Ni sababu ipi hupelekea watu kujenga bila ramani au kwa ramani za kukopi kutoka kwa watu wengine?

Ni sababu ipi hupelekea watu kujenga bila ramani au kwa ramani za kukopi kutoka kwa watu wengine?

Black Thought

Senior Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
161
Reaction score
408
Habarini wakuu.

Hivi ni kwanini watu hujenga kwa ramani za kufikirika tu zisizokuwa na mpangilio wa kitaalamu. Yaani umejibana kukusanya milioni zako flani, unamtafuta fundi na kumtajia idadi ya vyumba tu ajenge au unampa mfano wa ramani uliyoipata kwenye mtandao.

Hebu fikiria umetumia milioni zako kadhaa kuinua mjengo, halafu baada ya kuhamia na kuanza kupigwa na jua, huku ‘ventilation’ ikiwa mbaya yaani upepo ukipiga upande usio na vyumba, ndio unagundua kwa ‘proper zoning’ chumba chako kilitakiwa kikae mahali ilipo public toilet, au dining au store+jiko.

Pia unagundua kuwa unakosa faragha (privacy) kwa wageni na changamoto nyingine nyingi.

Ni rahisi sana kulitambua hilo ukianza na ramani yako kwa kuleta wataalamu kwenye kiwanja chako, ili utengenezewe ramani kulingana na kiwanja chako na mahitaji yako.

Ungeweza kujenga kwa ramani ileile ulioipenda lakini ikahitaji mabadiliko kidogo sana iendane na kiwanja chako na kukufanya ufurahie uwekezaji wako.

Unaweza kutucheki kwa namba 0717682856 tuje kufanya 'site analysis' upate kilicho bora kwa uwekezaji wako
 
Maneno yote hayo na kujifanya mtaalamu ila kazi yako uliyoweka kwenye profile ipo low sana.
Kama kazi zako zingine ni sawa na hiyo picha kwenye profile basi hii post inabidi uifute
Humu nilichoona wengi sio wataalamu wa ramani na ujenzi, bali ni mtu kafundishwa kidogo tu kuchora nae anakuja humu kuleta upupu
Chini ni picha ya mchoro wa nyumba ambayo ume-design, nakuhakikishia kwa mchoro huu huwezi kupata serious customer.
Jaribu kujifunza zaidi na zaidi, ukiiva ndio uje kutafuta kazi
JamiiForums1340831049.jpg
 
View attachment 1653197
We jamaa nishaona comments zako kabla kwenye kazi za ramani. Na kuna jamaa alikuuliza kama wewe ni architect/Engineer ukakanusha. Unakashifu bila kuonesha tatizo lipo wapi, So sina sababu ya ku'justify uwezo wangu kwako. Ila Hongera maana unajua sana yani
 
Kujua najua kweli tena sana, nasisitiza mimi sio mchora ramani/architect, bali mimi ni structural engineer.
Nakuapia kwa aina ya mchoro ulioweka kwenye profile yako HUWEZI KUPATA SERIOUS CUSTOMER.
Nimekupa ushauri wewe pamoja na wengine humu wanaopost kazi zao mbovu, wajifunze zaidi na zaidi wakiiva ndio waje kutafuta kazi humu.
 
Poa mtaalamu kwakuwa wewe unajua. Ila next time jaribu kutoa technical reason Issue ya muonekano wa nje ni very subjective, kila mtu na anavyoona yeye.
Nafikiri ungeonesha mfano nakueleza tatizo liko wapi point yako ingekuwa na mashiko sana.
Nasisitiza kukosoa kwako sio tatizo, ila ni kwamba huna technical point, just personal opinion na sio kwangu tu nshakuona kabla. As a matter of fact 3Ds sio big deal kwenye design.
Ila hongera kwakuwa unajua na hongera kwa kufanikiwa kuapa hapo.
 
Maneno yote hayo na kujifanya mtaalamu ila kazi yako uliyoweka kwenye profile ipo low sana.
Kama kazi zako zingine ni sawa na hiyo picha kwenye profile basi hii post inabidi uifute
Humu nilichoona wengi sio wataalamu wa ramani na ujenzi, bali ni mtu kafundishwa kidogo tu kuchora nae anakuja humu kuleta upupu
Chini ni picha ya mchoro wa nyumba ambayo ume-design, nakuhakikishia kwa mchoro huu huwezi kupata serious customer.
Jaribu kujifunza zaidi na zaidi, ukiiva ndio uje kutafuta kazi
View attachment 1653197
Aseee, hilo ghorofa ama?
 
Kujua najua kweli tena sana, nasisitiza mimi sio mchora ramani/architect, bali mimi ni structural engineer.
.

Sasa mkuu toka lini engineer akakosoa kazi ya architect technically? Yani umejuaje iko low quality wakati wewe sio architect? Je huku sio kuingilia field isiyokuhusu? Atleast ungekua architect inge make sense!!

Pili, kama kweli wewe ni engineer je code of ethics zinasemaje injinia kumkosoa mwenzake publically?

Je code of conduct inasemaje kuhusu kukosoa kazi ya mwenzako? Je kama unajua ulichofanya hapa ni sahihi?

