Ni sababu gani zinazochangia kushuka kwa Shilingi yetu na Dola kuwa juu?

Ni sababu gani zinazochangia kushuka kwa Shilingi yetu na Dola kuwa juu?

Joined
Oct 5, 2014
Posts
30
Reaction score
0
Habari zenu wanajamvi la biashara,

Naomba msaada wenu kwa kunielewesha ni sababu zipi zinazochangia kushuka kwa shilingi yetu na dollar kuwa juu sana kiasi kwamba mzunguko wa biashara umekuwa ni mgumu sana kutokana na kushuka kwa shiling yetu.
 
Sababu kubwa kuwapa wazungu wachimbe dhahabu yetu halafu wauze nje na kuipeleka nje kuimarisha akuba zao za dhahabu .
Dhahabu ndio akiba kuu inayofanya fedha ya nchi kutiyumba
Nchi nyingi zinanunua na kuweka akiba.

Sisi tuna dhahabu ya lili Africa tumewapa wazungu wanaichukua yote na mauzo wafanyao pesa hubaki mabenki ya nje huku benki zetu zikiwa na ukwasi wa fedha za kugeni.Cha kusikitisha hakuna Chadema wala Cuf wenye sera inayo eleweka kuhusu dhahabu yetu wote wameufyata kwa wazungu.

Sababu ya pili ni wasimamuzi wa fedha na mfumuko wetu BOT kuajiri watoto wa wakubwa na dini zaidi hivyo chombo hicho hakuna watu makini.Tuendelee kuumia tu.
 
ukiachilia mbali itikadi ya vyama hizi ndizo sababu za kushuka kwa dhamani ya fedha yetu dhidi ya dollar, kushindwa kudhibiti mfuko wa bei hii kwa wafanya biashara kupanga bei wanavyotaka na serikali kushindwa kudhibiti bei,

Pili ni Monitary police hapa ni wajibu wa benki kuu kudhibiti mzunguko wa fedha kwa kuzuia upatikanaji wa fedha nyingi kwenye jamii., Tatu ni kwasababu ya dollar kutumika wide na si kwa tanzania tu..
 
Tatizo ni matumizi makubwa ya bidhaa za nje na mauzo madogo ya bidhaa zetu nje ya nchi, mfano; wanasiasa wanatumia maelfu ya lita za diesel kuzunguka na maspika yao wanaongeza matumizi ya mafuta pasipo sababu za msingi. hawa akina mnyika badala ya kuhimiza maendeleo kama kinana wao wanahimiza maandamano, jumatatu asubuhi akina slaa wanaandamana kutoka airport badala ya kuwa katika maeneo ya uzalishaji mali, hivi alishindwa nini kurudi siku ya mapumziko ya wiki?

Lipo tatizo la wafanyabishara wetu kukosa uwezo wa kuuza bidhaa nje ya nchi, wakati maji ya ruwenzori yametapakaa madukani kwetu, maji ya kilimanjaro hata kuuza nairobi na kampala wameshindwa. kupata fedha za kigeni hadi chibu akapige show nje. uchumi utaachaje kudorora.
 
sababu kubwa ni kuwa ili ufanye manunuzi yoyote na nchi nyingine unapaswa kununua kwanza dola kwa kuwa ndiyo pesa imara ili ununulie mahitaji yako
 
we are importing more than we are exporting.pengine msimu ukifika hali itaimprove kidogo.kwani sasa dola inakuwa in high demand that is why bei iko juu
 
Kuna utafiti binafsi nimefanya kuilinganisha shilingi yetu na fedha zingine! Ukweli shilingi yetu ni pesa nyepesi sana kuilinganisha na dolla au hata paund, katika miezi ya hivi karibuni hasa kuanzia November 2014 dolla ya marekani imekua na nguvu sana baada ya kuimalika kwa uchumi wao na hasa kupungua kwa wasio na kazi! Dola ya marekani imekua juu sana kulinganisha na fedha zingine fedha nyingi duniani zimeanguka thamani sio tu shilingi yetu! Mie sio mwana ccm na siipendi kabisa ila kitakwimu kwenye makaratasi figure zinaonyesha uchumi unakua vzr tu Lkn pamoja ukuaji huo fedha yetu haiwezi kushindana na us dolla! Achlia mbali manunuzi yetu nchi za nje Ila kubwa ni Kua American dolla iko strong sana! Nchi nyingi ulaya zinajitahidikuimarisha sarafu zao hata kwa kupunguza baadhi ya riba katika bidhaa na mikopombali mbali Kama mikopombali nyumba nk
 
