Ni rasmi sasa kwa watu wa mkoa wa Kigoma ni rukra kuvaa chapa (logo) ya JWTZ

Hawa
Hawa msimu ujao hawatoboi wataishia kubishana tu, itakuwa timu ya kwanza kushuka daraja.
 
Kelele zote zile za akina ZZK kumbe timu ya jeshi 🤣🤣🤣. Hao hata wakiamua kuipeleka Ruvu wanaupeleka tu.
 
Morogoro itapatikana duka gani.
Napendaga jezi zisizo na machata chata mengi.
 
Jezi zinapatikanaje kwa tulio mikoa mingine?.
Ninahitaji mbili
 
Bei zake???
 
timu itakayofungwa 8, 7, 9, 6, chache 5. Timu inategemea uchawi.
 
Ndio nini sasa? Sasa, kuvaa logo ya jw, kuna, saidia nini? Unajivunia hili jeshi, kwa lipi waliofanya? Kuna, watu richa ya kuwa tupo 2023! Wao bado wanaishi 1980!!!
 
Muombe Moderator akurekebishie title ya thread
 
Kuna wazee wa Mrumbani Ujiji wacheza Ludo maarufu mashefu , raha yao wazitungue Yanga na Simba tu! Hizo mechi watalala Lake Tanganyika Kisha makaburini Kaza Roho! Wataroga kuliko uchawi wenyewe!

Hii timu ya Mashujaa kuifunga kwao lazima uwe na mganga toka Sumbawanga au Nigeria!

Ila wakiweka nyasi bandia na taa uwanja utakuwa kama ulaya! Wakimbizi wataongezeka!

Last time 1994 niliona kama vile ule uwanja ulianza kutumika bila kukamilika kwenye majukwaa ila sijui hali ikoje kwasasa! Waliufisadi!

Wana Kigoma wana raha sana ila wajipange uganga wa maana, pia wapewe ndege ya jeshi Ili wasafiri bila kuchoka wasifungwe ugenini Kwa uchovu , ligi ngumu sana hii NBC premier , wasijekuwa timu ya msimu mmoja!!

Pia ikiwezekana waazime wachezaji mamluki toka Congo, Burundi na Rwanda ni ndugu zao.
 
Timu gani hilo kazi ukorofi tu na ubabe ubabe,mjiangaliee sana mtakuja kula 10 bila hapo hapo kwenu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…