Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Kile chuo kimenitesa sana mkuu siwezi kukisahau daima japo now nipo sehemu nawashukuru sana kwa kifupi wapo vizuri.
Sidhani kama unanizidi nilisoma HKL nikaenda pale taxation, siji kurudia ni pagumu balaa
 
Pale hakuna anaekubembeleza kuja chuo, kufanya presentation wala chochote. Wewe fanya ufyokolo wako ukitegemea kuna make up test uone utavyorudi kwenu
Yaani Mimi sina hamu nashukuru Mungu nilimaliza salama
 
Pole sana na pale palivyo pa ovyo ni ukiwakuta watu wanakula bata unaweza jiuliza wana maisha gani mazuri, ila ndio kila mtu na ratiba yake
Yaani Mimi sina hamu nashukuru Mungu nilimaliza salama
 
Mimi binafsi naamini katika specialisation ya chuo husika wala sio kugeneralize kuwa Udom or Udsm ni vipanga kwa kila kitu eg kama kuna kozi za afya nitachagua Muhimbili na si chuo kingine kama first choice vivo hvyo logistics &transportation nitaopt kwa wenye fani yao DMI/NIT
 
Nathan Jr, Mkuu una uhakika na unachosema? Una ushahidi wa hizo first class70? Ni kozi gani yenye first class 70? UDOM wanatangaza GPA za wanafunzi siku ya graduation?
 
Nilipoona andiko la mtoa mada hapo juu imenilazimu nitafute kitabu cha orodha ya Graduate mwaka 2016 ambapo mimi ni miongoni mwa nilie-graduate mwaka huo nimetumia nusu saa kuangalia wenye FIRST CLASS kwa mwaka huo, lakini nikajikuta nacheka hadi kufikia kuidharau sana elimu ya Tanzania, kwamba kweli mtu anayejinasibisha kuwa na PTS 12 mara sijui ngapi huko anaweza akasema kama alichokisema na kibaya zaidi wachangiaji nao bila kufanya utafiti kabla hawajachangia pengine kujilizisha Kwa kile ambacho mtoa mada amekisema wameamua kuchangia UONGO wa mtoto mada. Jamani kama tunajinathibisha kuwa wasomi ni vizuri pia tukachangia vitu ambavyo tuna uhakika navyo kwa kufanya utafiti ama kujilizisha hapo tutakuwa tunaendana na sifa jadidi ya sisi kuuvaa uhusika wa USOMI wetu.
Kitu ulichokifanya ndio Utanzania wenyewe sasa.maana umebisha kwenye bishano ili mradi ubishe.ingefaa utoe data kutoka hicho kitabu chako ambazo ni kinyume na za mtoa mada.sasa hapa na wewe umetoa porojo na ndio uhovyo wa elimu yetu ya Tanzania.
 
Nina kila sababu ya kuheshim wazo lako na sina data za kutosha kukupinga maana sijafanya utafiti huo..ila pengne nisaidie kidogo katika ili

1 asilimia 85 ya walimu wanaofundisha UDOM ni wahtim wa UDSM

2 Wakaguzi waitihani wanayofanya wanafunzi wa udom kutoka nje ni kutoka UDSM

3 Wasimamizi wa Chuo kwa maana ya uongoz wa chuo 95% ni wahtim wa UDSM

swali kwann wahtim hawa kutoka Chuo bora ambao ndio college mate wenzio ndo mazao yawe ovyo? Je tafsiri yake na ww huduma unayotoa huko ni mbovu?

Ningeshawishika kukubal kama tu ungeonesha wahtim ndiyo wabovu pamoja na kutoka GPA ndogo lakini tuhuma yako ni walimu hawa kutoa GPA kubwa.
Wewe Nathan Jr njoo ujibu apa
 
Mkuu una uhakika na unachosema? Una ushahidi wa hizo first class70??Ni kozi gani yenye first class 70? UDOM wanatangaza GPA za wanafunzi siku ya graduation?
Kumbe wewe upo upo tu nimesema wanatangaza? Au wanataja tu idadi ya ufaulu, then unaleta ubishi
 
Wahadhiri wengi wanaofundisha UDOM wametoka UDSM, SUA, ARU, na MZUMBE na ufundishaji wao ni ule ule so hapo kwenye GPA wanatoa kwa mfumo upi? Back ni 2012 First class UDOM zilikua 6 kati wa wahitimu 6572.
 
Hizo 1st class 70 za UDOM zinatokea college gani?? Informatics zipo ngapi?
Wahadhiri wengi wa UDOM wametoka UDSM, SUA na MZUMBE sasa ufundishaji unatofautiana kikubwa kitu gani
 
Wahadhiri wengi wa UDOM wametoka UDSM, SUA na MZUMBE sasa ufundishaji unatofautiana kikubwa kitu gani
Hakika hawali nasikia hizo propaganda niliamini katika hii dhana, baada ya kwenda pale UDOM nilipokuwa nasoma wasifu wa walim wangu wote walionifundisha toka Mwaka Wa kwanza mpaka Wa tatu ni mmoja tu alikuwa kahtim kutoka Chuo cha SUZA ila walo baki wote ni wahtim wa UDSM na la kushangaza walim wangu hao weng waliokuwa si madaktari walikuwa ni wanafunz wa UDSM, nikawa najiuliza why UDOM isemekane kuwa na wahitimu wabovu ili khali wanaandaliwa na wahtimu kutoka Chuo bora? Nikafanya tafiti zangu kidogo nikabaini haya

1. UDOM ina miaka kumi toka kuanzishwa kwake na iko katika 5 bora ya vyuo hapa nchini na mwaka jana nimeona imekuwa ya 2 kwa hapa Tanzania. Vyuo vingine hivyo vinavyosifiwa vimeanzishwa miaka kenda ilo pita tena kabla ya kuzaliwa, ambapo wahitimu wake ndio wataalamu na sisi wa UDOM tunarejelea maandiko yako katika soma yetu, kama kasi ndio hiyo unategemea nini

2. Kwakuwa walimwengu wengi huamini kwa kurithishwa hivo sikupata shaka juu ya ubora huu kubak katika dhana ya kurithishwa kwani walishaaminishwa kuwa chuo bora ni UDSM, SUA, MZUMBE n.k leo kuona na UDOM inaanza kuvishika mkia si rahisi wakaamini.

