Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni

Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni

john achila mukumwa

Senior Member
Joined
Jan 4, 2024
Posts
142
Reaction score
281
Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu la sindano
kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni

Yesu Kristo alisema, ni vigumu kwa tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni kama ilivyo vigumu kwa ngamia kupita katika tundu la sindano. Je, Yesu alikuwa anarejelea ngamia na sindano halisi?


Kama tunavyoifahamu habari hiyo, ni kuwa mtu tajiri alimfuata Bwana Yesu, na kumuuliza atende jambo gani jema ili aurithi uzima wa milele. Ndipo Bwana akamwuliza, umezishika Amri?

Yule kijana akasema, hizo nimezishika tangu utoto wangu, nimepungukiwa na nini tena? Bwana akampenda sana. Lakini akamwambia ukitaka kuwa mkamilifu, nenda uuze vyote ulivyonavyo, kisha unifuate. Lakini yule kijana aliposikia vile aliondoka kwa huzuni, kwa sababu alikuwa na mali nyingi.

Ndipo Bwana akawaambia wanafunzi wake maneno haya kwenye Mathayo 19:
23 “Yesu akawaambia wanafunzi wake, Amin, nawaambieni, ya kwamba itakuwa shida tajiri kuingia katika ufalme wa mbinguni. 24 Nawaambia tena, Ni rahisi zaidi ngamia kupenya tundu la sindano, kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu".


Maandiko mawili kati ya matatu yanayozungumzia jambo hilo yanafanana. Kulingana na masimulizi ya Mathayo, Yesu alisema: “Ni rahisi zaidi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu" (Mathayo 19:24).

Andiko la Marko 10:25, linasema: “Ni rahisi zaidi ngamia kupita katika tundu la sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu".

Vitabu fulani vya marejeo vinasema kwamba tundu la sindano lilikuwa lango dogo kwenye mojawapo ya malango makubwa ya Yerusalemu. Lango kubwa (main gate) lilipofungwa usiku, lile dogo lilifunguliwa. Inaaminika kwamba ngamia angeweza kupitia lango hilo dogo, baada ya mizigo kuondolewa kwake. Je, Yesu alikuwa anarejelea lango hilo?

Yaonekana hakuwa anarejelea lango hilo. Yaelekea Yesu alikuwa anarejelea sindano ya kushonea. Kwa kuwa sindano za zamani za mifupa na chuma, zimepatikana katika eneo hilo, bila shaka zilitumiwa kwa shughuli za nyumbani wakati huo, ikiwa ni pamoja na kushonea.

Andiko la Luka 18:25 linaondoa shaka yo yote kuhusu maneno ya Yesu, kwa kuwa linamnukuu kuwa alisema: “Kwa kweli, ni rahisi zaidi ngamia kupita katika tundu la sindano ya kushonea (needle’s eye) kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu". Biblia ya Kiingereza iko wazi.

Watungaji kadhaa wa kamusi hukubaliana na tafsiri “sindano ya kushonea” kama ilivyo katika tafsiri ya ulimwengu mpya. Neno la Kigiriki (rha·phisʹ) linalotafsiriwa kuwa ‘sindano’ kwenye Mathayo 19:24 na Marko 10:25, linatokana na kitenzi kinachomaanisha “shona.” Nalo neno la Kigiriki (be·loʹne) kwenye Luka 18:25, linatumiwa kurejelea sindano halisi inayotumiwa katika upasuaji.

Wengine hudokeza kwamba katika mistari hiyo, neno “ngamia” linapaswa kutafsiriwa kuwa ni “kamba”. Neno la Kigiriki (kaʹmi·los) linalotafsiriwa kuwa kamba linafanana na neno (kaʹme·los) linalotafsiriwa kuwa ngamia. Hata hivyo, neno la Kigiriki linalotafsiriwa “ngamia,” wala si lile linalotafsiriwa “kamba,” ndilo limetumiwa kwenye Mathayo 19:24 katika maandishi ya zamani ya Kigiriki ya injili ya Mathayo yaliyopo leo.

Yasemekana kwamba mwanzoni Mathayo aliandika injili yake katika Kiebrania na huenda yeye mwenyewe aliitafsiri katika Kigiriki. Alijua hasa yale Yesu aliyosema, hivyo akatumia neno linalostahili.

Hivyo basi, Yesu alimaanisha sindano halisi na ngamia (mnyama) halisi.

Yesu alitumia mifano kama hiyo ili kukazia jambo fulani lisilowezekana.


Lakini, je, Yesu alimaanisha kwamba hakuna tajiri, anayeweza kwa vyo vyote kuingia katika Ufalme? La hasha, kwa kuwa maneno ya Yesu hayakupaswa kuchukuliwa kihalisi. Yesu alitumia usemi uliotiwa chumvi ili kuonyesha kwamba, kama vile ngamia halisi asivyoweza kupita katika tundu la sindano halisi, ndivyo tajiri asivyoweza kupita katika Ufalme, ikiwa ataendelea kushikamana na mali zake na kutotanguliza Yehova maishani mwake (Luka 13:24; 1Timotheo 6:17-19).

Mtu tajiri anayependa mali zake zaidi ya mambo ya kiroho hawezi kutarajia kupata uzima wa milele katika mpango wa Ufalme. Hata hivyo, matajiri fulani walipata kuwa wanafunzi wa Yesu. Mifano ni Yusufu wa Arimathaya na Zakayo mtoza ushuru (Mathayo 27:57; Luka 19:2, 9). Hivyo, tajiri ambaye anatambua uhitaji wake wa kiroho na anayetafuta msaada wa Mungu, anaweza kupata wokovu kutoka kwa Mungu.

Lakini, kwa vyo vyote vile, tunapaswa kufahamu kiini cha ujumbe ambacho tunakipata katika habari ile. Pale tunaona Bwana alikuwa anajaribu kutueleza ugumu uliopo kwa watu wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa mbinguni, ndipo akatumia mfano ule ili kuuwekea msisitizo zaidi.

Ni sawa tu na pale aliposema “toa boriti iliyo katika jicho lako, ndipo uone vema kutoa kibanzi kilicho katika jicho la ndugu yako (Luka 6:41-42). Lakini kiuhalisia kibanzi au boriti haviwezi kukaa katika macho ya mtu.

Ili kufikisha ujumbe kwa uzito zaidi, ilimpasa Yesu atoe mifano ya namna hiyo, ambayo kiuhalisia haiingia akilini, kama vile mahali pengine aliposema, “mnachuja mbu na kumeza ngamia” (Mathayo 23:24). Na ndivyo ilivyo katika habari ya tajiri, ngamia na sindano.
 
Ulivyosoma Kama Ngamia ukichukulia ni mnyama wa Jangwani ... Apostle umeliwa kichwa ni Uzi.
 
Back
Top Bottom