Ni sababu gani zinazochangia kushuka kwa Shilingi yetu na Dola kuwa juu?

Ni sababu gani zinazochangia kushuka kwa Shilingi yetu na Dola kuwa juu?

WATANZANIA ifike mahali tuache kuishi kwa nadharia zaidi,haswa nadharia tulizokariri kutoka mashuleni na vyuoni na kuja na majibu rahisi na ya kinadharia,na wala tusihitimishe tu kwa eti oh si tanzania tu bali dunia nzima thamani ya dollar imepanda sababu kubwa ni moja tu uhitaji wa dollar na matumizi yake umekuwa ni mkubwa kila kukicha na si tu kwenye exports na imports hebu liangalieni hili..

Maelezo haya ninayoyatoa yanatokana na uzoefu (experience) ya ngu mwenyewe kwa miezi hii ya karibuni, nilikuwa na wageni wangu kadhaa kutoka nje ya nchi wakiwa nchini kwa shughuli zao binafsi ambapo ilibidi waende uhamiaji na kubata vibali (permits) kulingana na shughuli hizo cha kusikitisha huko huko uhamiaji malipo yote yanafanyika kwa dollar ya marekani tu,tulikuwa ni shillingi zetu ikatubidi tuende bureau de change kununua dollar tukafanye malipo uhamiaji,je kwa mwendo huu mnadhani ni dollar ngapi zinanunuliwa kwa ajili ya malipo kama haya kila siku?

wakati huo huo serikali inasema si halali kwa mtu yeyote kulazimishwa kulipa kwa dollar nchini sasa kama si unafiki ni nini wakati wao wenyewe ndio maadvocate wa ugonjwa huu,tuithamini hela yetu jamani..


Siku hizi imekua ni "mtindo wa kisasa" watu kutoa huduma au kuuza bidhaa kwa dollar na hii ni experience yangu binafsi, kwa miezi takribani mitatu nimekuwa nikitafuta nyumba ya kupanga mjini hapa na karibu nyumba zote nilizokuwa interested nazo wanataka kodi kwa dollar,huyu dollar 300,huyu 400 yule 250 wengine hadi plots na nyumba utaona wnauza kwa dollari mara $ millioni 1, $millioni 3 n.k ulimbukeni unatuumiza sana,tumekaa kuangalia mambo kiushabiki ushabiki tuuuuu.

Serikali nafasi yake ni kubwa sana katika kubadilisha hali ya mambo lakini hamna lolote,wanaiba mabilioni yta shillingi na kuyaficha huko uswizi,wamekuja na ilani ya kudhibiti matumizi ya dollar lakini siasa nyingi,unafiki umewatawala hamana linalofanyika,binafsi hata sielewi nikilazimishwa kulipa kwa dollar nikaripoti polisi,BOT,ama vipi (viongozi wetu kama wanaona haya hivi kuwa straight na hili jambo)

Huo ni mtazamo wangu tu binafsi,based on my experience naamini kuna wataalamu wazalendo zaidi wa mambo ya uchumi katika uhalisia wake zaidi (sio yale matheory ya ECO101) amabao wanaweza kutudadavulia hili tatizo katika kiini chake watusaidie,tusaidiane kuikomboa hii shillingi tunayoichezea na kuidharau.

Chanzo kikubwa ni sheria zetu za fedha. Sheria zetu hasa za utalii na madini zinamlazimisha muwekezaji au mdau kulipa kwa dola. Thamani ya pesa ni jinsi gani inavyotafutwa (demanded) na watu ambao wako tayari kutoa fedha (supply) ili waipate hiyo shilingi.
Kwa kufanya hapo juu yaani kuondoa sheria hizo hapo juu nchi itakuwa na ulazima kutumia shilingi tu mtu akiingia Tanzania na hii itaifanya shiling itafutwe (demanded) sana na hivyo kuipandisha bei yake ya kubadilishana. Tuna madini na utalii mkubwa sana (hizi ndiyo export zetu) ambazo zingefanya hela yetu itafutwe kama lulu ili wayapate mazao ya madini na utalii.
Hakuna kipya sana tukirebisha sheria zetu uthamani wa shilingi yetu utapaa na pengine kufikia chini ya 500 kwa dola moja. Tuache kuendekeza fedha ya wenzetu $ na kuacha mtoto wetu shilingi akiwa hana mlezi. Kama nchi imeshindwa kuthamini hela yake basi iamue kutumia dola yaishe bila hivyo mnaumiza sana walaji (consumers) na wawekezaji (investors)

Shikamoni wana uchumi...mmegusa penyewe..huu ndo u reality tuutakao...
 
