Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Ni rahisi sana kupata first class Ukiwa UDOM kuliko UDSM, IFM, SUA na Mzumbe. Inaonekana Walimu wa UDOM wanafundisha sana

Mkuu ujue vyuo vinatofautiana kuanzia kwenye;
Minimum pass marks yaan alama C kuna baadhi 45% inatosha kuna baadhi hadi ufike 50%

Pia namna wanavyo calculate grade points kwa kila somo hapa kuna vyuo ukiscore alama A tu wewe tayari una points zako 5 haijalishi iwe A ya 75% au 100%

Wakati SUA kila alama unayo score katika somo ina specific points mfano mwanafunzi aliye na A ya 100% atapata 5 points wakati mwenye 90% atapata 4.5 points hali kadhalika mwenye A ya 75% atapata 4 points

Kwahiyo ukija kwenye kucalculate average grade point (GPA) lazma utakuta utofauti

Hivyo basi unakuta kupata first class ni rahisi kwa baadhi ya vyuo na ni ngumu sana kupata kwa baadhi ya vyuo na hii husababishwa na huo utofauti nilio eleza hapo juu
 
Nathan Jr, Mkuu nenda na wewe ukasome uchomoke na first class. Kwa ufupi UDOM kuna malecture wanaotoka UDSM na SUA.
 
Hahaha vimitihani sio? Siwatetei UDOM. Embu mpeleke mwanao kafanye hivyo "vimitihani" tuone itakuwaje
Hujui UDOM wewe yan vimitihani wanavyotoa vya kipuuzi, hata mtoto mdogo anajibu ni mitihani Lege lege, ukitaka iundwe Bodi ya Mitihani ya Vyuo Vikuu na mtihani wapige mmoja na UDSM, IFM IRDP au SUA utaona maajabu,
 
Mnaoidharau UDOM nawapa pole sana, naiman hamjafanya utafiti na pia mnadhirisha nyie wasomi makanyanja sana
 
Mnaoidharau UDOM nawapa pole sana, naiman hamjafanya utafiti na pia mnadhirisha nyie wasomi makanyanja sana
Waambie mkuu. Maprofesa wa UDSM wana mentality za kizamani kwamba ukimfelisha mwanafunzi ndipo unaonekana wa maana.
 
Naweza kubali kule UDSM wali discko watu wengi sana mwaka jana was masomo
I'm sure tena wanabana kukomoa ooooh wewe fanya research yako uone ukifaulisha sana unaulizwa kwanini wanafunzi wamefaulu sana.
 
Mjadala mzuri sana.
Ila mimi najua watu wana kasumba zinazo fanana.
Hivyo mwanafunzi na mwalimu wa UDOM wanafanana kasumba. Nimesoma UDOM. Wakati tuna graduate 2012 zilikuepo first class 3 tu BCOM, darasa letu walidisco watu zaidi ya 10, mtoa mada atuletee data hapa ili twende kisomi zaidi
 
josee88, Wanaoponda UDOM wanaponda kwa upya was majengo yake na sio content .

Aidha ni washamba wa elimu au ni academic sycophants
 
Ukihudhuria mahafali Yao vyuo Tajwa hapo juu
UDSM ,IFM,SUA ,MZUMBE Si rahis kusikia wanatangaza wanafunzi wenye first class wengi, utakuta wanne au watano hawazid kumi mara nyingi,

Lakin ukienda UDOM utakuta first class wapo karibia 70 kwa course zote ,

Sababu nini?
Udsm na IFM hawana walimu competent kama UDOM au walimu wao wanagawa marks ovyo? Au hakuna utaratibu wa kubana sana wanafunzi kama vyuo vingine?

UPDATE
Wakuu mpaka sasa humjajua mantiki ya uzi wangu? Hapo u great thinker wenu uko wapi?

Hii nimeileta makusudi sana kuona mtazamo wa watu na mawazo ya watu juu ya ku urgue kwenye masuala ya msingi, kukosoa mtoa mada kwa data, kuleta uthibitisho mbali mbali,

Badala yake waliotoa uthibitisho na kuchangia kama wasomi ni wachache sana,

Lakin sababu ya kwani ni nimeanzisha uzi huu?

1.Kuangalia ni watanzania wangapi bado wana mawazo potofu kwenye masuala ya kuamini chuo , bila kuangalia chuo kina deal na nini, ni yaan Ulinganishe DUCE na MUHIMBILI? Automatically hata marks zao hazitaendana maana kuna baadhi ya course hazishabihiani hata kulinganishwa si vema,

2. Nimetaka kujua je hawa tunaowaita wasomi hapa JF wameshapunguza kusifia vyuo walivyosoma bila kufanya utafiti juu ya Vyuo vingine?

