasumbua ila walitumia uzoefu tu. Ikabidi nijumuike jukwaani kutimiza ahadi yangu. Ilinitoka kama 120,000/=. Ile pesa naikumbuka mpaka kesho ingawa sikuipatia tabu.

Hahaaa jaman pesa inaushetani kiukwel mim nikiwa na mtungi wangu kichwani nimefanya upumbavu sana.
Napenda sana kukaa counter ile wanapiga nyimbo unaipenda utawanunulia wahudumu wote ndani vinywaji na dj ujue mtu anaweza kudhani ni sifa lakn sio kwel jamn.

Sema nikifulia unakuta siku hiyo nataka kuvaa shart au suluri flani nakuta bill ya kibabe ni clear na sina pesa hapo nafyonza mpaka basi.
 
  • Thanks
Reactions: amu
Forex daaahh niliambiwa nitadownload pesa kama unavyodownload video youtube....kilichonikuta sasa, ni siri yangu na Muumba wangu...sijui kwann umenikumbusha mkuu
 
Back
Top Bottom