Ni rahisi sana kujifunza Kifaransa

Ni rahisi sana kujifunza Kifaransa

Paragons

Member
Joined
May 3, 2016
Posts
60
Reaction score
47
Umewahi kuwa na ndoto ya kuzungumza Kifaransa kama lugha ya mama? Usikate tamaa, unaweza kuomba mwalimu kwa njia ya mtandao akakufundisha ukiwa nyumbani kwako maana KIFARANSA ukipata mwl mzuri, ni lugha rahisi sana kujifunza. Mwl anaweza kukufundisha ndani ya miezi mitatu ukazungumza kama vile umezaliwa Ufaransa kwa kutumia simu ya mkononi au internet. Ukihitaji ushauri wa namna ya kujifunza lugha hii ukiwa nyumbani kwako, usikose kuwasiliana na mimi au kutazama vipindi vyangu vya Kifaransa Star T.V kila alhamisi sa kumi na nusu jioni.

Kumbuka nchi 27 za Africa zinazungu Kifaransa, tunahitaji kufahamu lugha hii ili tuweze kuwasiliana nao kibiashara au kiplomasia pia, Kingereza na kifaransa ni lugha za kazi za Umoja wa mataifa (UN) hivyo ni vigumu sana kufanya kazi na taasisi za kimataifa bila ufahamu wa lugha hizi mbili. Wenzetu wa nchi jirani walilifahamu mapema, utawakuta kwenye taasisi nyingi za kimataifa kwa sababu ya kuchangamkia lugha nyingi. Watanzania pia tumeamka; Nakushauri usibaki nyuma!

Kwa wanaohitaji kuanza safari ya kuzungumza, kila siku kuanzia j3 nitaweka hapa somo moja, litakukua na maelekezo ya namna ya kutamka.

Ukishindwa kutamka utapiga sim 0673225148 kwa mda nitakaoelekeza.
 
Ina maana mkuu umekuwa fluent kwa miezi mitatu tu kwa kupitia star tv?
 
Ahsante kwa ushauri.

Nivyema ukatupa simple lesson kila siku au kutuwekea baadhi ya vitabu vizuri vya kujifunzia.
 
Nataka Kiitaliano Kuna demu mmoja wa Kirwanda alikuwa akinifundisha kwa njia ya whatsapp, sim nikaja kuipoteza na number ndiyo ikawa mwisho
 
Back
Top Bottom