Ni red flags zipi ukiziona kwenye mahusiano mapya unaanza kutafuta mlango wa kutoka?

Ni red flags zipi ukiziona kwenye mahusiano mapya unaanza kutafuta mlango wa kutoka?

She's very lucky to have you, km huna, Mungu akupe mke mwema ili uenjoy mahusiano yako. Vijana wengi hawajui raha ya kuwa kichwa ktk uhusiano. Ndo mana wanahangaika km kuku vishingo!
Aisee ila na nyie tatizo lenu hamtimizi majukumu yenu. Boss akikohoa mnakurupuka ila mume mnamnyanyulia mdomo.
 
Though hainihusu
1. Mwanaume mchafu (kuna tofauti ya kuwa rough na mchafu) kuna wakaka ni wachafu mpaka unajiuliza anaishije
2. Mwanaume bahili na mbinafsi huyu hata kwenye ndoa hamuwezi kuishi kama team
3. Mwanaume mwenye mfumo dume wa kijinga usio na tija wa hivi hata kushauriana inakua nongwa wanakuaga much know sana
4. Mwanaume mwenye verbal na physical abuse yani hawa kukupa sonana, ulemavu au kifo ni jambo la muda tu
5. Mwanaume anaependa mazoea yasiyo na tija na wanawake esp maex. Ukishakua na mwanamke haina haja ya mazoea ya hovyo hovyo na wanawake wengine, mwenza wako should be your best friend
6. MWANAUME AMBAE ANALINDA SIMU YAKE KAMA VILE YEYE NI CIA. Sio lazima kukagua simu ya mtu but ukihitaji kuitumia sio unakutana na vikwazo mpaka unajiuliza hii ni simu au ni kitu gani?

Maisha ni haya haya mahusiano sio vita.
Nashukuru Mungu, nlipata tu kijana muungwana tukahangaika weeeee na hatimaye tumekutana katikati. Kifo tu kitaingilia kati
 
1. Akishaniambia kwenye simu sijui dadaake au mdogo wake wanataka kunisalimia
2.Mjuaji sanaa yaani kila kitu anajua yeye kila story yumo
3.Akiwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wa kike
4.Akiniomba vocha ni bora aniombe kitu kingine na sio vocha haijalishi ya kiasi gani hata kama ni ya 500 lakini akitamka vocha ama niunganishe kifurushi.
 
Mambo yake yote ananiambia hanifichi, bado sijamuoa lkn akiwa anaenda sehem tofauti na job kwake lazima aniage na tuna miaka zaidi ya 3
Hapa umepata mke aisee oa kabisa huyoo. Ni raha sana kuwa na mwanamke muwazi na mwenye kufunguka kwako namna hiyoo.
 
Back
Top Bottom