Sababu kubwa kuwapa wazungu wachimbe dhahabu yetu halafu wauze nje na kuipeleka nje kuimarisha akuba zao za dhahabu .
Dhahabu ndio akiba kuu inayofanya fedha ya nchi kutiyumba
Nchi nyingi zinanunua na kuweka akiba.

Sisi tuna dhahabu ya lili Africa tumewapa wazungu wanaichukua yote na mauzo wafanyao pesa hubaki mabenki ya nje huku benki zetu zikiwa na ukwasi wa fedha za kugeni.Cha kusikitisha hakuna Chadema wala Cuf wenye sera inayo eleweka kuhusu dhahabu yetu wote wameufyata kwa wazungu.

Sababu ya pili ni wasimamuzi wa fedha na mfumuko wetu BOT kuajiri watoto wa wakubwa na dini zaidi hivyo chombo hicho hakuna watu makini.Tuendelee kuumia tu.

Yani kuwe na sera ya dhahabu tu au ya kupandisha uchumi kwa ujumla?
 
Tatizo ni matumizi makubwa ya bidhaa za nje na mauzo madogo ya bidhaa zetu nje ya nchi, mfano; wanasiasa wanatumia maelfu ya lita za diesel kuzunguka na maspika yao wanaongeza matumizi ya mafuta pasipo sababu za msingi. hawa akina mnyika badala ya kuhimiza maendeleo kama kinana wao wanahimiza maandamano, jumatatu asubuhi akina slaa wanaandamana kutoka airport badala ya kuwa katika maeneo ya uzalishaji mali, hivi alishindwa nini kurudi siku ya mapumziko ya wiki?

Lipo tatizo la wafanyabishara wetu kukosa uwezo wa kuuza bidhaa nje ya nchi, wakati maji ya ruwenzori yametapakaa madukani kwetu, maji ya kilimanjaro hata kuuza nairobi na kampala wameshindwa. kupata fedha za kigeni hadi chibu akapige show nje. uchumi utaachaje kudorora.


Kuna watu wana vinyesi kichwani badala ya ubongo..
 
Matatizo haya yalianza zamani. Ila huwa tunayachukulia kijuu juu tu .
Mbali ya sababu walizotaja wana jf mbali mbali tatizo kubwa linalo yumbisha currency yetu ilianzia pale Mkapa alipo amua kuwahonga na hujumu nchi kwa kuzigawa maelfu kwa maelfu ya zilizo kuwa nyumba za serikali.
Nyumba hizi zenye thamani kubwa zimeenea nchi nzima katika mikoa yote.
Nyumba za zerikali nyingi zilikua katika maeneo nyeti ya miji yetu mfano hapa dar ni masaki . Oysterbay. Seaview.mikicheni. nk.
Kutokana na mahitaji ya nyumba za hali ya juu kuongezeka na mafisadi wenye pesa za madafu kuwa wengi nyumba hizi zime attract bei ya juu sana na nyingi zimeuzwa kwa Dolla.
Nyumba hizi zimeuzwa kwa mikataba feki kuanzia dolla milion moja $1m to $8m kwa nyumba moja.
Zaidi ya asilimia 50 ya nyumba hizi tayari zimeuzwa kwa mafisadi kwa dola .
Hivyo athari yake ya ufisadi huu wa Mkapa kuwauzia nyumba za serikali kwa bei ya kununua dagaa na hawa walohingwa ndio sasa wanayumbisha sarafu yetu.
Maelfu ya dolla wamepata na kuyatorosha nje hivyo kuifanya dolla kupanda sana.
Na bado suala hili litaendelea kuitesa sarafu yetu kwani bado kuna nyumba nyingi hazijauzwa lakini zipo sokoni na zikiuzwa kwa bei mbaya sana kwa Dolla tu.
Kule marekani nyumba ndio zilileta balaa lile la uchumi kwa walokopa pesa za kununua nyumba kuziachia mabenki myumba hizo baada ya kushuka thamani na kuyafanya mabenki makubwa kuanguka.
Hapa kwetu ni tofauti. Serikali imeziuza kifisadi nyumba zenye thamani ya kubwa ya mabilion kwa fedha ndogo sana na wale walouziwa wanaziuza kwa Dolla kwa fedha nyingi sana hivyo kuyumbisha uchumi na sarafu yetu.

Sababu hizi Prof Ndulu hawezi kuzitaja hata siku moja.
 
watanzania ifike mahali tuache kuishi kwa nadharia zaidi,haswa nadharia tulizokariri kutoka mashuleni na vyuoni na kuja na majibu rahisi na ya kinadharia,na wala tusihitimishe tu kwa eti oh si tanzania tu bali dunia nzima thamani ya dollar imepanda sababu kubwa ni moja tu uhitaji wa dollar na matumizi yake umekuwa ni mkubwa kila kukicha na si tu kwenye exports na imports hebu liangalieni hili..

