Mods! Tafadhari, mada hii haina uhusiano wowote na kabila la mtu, hivyo naombeni sana!
Shalomu Tanzania!
Zamani za mfalume Farao, mfalume huyu wa Misiri kipindi cha yeye kuongoza Misiri' alitoa amri ya kuwauwa watoto wote wa kiume waliotokana na wayahudi wahamiaji wa Kiisraeli katika nchi hiyo!
Lilikuwa ni agizo ambalo liliwatia simanzi watumwa hao wa Kiisraeli katika nchi ya ugeni!
Mfalume huyo, hofu yake ni kuona ongezeko kubwa la wahamiaji hao katika nchi na kwamba wakiongezeka sana, wanaweza kuja kuwatawala wa Misiri, ili kuwadhibiti waisrael kuongezeka na kuwa tishio, basi akatoa amri hiyo ya watoto wote wa kiume watakaokuwa wakizaliwa, basi wauwawe!
Siku moja mama wa kiyahudi, alijifungua mtoto wa kiume, hakutaka kuwakabidhi hao waliopewa amri ya kinyonga vitoto hivyo, basi akatengeneza kisafina na kisha kukaweka kwenye kijito ambacho hutilirisha maji yake kupitia maeneo ya Ikulu ya Farao ambapo watoto wake huogelea humo!
Wakati watoto wa Farao wakiogelea, binti Farao akakiona kile kisafina kikiwa kinaelea kufuata mkondo wa maji, akakifuata na kumbe mlikuwemo mtoto, naye bila hiyana, akakipeleka Ikulu na mtoto yule kulelewa hapo Ikulu, na wao kumpa jina la Musa!
Masikini Farao haukujua kwamba mtoto waliyemlea ndiyo huyo atakayeleta mapinduzi na kuwaokoa wayahudi wote waliokuwa wakitumikishwa na Farao!
Nataka kusema nini! Kupambana na sukuma gang na usijue hasa nani ni sukuma gang ni kujichosha saana
Twende kwenye mada
👇👇
Kwenye mitandao ya kijamii, kumekuwepo na mjadara wa jina (SUKUMAGANG) ambao umedumu sasa takrabani miaka miwili naa, tangu tu alipoondoka aliyekuwa rais wa Tanzania hayati John Magufuli
Kwa kujua ama kutojua, watunzi wa jina hili huwenda hawakujua athari itakayojitokeza mbele, na sasa hata wao ukiwauliza hawajui walilenga nani ndiye awe mwenye jina hilo Sukumagang!
Ukiuliza, Sukumagang ni wasukuma? Wanajibu hapana, bali wanakutajia majina ya mahasimu wao kisiasa!
Mwanzoni kabisa, matumizi ya jina hili lilimaanisha (Wasukuma) hawakujua athari ya jina hilo! Kwa sababu walikuja kugundua, hata kwenye vyama vyao, kuna wasukuma tena wengine ni viongozi wakubwa huko,
JPM alikuwa Msukuma ingawa wengine hawataki kumhusisha na usukuma lakini ni kwa sababu ya masilahi ya kisiasa, kwa sababu wanajua, wakimhusisha na wasukuma, moja kwa moja jina hilo walilolitunga kwa ajili yake, litawajumuisha wasukuma wote wa kanda ya ziwa kwa maana ya mikoa mitano na waliosambaa nchi nzima
wanachokihofu wanasiasa hawa, ni suala Zima la wao kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa kabila hilo kubwa nchini,
Tukirudi upande wa pili, kunawanaosema, hao sukuma gang wanapaswa kudhibitiwa ili wasithubutu tena kushika madaraka ya juu ya nchi hii,
Hoja hii ndiyo yenye maswali mengi yasiyo na majibu hata kwa hao wanaojaribu kusema hivyo,
Ikiwa jina Sukuma gang linaihusu jamii ya wasukuma, Mtu anaposema, Sukumagang hawapaswi tena kushika madaraka ya juu katika nchi, anakuwa anamaanisha nini, ni kudhibitiwa kwa wasukuma wote, kwamba hawatakiwi kuongoza nchi hii kwa sababu aliyekuwa Raisi wa nchi na ambaye amekuwa hasimu wa vikundi haramu nchini tangu tu alipowatangazia vita vya serikali aliyokuwa akiiongoza yeye na vikundi hivyo haramu vya mafisadi alikuwa ni Msukuma?
JE, Sukuma gang hawapaswi kuongoza nchi hii tena, inamaana gani? Kwa mjibu wa madai mapya ya kundi bunifu la kutoa majina kama ambavyo walibuni jina hilo la sukuma gang kuwa, jina hilo halihusiani kabisa na wasukuma, ingawa hata inapotokea ametumbuliwa msukuma, vikundi hivi vya wabunifu wa jina hili vimekuwa vikifanya sherehe kwenye mitandao ya kijamii.
Unajiuliza, ikiwa jina Sukuma gang halihusiani na wasukuma, kwa nini sasa msukuma mmoja akiondolewa madarakani kunakuwepo na shangwe miongoni mwa wabunifu wa jina hili?
Failsafa ya jina hili ni kama imegawanyika, imegawanyika kwa sababu tu ya kimasilahi hasa za kisiasa, ingawa vitendo havijagawanyika! Vitendo vinadili sana na wasukuma na ndiyo maana utaona, kila alitimliwa msukuma kwenye nafasi fulani, inakuwa sherehe kwao
Kuwadhibiti wasukuma ili lengo la falisafa yao itimie ni rahisi kwa sababu wasukuma wanajulikana kwa majina yao, wakijificha kwa majina yao, lafudhi yao itawatambulisha.
Kutumia nguvu kudhibiti Sukuma gang wasishike madaraka, ni kujaribu kukimbiza upepo.
Sukuma gang ukiondoa ubaguzi uliojificha kwenye jina hilo, kundi hili halidhibitiki hata kwa mtutu wa bunduki
Sukuma gang, Wapo kila wizara na kila sector zote za Serikali kwenye ngazi za juu za kati, na huku chini ndio usiseme! Wapo kwenye vyama mbalimbali nchini
Ni ujinga mtu kupigana na kitu kilicho moyoni mwa mtu.
Na mpaka sasa haijulikani ikiwa hata walioshushwa vyeo ndio walikuwa sukumagang na ambao wamewekwa kwenye nafasi hizo kama nao ni wale wale sukuma gang.
Sukumagang ni watu wote walioathiliwa na uongozi wa kuthubutu kufanya, uongozi mashuhuli wa JPM, sasa ni kina nani, Sio wasukuma, wachaga, warangi, wagogo, wamatumbi, wajita, wazaramo na kila kabila.
Kote huko sukumagang wapo wamejaa.
Unaweza kupigana na wasukuma ukawashinda ila sio Sukumagang!