3. Bado kuna ulimbukeni wa kudhaniwa chuo kikuu ni kimoja tu Udsm, vingine ni usindikizaji?

4. Pia nilitaka kuona kama kuna atakaye leta maelezo thabiti juu ya cv za walimu au wahadhiri wa vyuo husika kwa sifa zao, bila tu kukaa kubishana kama watoto wa chekechekea

5. Nilitegemea kuona kuna mapendekezo kadhaa juu ya nini kifanyike kuokoa elimu yetu ,yaan ni Upuuzi kujisifia umetoka UDSM wakati kimataifa ni ya 17,300 kwa ranking,

Ni hayo tu

KUNA WATU WAMEANZA KUBEZA ELIMU YANGU AU MNATAKA NA VYETI KABISA?

KATORO PRIMARY SCHOOL 1992-1998
Nikafaulu tulitoka wawili kata nzima elimu bado ni elimu kwenda TABORA BOYS 1999-2002
Mwanaume nikakung'uta PTS 12
Nikajoin MINAKI HIGH SCHOOL
2003-2005 EGM


Nikakung'uta 6 PTS kwenda zangu
B.COM IN CORPORATE FINANCE UDSM


Alafu mtu una elimu ya kuunga unga unajilinganisha na mimi,

Uzi huu nimeuleta makusudi kutrick point fulani ambayo vyuo vingi vinagawa marks za free,

Hatimaye tunazalisha wasio competent kazini

Nathan JR
Kumbe ni "Nshomire"!! Endeleza jadi Full kujisifia tu, wewe mbona hujatowa hata reference moja ya andiko lako?
Naona kila kitu una-quote "MAKUSUDI"
 
WALE MLIOMALIZA UDSM MMEPATA AJIRA ???? MAANA WASOMI WA UDSM HUA TUNAKUTANA NAO HATA FIELD WABOVU KWELI KAZI YAO SIFA TUU MTU UNAKUTA KASOMEA DUCE AU MUCE HATAKI KUSEMA AMESOMEA MUCE UTASIKIA UDSM UDSM, THEN ID YAKE UTAONA MKWAWA COLLEGE OF EDUCATION. ACHENI USHABIKI NA SIFA ZA KIJINGA WEWE KOMAA TUU UKIONA MWENZAKO KAPATA GPA ESPECIALLY KWA VYUO VYA SERIKALI UJUE AMEKAZA SIO UTOTO LABDA HIZI ST. FLAN JAPO SINA UHAKIKA MAANA WANASEMA NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK. KIUJUMLA WASOMI WA UDSM WAPO WANAOJIELEWA SANA NA WANAFANYA VITU VYENYE IMPACTS KATIKA JAMII LAKINI WAPO WENGI MAZWAZWA WAMEBAKI SIFA TUU AJIRA HAWANA COMPETENCE HAWANA. KUNA JAMAA MMOJA WA UDSM ALIPAMBANA NA FRIEND WANGU FIELD SHULENI, MWANZO JAMAA AKAWA ANAJIDAI MPAKA ANAWAAMBIA WANAFUNZI ET MM NIMETOKA UDSM CHUO CHA MAANA HAWA WENGINE MNAONA WAMETOKA VYUO VYA VILAZA TUU. SASA MAPINDI YAKAANZA WA UDSM KAPEWA HKL KUFUNDISHA LANGUAGE NA WA UDOM KAPEWA HGL KUFUNDISHA LANGUAGE FORM SIX. KILICHOTOKEA MKALI WA UDSM AKAWA HAELEWEKI DARASANI WANAFUNZI WAKAWA WANAKAKIMBILIA DARASA LA HGL AMBALO KUNA MDAU WA UDOM NA AKAWA ANAELEWEKA SANA YANI. KIUJUMLA KUNA WATU WAPO COMPETENT NO MATTER KASOMA CHUO GANI NA KUNA WENGINE MAZWAZWA TUU NO MATTER KASOMA WAPI HATA IWE USA. KWAHIYO ENYI WASOMI AMBAO HAMJAELIMIKA ACHENI SIFA FANYENI VITU VYA MSINGI VYENYE MANUFAA KWA JAMII SIO KUSIFIA CHUO NA KUPUUZA VINGINE KAMA USHABIKI WA UEFA
 
Kwanza kabisa nianze kwa kusema kuwa .
Kuwa suala la ufundishaji na ujifunzaji ni suala nyeti sana zaidi ya sana.
Na kama mtu huna taaluma ya masuala ya elimu na ualimu ni ngumu kuelezea bali wengi wataelezea kwa uelewa wa jumla bila kutambua nini wanaelezea.
Wakuu siko hapa kutaja chuo bora ni kipi au chuo ambacho sio bora ni kipi.
Ila nataka watu wafahamu kidogo kuhusu suala la ufundishaji na ujifunzaji na ubora wa elimu.