3. Vyuo vyote nchini hakuna chenye kuchukua wanafunzi wanaoweza kufikia hata nusu ya idadi ambayo UDOM inaweza kudahili, sasa kama uelewa wa ubora upo katika idadi na alipokuwa darasan aliamin Elimu ya juu ni ya wachache si rahisi kukubali kuwa UDOM ni miongoni mwa vyuo bora

4. Wahenga hunena ya kuwa unaposhindwa kushindana na mshindani wako amua kuungana naye, kauli hii ni ngumu kumeza na maamuzi yake lazima yawe kama ya mfa maji kwanza. Atatapa tapa mwishowe atasalimu amri
 
josee88,
Mkuu mpaka sasa hujua mantiki ya uzi wangu? Hapo u great thinker wako uko wapi?

Hii nimeileta makusudi sana kuona mtazamo wa watu na mawazo ya watu juu ya ku urgue kwenye masuala ya msingi, kukosoa mtoa mada kwa data, kuleta uthibitisho mbali mbali,

Badala yake waliotoa uthibitisho na kuchangia kama wasomi ni wachache sana,

Lakin sababu ya kwani ni nimeanzisha uzi huu?

1. Kuangalia ni watanzania wangapi bado wana mawazo potofu kwenye masuala ya kuamini chuo , bila kuangalia chuo kina deal na nini, ni yaan Ulinganishe DUCE na MUHIMBILI? Automatically hata marks zao hazitaendana maana kuna baadhi ya course hazishabihiani hata kulinganishwa si vema,

2. Nimetaka kujua je hawa tunaowaita wasomi hapa JF wameshapunguza kusifia vyuo walivyosoma bila kufanya utafiti juu ya Vyuo vingine?

3. Bado kuna ulimbukeni wa kudhaniwa chuo kikuu ni kimoja tu UDSM, vingine ni usindikizaji?

4. Pia nilitaka kuona kama kuna atakaye leta maelezo thabiti juu ya CV za walimu au wahadhiri wa vyuo husika kwa sifa zao, bila tu kukaa kubishana kama watoto wa chekechekea

5. Nilitegemea kuona kuna mapendekezo kadhaa juu ya nini kifanyike kuokoa elimu yetu ,yaani ni Upuuzi kujisifia umetoka UDSM wakati kimataifa ni ya 17,300 kwa ranking,

Ni hayo tu
 
Mimi binafsi naamini katika specialisation ya chuo husika wala sio kugeneralize kuwa Udom or Udsm ni vipanga kwa kila kitu eg kama kuna kozi za afya nitachagua Muhimbili na si chuo kingine kama first choice vivo hvyo logistics &transportation nitaopt kwa wenye fani yao DMI/NIT
Safi sana uzi wangu nime u UPDATE
 
Watu wanaibeza sana UDOM ila nimekuja kufuatilia historia ya collage of informatics (sio chuo kizima) mwaka huu wameondoka wanafunzi 178 kwa collage moja pili toka collage hii kuanzishwa ilichukua muda kupatikana first class, binafsi nilikwepa kuomba DIT nikiamini huko mambo magumu ila nilipokuja hapa nimeona nitulize akili na nipunguze bata nisome
 
Watu wanaibeza sana UDOM ila nimekuja kufuatilia historia ya collage of informatics (sio chuo kizima) mwaka huu wameondoka wanafunzi 178 kwa collage moja pili toka collage hii kuanzishwa ilichukua muda kupatikana first class, binafsi nilikwepa kuomba DIT nikiamini huko mambo magumu ila nilipokuja hapa nimeona nitulize akili na nipunguze bata
Hatujaelewa mkuu eleza vema
 
[QUOTE="Nathan Jr, Nimekuelewa sana kiongozi, ninakushukuru sana katika hili, wazo lako ni sahihi tena kwa uekevu, hata mimi nimejikwaa kwa ugusi wa mtazamo, ila kama pia umesoma ujumbe wangu utakuwa umebaini kuwa pia hata mimi siko katika mrengo huo wa kurithi ubora, asante kiongozi
 
Nimekuelewa sana kiongozi, ninakushukuru sana katika hili, wazo lako ni sahihi tena kwa uekevu hata mimi nimejikwaa kwa ugusi wa mtazamo, ila kama pia umesoma ujumbe wangu utakuwa umebaini kuwa pia hata mimi siko katika mrengo huo wa kurithi ubora, asante kiongozi
Sawa sawa mkuu nimekuelewa
 
josee88, kaka unasema kweli mimi nimekuja UDOM mwaka huu nikijua mambo ni lele mama ili nile bata but kulingana na utafiti niliofanya few days kwenye course ya Informatics ni kujikana
 
Back
Top Bottom