Habari zenu wanajamvi la biashara,

Naomba msaada wenu kwa kunielewesha ni sababu zipi zinazochangia kushuka kwa shilingi yetu na dollar kuwa juu sana kiasi kwamba mzunguko wa biashara umekuwa ni mgumu sana kutokana na kushuka kwa shiling yetu.

dola inakimbiza sarafu nyingi duniani kwa hiyo siyo shilingi tu at least hichi ndicho ninachofahamu
 
Kuna sababu kuu moja. Sababu yenyewe ni hii: Tunaingiza bidhaa nyingi mno kutoka nje ya nchi LAKINI hatuuzi bidhaa nje ya nchi. Kwa lugha nyepesi ni: WE IMPORT MORE THAN WHAT WE EXPORT.
Wewe fikiria hadi vijiti vya kuchokonolea meno (tooth picks), pamba za kusafishia masikio nyingi tunachukua kutoka china

Nchi inaendelea kwa kuwa na viwanda. Tanzania kuja kuendelea hadi YESU arud coz ipo nyuma sana kujenga na kuendeleza viwanda
 
Dollar is doing well globally, sio apa tu
 
Attachments

  • 1429827811438.jpg
    1429827811438.jpg
    55.5 KB · Views: 297
For more than 2 decades kenyan shilling has been exchanged at 67Ksh against the US$.
Soon we gonna hit 5000tzs against the US$
What's wrong with Tz?
 
WATANZANIA ifike mahali tuache kuishi kwa nadharia zaidi,haswa nadharia tulizokariri kutoka mashuleni na vyuoni na kuja na majibu rahisi na ya kinadharia,na wala tusihitimishe tu kwa eti oh si tanzania tu bali dunia nzima thamani ya dollar imepanda sababu kubwa ni moja tu uhitaji wa dollar na matumizi yake umekuwa ni mkubwa kila kukicha na si tu kwenye exports na imports hebu liangalieni hili..

Maelezo haya ninayoyatoa yanatokana na uzoefu (experience) ya ngu mwenyewe kwa miezi hii ya karibuni, nilikuwa na wageni wangu kadhaa kutoka nje ya nchi wakiwa nchini kwa shughuli zao binafsi ambapo ilibidi waende uhamiaji na kubata vibali (permits) kulingana na shughuli hizo cha kusikitisha huko huko uhamiaji malipo yote yanafanyika kwa dollar ya marekani tu,tulikuwa ni shillingi zetu ikatubidi tuende bureau de change kununua dollar tukafanye malipo uhamiaji,je kwa mwendo huu mnadhani ni dollar ngapi zinanunuliwa kwa ajili ya malipo kama haya kila siku?

wakati huo huo serikali inasema si halali kwa mtu yeyote kulazimishwa kulipa kwa dollar nchini sasa kama si unafiki ni nini wakati wao wenyewe ndio maadvocate wa ugonjwa huu,tuithamini hela yetu jamani..

Siku hizi imekua ni "mtindo wa kisasa" watu kutoa huduma au kuuza bidhaa kwa dollar na hii ni experience yangu binafsi, kwa miezi takribani mitatu nimekuwa nikitafuta nyumba ya kupanga mjini hapa na karibu nyumba zote nilizokuwa interested nazo wanataka kodi kwa dollar,huyu dollar 300,huyu 400 yule 250 wengine hadi plots na nyumba utaona wnauza kwa dollari mara $ millioni 1, $millioni 3 n.k ulimbukeni unatuumiza sana,tumekaa kuangalia mambo kiushabiki ushabiki tuuuuu.

Serikali nafasi yake ni kubwa sana katika kubadilisha hali ya mambo lakini hamna lolote,wanaiba mabilioni yta shillingi na kuyaficha huko uswizi,wamekuja na ilani ya kudhibiti matumizi ya dollar lakini siasa nyingi,unafiki umewatawala hamana linalofanyika,binafsi hata sielewi nikilazimishwa kulipa kwa dollar nikaripoti polisi,BOT,ama vipi (viongozi wetu kama wanaona haya hivi kuwa straight na hili jambo)

Huo ni mtazamo wangu tu binafsi,based on my experience naamini kuna wataalamu wazalendo zaidi wa mambo ya uchumi katika uhalisia wake zaidi (sio yale matheory ya ECO101) amabao wanaweza kutudadavulia hili tatizo katika kiini chake watusaidie,tusaidiane kuikomboa hii shillingi tunayoichezea na kuidharau.

Umeandika jambo la msingi sana na kwa uzalendo wa hali ya juu...heshima kwako mkuu...
 
