Ni Rahisi Kupata Kazi Serikalini Kuliko Sekta Binafsi?

Ni Rahisi Kupata Kazi Serikalini Kuliko Sekta Binafsi?

Nyie vijana wa law bwana ukiritimba mwingii ila tukiwapa kazi za mahakamani hamtoboagi hata kama kesi ina evidence moja kwa moja. Huwa nasema au mnaharibu makusudi ili mshauri client akate rufaa muendelee kumpiga hela.
Imefika hatua kupeleka kesi mahakamani bora mtu uache.

Unamdai mtu deni la laki 5 ukipeleka mahakamani kesi kama hiyo utatumia laki 8 hadi 1m
 
Duuuuh!
Una degree ya sheria, umeenda law school hivyo wewe ni licensed lawyer, Advocate, legal Consultant, Negotiator, na mengineyo. Hapo unahitaji kuajiriwa ili ulipwe laki 4??

Change your approach kijana, mashirika mengi hayahitaji "employee" bali wanahitaji "business partners".
Law School bado napambana na kimeo ndugu. Ningekua na leseni mambo yangekua angalau kidogo.
 
Hahah, tatizo ni hana kitu tunaita LOCUS STANDI yeye ni mhitimu wa shahada ya sheria tu ambayo haruhusiwi hata kuandaa nyaraka za kisheria.

Hapo ni labda atafute NGO mpya awe mwanaharakati kulingana na mwelekeo wa hiyo NGO. Ila hili nalo sio jambo jepesi maana inahitaji kujitoa hasa sio poa.

Anyway Mkuu Kalamu Nzito upo mkoa gani?

Mimi kukushauri ni fungua akaunti mpya humu JF, tumia majina rasmi na kuwa verified. Alafu tafuta eneo la sheria ambalo utakuwa una research na kuandika huku. Sana sana andikia mambo ya litigation ili uweze kuonesha uwezo wako wa ku research.

Then baada ya muda kama mwaka mmoja anza kuitumia hiyo akaunti kama port folio yako, pia uwe una publish na LinkedIn. Inaweza kukusogeza hatua kadhaa. Humu kuna mawakili kibao na wengi wetu hatupendi kuresearch sana mambo ya litigation sasa unaweza ukajipatia CV nzuri na uhakika wakazi.

Ila usimuige Mendez wewe andika kivyako kwa ubunifu wako ili uweze kutofautishwa.

All the best.
Kaka shukrani sana. Hii idea nzuri sana. Nimekua nikiandika articles mara kadhaa ila sio consistently. Nitalifanyia kazi zaidi. Thank you once again.
 
Je hatuwezi kuboresha MTU akisoma degree awe na sifa za kuwa na muhuri ikiwa issues ni masomo tunayaongeza na field anaenda Kama kawaida inashindika nini
Haiwezekani Mkuu, sababu digrii ya sheria ni academic degree. Alafu mtu haendi shule ya sheria kwa ajili ya mhuri hapana bali anaenda kwa ajili ya kukidhi vigezo vya kupewa leseni ya uwakili.

Ina maana mtu anaweza pia akaenda law school akafaulu na bado asiwe wakili, uwakili anakupokea Mh. Jaji Mkuu na sio kwamba ukienda na kufaulu law school basi tayari ni wakili, hapana haipo ivyo.

Kitu ambacho tunatakiwa kufanya ni kuruhusu watu wenye digrii zingine kuweza kwenda law school kusomea diploma ya juu ya sheria kwa vitendo badala ya kufanya watu waliosoma digrii ya sheria pekee kuweza kusoma hiyo diploma ya juu ya sheria kwa vitendo.

Sababu hata mtu aliyesoma digrii ya sheria akienda pale law school ananlenda kusoma vitu vipya kabisa.

Mtu anaweza akawa na digrii ya sanaa na elimu na akafaulu vizuri kabisa law school. Kama ni mabadiliko basi yawepo kwenye hicho kipengele cha kigezo cha kuweza kujiunga na law school
 
Back
Top Bottom