Sababu kitaaluma ni makosa makubwa kuelezea mambo ya taaluma fulani kiundani bila kujua kile unachokielezea maana mbele za watu wenye taaluma husika unaweza onekana wa ajabu sana.

Kwa kiwango kikubwa nchini kwetu wengi wanayoifahamu elimu kiundani na kitaaluma huwezi kuta wanaongelea ovyo ovyo udhaifu wa taasisi fulani sababu wanajua fika hali halisi ya maana na mfumo mzima.

Lakini wale ambao akili zao ni nyepesi huwa wepesi kuelezea hali hizo.

Labda ni nukuu kauli ya mhadhiri kutoka Chuo kikuu cha Dodoma katika kitivo che elimu ,tena katika kozi ya Pedagogy in teaching .alisema TEACHING IS COMPLEX AND DYNAMIC PROCESS WHICH REQUIRE DEEP AND WIDE KNOWLEDGE TO UNDERSTAND AND EXPLAIN IN THE RIGHT WAY.
Ukitafakari maneno hayo kwa kina utaona kuwa wengi huwa wanakurupuka katika kuelezea Masula hayo ya kitaaaluma sababu Hawajui wakisemacho.
Basi nami namalizia kwa kusema kuwa
MUNGU AWASAMEHE SABABU HAMJUI MLITENDALO.
Kutoka kwa
Mhandisi wa Elimu.
 
Hizo 1st class 70 za udom zinatokea college gani?? Informatics zipo ngapi?
Hivi hawa jamaa wanaongelea udom ipi mbona hawaendani na uhalisia hawatumii experience katika maneno wengi ni ku guess tu na fact za uongo
 
Wewe utakuwa unazungumzia UDOM ya Central African Republic. UDOM ya Tanzania na haswa Idara niliyopo First Class ya Kwanza na pekee baada ya miaka 10 ilipatikana mwaka jana. Lakini sasa... wana UDOM wenye GPA za 2.5 wanawashinda wenye GPA za >4 kutoka vyuo vingine vikiwepo ulivyovitaja inapokuja suala la interview. No Research No Freedom to Speak. BTW huwa Degree classifications hazitangazwi kwenye mahafali. Acheni kusumbua chuo pendwa cha watu.
Exactly kk
Ujue kama mtu haupo ktk madhingira husika lazima uongee pumba Kama jamaa mleta mada
Kikuweli udom pagumu bana harafu swala la gpa ni jitihada za mwanafunzi..
Na uwezo wa mwanafunzi hatu calculate kwa kuangalia gpa tunaangalia content kichwani
 
nasupport asilimia mia moja ingawa umesema umepost kupima watu, but mimi nadiriki kusema Udsm ni kugumu aisee asiwaambie mtu, mimi nina akili nafahamu, ila nimetoka na lower second bcom Accounting ingawa nilikua na one zangu o level na advanced, yani chuo hata nisomeje nilikuwa nasoma kichizi ile second year na third ila naishia b plus hapo ndo nafaulu sana,tena hayo ni yale masomo mepesii kabisaa , ila mengine nilikua nachezea tu B plain na makarai, ila kuna jamaa mmoja kapiga tudarco hapo katoka na second upper yake wakati o level kapiga three na chuo hata alikua hasomi yupo bize na mishe kitaa, yani mimi ndo ningesoma sijui tudarco, ifm ,udom aisee ningepiga first class nna uhakikaaa , ila nataka nikajaribu hiyo ishu, nitaapply course nyingine ya undergraduate nichek itavokuwa
 
nasupport asilimia mia moja ingawa umesema umepost kupima watu, but mimi nadiriki kusema Udsm ni kugumu aisee asiwaambie mtu, mimi nina akili nafahamu, ila nimetoka na lower second bcom Accounting ingawa nilikua na one zangu o level na advanced, yani chuo hata nisomeje nilikuwa nasoma kichizi ile second year na third ila naishia b plus hapo ndo nafaulu sana,tena hayo ni yale masomo mepesii kabisaa , ila mengine nilikua nachezea tu B plain na makarai, ila kuna jamaa mmoja kapiga tudarco hapo katoka na second upper yake wakati o level kapiga three na chuo hata alikua hasomi yupo bize na mishe kitaa, yani mimi ndo ningesoma sijui tudarco, ifm ,udom aisee ningepiga first class nna uhakikaaa , ila nataka nikajaribu hiyo ishu, nitaapply course nyingine ya undergraduate nichek itavokuwa
Ukweli mtupu
 
Back
Top Bottom