...hizo zooote ni sababu za msingi sana , lakini nyingi ya hizi za wadau ni sababu za kuifanya shillingi iwe weak against dollar. ninavyo fahamu mimi jambo kubwa sana linalofanya huu mporomoko Wa ajabu wa thamani ya dollar huwa na wafanabiashara wakubwa hasa wenye asili ya kihindi kukimbiza fedha zao kipeleka nje ya nchi hasa unapokaribia uchaguzi mkuu. Mara nyingi unapokaribia uchaguzi huwa thamani ya shilingi inashuka sana hasa wanapoona kunadalili za kumkosa mgombea wanaye mpenda wakihofia sera ya wahujumu uchumi maana azimio LA arusha bado lipo hai ila mafisadi wamelizima kwa mfumo corrupt. Kwaiyo kundi kuuubwa la wanasiasa na wafanyabiashara wanatorosha fedha in dollar na kusababisha upungufu wa dollar nchini so demand inaongezeka na BOT wanaibana matokeo yake inaua shilingi.....
 
Deni kubwa la Taifa 35 Trillioni, kupungua kwa mapato ya pesa za kigeni, uhamishaji haramu wa pesa za kigeni kwenda nchi za nje na ikiwemo pia hali ya hofu kuelekea kwenye kura ya maoni na uchaguzi Mkuu.
 
Hata mahoteli mengi haya makubwa wananunua bidhaa zao nje na tunanunua mno magari japan
 
Chanzo kikubwa ni sheria zetu za fedha. Sheria zetu hasa za utalii na madini zinamlazimisha muwekezaji au mdau kulipa kwa dola. Thamani ya pesa ni jinsi gani inavyotafutwa (demanded) na watu ambao wako tayari kutoa fedha (supply) ili waipate hiyo shilingi.
Kwa kufanya hapo juu yaani kuondoa sheria hizo hapo juu nchi itakuwa na ulazima kutumia shilingi tu mtu akiingia Tanzania na hii itaifanya shiling itafutwe (demanded) sana na hivyo kuipandisha bei yake ya kubadilishana. Tuna madini na utalii mkubwa sana (hizi ndiyo export zetu) ambazo zingefanya hela yetu itafutwe kama lulu ili wayapate mazao ya madini na utalii.
Hakuna kipya sana tukirebisha sheria zetu uthamani wa shilingi yetu utapaa na pengine kufikia chini ya 500 kwa dola moja. Tuache kuendekeza fedha ya wenzetu $ na kuacha mtoto wetu shilingi akiwa hana mlezi. Kama nchi imeshindwa kuthamini hela yake basi iamue kutumia dola yaishe bila hivyo mnaumiza sana walaji (consumers) na wawekezaji (investors)
 
Point ni less productivity...
We are not producing at all...
Kila kitu tuna import nenda kkoo utaona hata mdoli kawa imported toka nje then kuna miujiza gan ya TSHS kupanda thaman?
 
Chanzo kikubwa ni sheria zetu za fedha. Sheria zetu hasa za utalii na madini zinamlazimisha muwekezaji au mdau kulipa kwa dola. Thamani ya pesa ni jinsi gani inavyotafutwa (demanded) na watu ambao wako tayari kutoa fedha (supply) ili waipate hiyo shilingi.
Kwa kufanya hapo juu yaani kuondoa sheria hizo hapo juu nchi itakuwa na ulazima kutumia shilingi tu mtu akiingia Tanzania na hii itaifanya shiling itafutwe (demanded) sana na hivyo kuipandisha bei yake ya kubadilishana. Tuna madini na utalii mkubwa sana (hizi ndiyo export zetu) ambazo zingefanya hela yetu itafutwe kama lulu ili wayapate mazao ya madini na utalii.
Hakuna kipya sana tukirebisha sheria zetu uthamani wa shilingi yetu utapaa na pengine kufikia chini ya 500 kwa dola moja. Tuache kuendekeza fedha ya wenzetu $ na kuacha mtoto wetu shilingi akiwa hana mlezi. Kama nchi imeshindwa kuthamini hela yake basi iamue kutumia dola yaishe bila hivyo mnaumiza sana walaji (consumers) na wawekezaji (investors)

Mkuu umetoa point ya muhimu sana. Nimeikubali argument yako. Big up
 
Dollar imepanda karibu ulimwengu woote jombaaa kwa kifupi America uchumi umekuwa stronger mfano mzuri ni Australian dollar tofauti ilikuwa few cents lakini sasa ni zaidi ya dollar 2 so sio kweli kwamba Tz sijui siasa no ni USA wame rudi mahali Yao
 
Back
Top Bottom