Maelezo haya ninayoyatoa yanatokana na uzoefu (experience) ya ngu mwenyewe kwa miezi hii ya karibuni, nilikuwa na wageni wangu kadhaa kutoka nje ya nchi wakiwa nchini kwa shughuli zao binafsi ambapo ilibidi waende uhamiaji na kubata vibali (permits) kulingana na shughuli hizo cha kusikitisha huko huko uhamiaji malipo yote yanafanyika kwa dollar ya marekani tu,tulikuwa ni shillingi zetu ikatubidi tuende bureau de change kununua dollar tukafanye malipo uhamiaji,je kwa mwendo huu mnadhani ni dollar ngapi zinanunuliwa kwa ajili ya malipo kama haya kila siku?

Wakati huo huo serikali inasema si halali kwa mtu yeyote kulazimishwa kulipa kwa dollar nchini sasa kama si unafiki ni nini wakati wao wenyewe ndio maadvocate wa ugonjwa huu,tuithamini hela yetu jamani..


Siku hizi imekua ni "mtindo wa kisasa" watu kutoa huduma au kuuza bidhaa kwa dollar na hii ni experience yangu binafsi, kwa miezi takribani mitatu nimekuwa nikitafuta nyumba ya kupanga mjini hapa na karibu nyumba zote nilizokuwa interested nazo wanataka kodi kwa dollar,huyu dollar 300,huyu 400 yule 250 wengine hadi plots na nyumba utaona wnauza kwa dollari mara $ millioni 1, $millioni 3 n.k ulimbukeni unatuumiza sana,tumekaa kuangalia mambo kiushabiki ushabiki tuuuuu.

Serikali nafasi yake ni kubwa sana katika kubadilisha hali ya mambo lakini hamna lolote,wanaiba mabilioni yta shillingi na kuyaficha huko uswizi,wamekuja na ilani ya kudhibiti matumizi ya dollar lakini siasa nyingi,unafiki umewatawala hamana linalofanyika,binafsi hata sielewi nikilazimishwa kulipa kwa dollar nikaripoti polisi,bot,ama vipi (viongozi wetu kama wanaona haya hivi kuwa straight na hili jambo)

huo ni mtazamo wangu tu binafsi,based on my experience naamini kuna wataalamu wazalendo zaidi wa mambo ya uchumi katika uhalisia wake zaidi (sio yale matheory ya eco101) amabao wanaweza kutudadavulia hili tatizo katika kiini chake watusaidie,tusaidiane kuikomboa hii shillingi tunayoichezea na kuidharau.

chanzo kikubwa ni sheria zetu za fedha. Sheria zetu hasa za utalii na madini zinamlazimisha muwekezaji au mdau kulipa kwa dola. Thamani ya pesa ni jinsi gani inavyotafutwa (demanded) na watu ambao wako tayari kutoa fedha (supply) ili waipate hiyo shilingi.
Kwa kufanya hapo juu yaani kuondoa sheria hizo hapo juu nchi itakuwa na ulazima kutumia shilingi tu mtu akiingia tanzania na hii itaifanya shiling itafutwe (demanded) sana na hivyo kuipandisha bei yake ya kubadilishana. Tuna madini na utalii mkubwa sana (hizi ndiyo export zetu) ambazo zingefanya hela yetu itafutwe kama lulu ili wayapate mazao ya madini na utalii.
Hakuna kipya sana tukirebisha sheria zetu uthamani wa shilingi yetu utapaa na pengine kufikia chini ya 500 kwa dola moja. Tuache kuendekeza fedha ya wenzetu $ na kuacha mtoto wetu shilingi akiwa hana mlezi. Kama nchi imeshindwa kuthamini hela yake basi iamue kutumia dola yaishe bila hivyo mnaumiza sana walaji (consumers) na wawekezaji (investors)

heshima kwenu wakuu
 
sababu kubwa ni kuwa ili ufanye manunuzi yoyote na nchi nyingine unapaswa kununua kwanza dola kwa kuwa ndiyo pesa imara ili ununulie mahitaji yako

Uchaguzi nao umeangusha uchumi na thamani ya shilingi, kipindi hiki wafanya biashara hupunguza speed ya kufanya biashara kwa hofu ya machafuko.
Pili kukosekana kwa watalii, ambao utalii ni pato kubwa kwa taifa.
Tatu rushwa na ukandamizaji wa democracy ni chanzo cha kushuka kwa thamani ya shilingi, matajiri wote washaondoa fedha zao nchini, kwa kuogopa machafuko na chama tawala kudai pesa ya campaign au kuwaangusha kiuchumi wafanyakazi biashara, hilo huwa lazima, Hivyo hukimbia nchini kipindi hiki.
 
Back
Top Bottom