Kaudunde Kautwange
JF-Expert Member
- Nov 15, 2011
- 1,644
- 1,648
WATANZANIA ifike mahali tuache kuishi kwa nadharia zaidi,haswa nadharia tulizokariri kutoka mashuleni na vyuoni na kuja na majibu rahisi na ya kinadharia,na wala tusihitimishe tu kwa eti oh si tanzania tu bali dunia nzima thamani ya dollar imepanda sababu kubwa ni moja tu uhitaji wa dollar na matumizi yake umekuwa ni mkubwa kila kukicha na si tu kwenye exports na imports hebu liangalieni hili..
Maelezo haya ninayoyatoa yanatokana na uzoefu (experience) ya ngu mwenyewe kwa miezi hii ya karibuni, nilikuwa na wageni wangu kadhaa kutoka nje ya nchi wakiwa nchini kwa shughuli zao binafsi ambapo ilibidi waende uhamiaji na kubata vibali (permits) kulingana na shughuli hizo cha kusikitisha huko huko uhamiaji malipo yote yanafanyika kwa dollar ya marekani tu,tulikuwa ni shillingi zetu ikatubidi tuende bureau de change kununua dollar tukafanye malipo uhamiaji,je kwa mwendo huu mnadhani ni dollar ngapi zinanunuliwa kwa ajili ya malipo kama haya kila siku?
wakati huo huo serikali inasema si halali kwa mtu yeyote kulazimishwa kulipa kwa dollar nchini sasa kama si unafiki ni nini wakati wao wenyewe ndio maadvocate wa ugonjwa huu,tuithamini hela yetu jamani..
Siku hizi imekua ni "mtindo wa kisasa" watu kutoa huduma au kuuza bidhaa kwa dollar na hii ni experience yangu binafsi, kwa miezi takribani mitatu nimekuwa nikitafuta nyumba ya kupanga mjini hapa na karibu nyumba zote nilizokuwa interested nazo wanataka kodi kwa dollar,huyu dollar 300,huyu 400 yule 250 wengine hadi plots na nyumba utaona wnauza kwa dollari mara $ millioni 1, $millioni 3 n.k ulimbukeni unatuumiza sana,tumekaa kuangalia mambo kiushabiki ushabiki tuuuuu.
Serikali nafasi yake ni kubwa sana katika kubadilisha hali ya mambo lakini hamna lolote,wanaiba mabilioni yta shillingi na kuyaficha huko uswizi,wamekuja na ilani ya kudhibiti matumizi ya dollar lakini siasa nyingi,unafiki umewatawala hamana linalofanyika,binafsi hata sielewi nikilazimishwa kulipa kwa dollar nikaripoti polisi,BOT,ama vipi (viongozi wetu kama wanaona haya hivi kuwa straight na hili jambo)
Huo ni mtazamo wangu tu binafsi,based on my experience naamini kuna wataalamu wazalendo zaidi wa mambo ya uchumi katika uhalisia wake zaidi (sio yale matheory ya ECO101) amabao wanaweza kutudadavulia hili tatizo katika kiini chake watusaidie,tusaidiane kuikomboa hii shillingi tunayoichezea na kuidharau.
Chanzo kikubwa ni sheria zetu za fedha. Sheria zetu hasa za utalii na madini zinamlazimisha muwekezaji au mdau kulipa kwa dola. Thamani ya pesa ni jinsi gani inavyotafutwa (demanded) na watu ambao wako tayari kutoa fedha (supply) ili waipate hiyo shilingi.
Kwa kufanya hapo juu yaani kuondoa sheria hizo hapo juu nchi itakuwa na ulazima kutumia shilingi tu mtu akiingia Tanzania na hii itaifanya shiling itafutwe (demanded) sana na hivyo kuipandisha bei yake ya kubadilishana. Tuna madini na utalii mkubwa sana (hizi ndiyo export zetu) ambazo zingefanya hela yetu itafutwe kama lulu ili wayapate mazao ya madini na utalii.
Hakuna kipya sana tukirebisha sheria zetu uthamani wa shilingi yetu utapaa na pengine kufikia chini ya 500 kwa dola moja. Tuache kuendekeza fedha ya wenzetu $ na kuacha mtoto wetu shilingi akiwa hana mlezi. Kama nchi imeshindwa kuthamini hela yake basi iamue kutumia dola yaishe bila hivyo mnaumiza sana walaji (consumers) na wawekezaji (investors)
Shikamoni wana uchumi...mmegusa penyewe..huu ndo u reality tuutakao...