Okay Kaka! Kusema ukweli sina kumbukumbu nimewahi waambia na kutamkia wanangu kuwa na wapenda.
Ila hata ndugu, huwa wanawaambia mna Baba mzuri sana anawapenda, na wao wanakiri hayo kwa kusema, I dont know how and why, bu haiji tu.
Upo sahihi Kabisa.
Kuna upendo wa Matendo na upendo wa maneno.
Mtoto anaweza akajua unampenda Kwa kuona mambo hayo mawili. Matendo na maneno yako.
Epuka kuonyesha Huduma unazowapa Watoto au MKE kama sehemu ya Upendo, hiyo ni big mistake.
Na epuka kusema kwa mdomo Kuwa unawapenda Watoto kuliko wao wanavyoona.
Hata hivyo Haivutii wala kupendeza Kwa Baba kumwambia "NAKUPENDA"mtoto wake wakiume (kijana). Upendo wa Baba Kwa mtoto utahusu kauli za kumtia moyo Kwa mfano, Kijana wangu wewe unaakili Sana, au ingawaje umekosea lakini ukitulia Kwa wakati mwingine utafanya vizuri zaidi; nakuamini kijana wangu,
Kauli za ujasiri, kama Wewe ni jembe, wewe ni dume la Simba, unatakiwa uwe na maamuzi magumu yenye tija, usiogope bali uwe na tahadhari,
Pamoja na kumnenea maneno mazuri.
Hayo ndio maneno ya upendo, hata usipomwambia nakupenda.
Mtoto wakike, kuambiwa na Baba yake Nakupenda Binti yangu ni Haki yake, Upendo ni Haki ya wanawake, heshima ni Haki ya wanaume. Ingawaje wote Kwa kiasi Fulani huweza kupewa upendo na heshima.
Anachosema Mtoa mada ni zile pigo za kuisakama Saikolojia ya mtoto Kwa kumtolea maneno ya shombo ATI Huko ndio kumfanya awe shujaa wakati ni kumharibu kisaikolojia.