Kabisaaaaaaaa Babu, na mimi nikiangalia hapo, Mkoloni hakucheza kiume kabisa.
Haiwezekani mtu hakupendi halafu aendelee kufanya na wewe shughuli za maendeleo bwana.
Tena mi namsifu kwa jinsi alivyokubania mwanzo, manake wakati mwingine biashara au ishu muhimu za maendeleo, ukishaingiza mapenzi ndani yake, wala hazifanikiwi vizuri. Bora alivyogoma mambo yakakaa sawa kwanza. Sasa we mkoloni ukashindwa kusoma katikati ya mstari.
Kwanza angekua hakupendi angekuchuna, na yeye aanzishe cha kwake mwenyewe, lakini unaona anafanya kwa juhudi, moyoni akijua mpo pamoja. We Mkoloni wewe, acha ukoloni, utakuja kumkumbuka huyu dada nakwambia.