Naomba majibu tafadhali.
 
Sasa mkuu toka lini engineer akakosoa kazi ya architect technically? Yani umejuaj3 iko low quality wakati wewe sio architect? Je huku sio kuingilia field isiyo kuhusu? Atleast ungekua architect inge make sense!!

Pili, kama kweli wewe ni engineer je code of ethics zinasemaje injinia kumkosoa mwenzake publically?

Je code of conduct inasemaje kuhusu kukosoa kazi ya mwenzako? Je kama unajua ulicho fanya hapa ni sahihi?

Naomba majibu tafadhali.
Wewe hujielewi, ndio umejifunza leo hilo neno "code of conduct"?
Ni nani amekuambia huyo ni Architect?? HAKUNA Architect anayeweza kuchora mchoro wa aina hiyo, nasisitiza HAKUNA
Kwa faida yako;
Sio lazima uwe Architect ndio umkosoe Architect, yoyote mwenye ufahamu wa ujenzi awe QS, Civil Eng, Structural n.k wanaweza kukosoa
Hebu ngoja, una maanisha pia huwezi kumkosoa dereva ikiwa wewe sio dereva? Au huwezi kumkosoa mwanasiasa ikiwa wewe sio mwanasiasa?
January ifike mapema tu shule zifunguliwe, maana kuna vitoto vingi humu
 
Kuna architect nilimwambia anichoree ramani daah akawa anadai dau kubwa mno basi nikaona ishu nikamtafuta mwingine nikampa kazi ya kuchora ramani nyumba ya vyumba vitatu na picha nilikuwa nayo nikampa na alidai hela ndefu pia nikaona poa, nilikuwa nahitaji vitatu tu foundation planning, elevation planning na roof planning asubuhi namwambia atumie alipofikia anatuma vipicha vya ajabu ajabu na vitu simple tu.

Nikampiga fundi akasema napoteza pesa, nikaona kweli mimi ni IT nikaona hakuna kitu kipya nikakaa na fundi tukachora ramani tena nzuri sana nikasave pesa...niligundua architecture wengi wababaishi na kazi ukikaa na fundi mzoefu unachora ramani nzuri bila gharama.
 
kuna architect nilimwambia anichoree ramani daah akawa anadai dau kubwa mno basi nikaona ishu nikamtafuta mwingine nikampa kazi ya kuchora ramani nyumba ya vyumba vitatu na picha nilikuwa nayo nikampa na alidai hela ndefu pia nikaona poa nilikuwa nahitaji vitatu tu foundation planning, elevation planning na roof planning asubuhi namwambia atumie alipofikia anatuma vipicha vya ajabu ajabu na vitu simple tu nakampiga fundi akasema napoteza pesa nakaona kweli mimi ni IT nikaona hakuna kitu kipya nikakaa na fundi tukachora ramani tena nzuri sana nikasave pesa...niligundua architecture wengi wababaishi na kazi ukikaa na fundi mzoefu unachora ramani nzuri bila gharama
Mkuu, hujui maana ya ramani..
Ni vizuri upate professional architect, mfikishe eneo husika aone, then mwelekeze mahitaji yako ayatimize professionally
 
Ikiwa umesoma technical school ukachagua civil engineering kiukweli unaweza kubuni ramani yako nzuri tu
Namuunga mkono Countrywide kuwa wachoraji wengi wanafanya kurubuni na muonekano wa nje/rangi lakini mambo mengi ni yale yale tu na mara nyingi nao pia hutoa ramani kwenye mitandao
Ndio maana huwezi kukuta ubunifu tofauti kwenye hizi nyumba zetu za makazi sie wa kipato cha chini
 
kuna architect nilimwambia anichoree ramani daah akawa anadai dau kubwa mno basi nikaona ishu nikamtafuta mwingine nikampa kazi ya kuchora ramani nyumba ya vyumba vitatu na picha nilikuwa nayo nikampa na alidai hela ndefu pia nikaona poa nilikuwa nahitaji vitatu tu foundation planning, elevation planning na roof planning asubuhi namwambia atumie alipofikia anatuma vipicha vya ajabu ajabu na vitu simple tu nakampiga fundi akasema napoteza pesa nakaona kweli mimi ni IT nikaona hakuna kitu kipya nikakaa na fundi tukachora ramani tena nzuri sana nikasave pesa...niligundua architecture wengi wababaishi na kazi ukikaa na fundi mzoefu unachora ramani nzuri bila gharama
Sawa mkuu endeleeni kuchora na fundi wako.
NB: Mafundi wa VETA wamejifunza uchoraji na pia programs za kujifunza ziko kibao mtandaoni.
 
Tatizo kubwa ni umaskini! Watu wengi wanaona kuweka Architect ni gharama lakini gharama kubwa zaidi ni kutengeneza jengo bovu lisiloendana na kiwanja na hali mahalia( micro climate).

Kingine ni kuwa wengi hawakuzoea vitu vizuri. Mtu anaona nyumba ni kuta na sakafu na dari bila kuangalia uzuri ( aesthetics)

Lakini kingine ni ushauri mbaya kutoka kwa marafiki na ndugu
 
Back
Top Bottom