Ni sababu ipi hupelekea watu kujenga bila ramani au kwa ramani za kukopi kutoka kwa watu wengine?

Habarini wakuu.

Hivi ni kwanini watu hujenga kwa ramani za kufikirika tu zisizokuwa na mpangilio wa kitaalamu. Yani umejibana kukusanya milioni zako flani, unamtafuta fundi na kumtajia idadi ya vyumba tu ajenge, au unampa mfano wa ramani uliyoipata kwenye mtandao.

Hebu fikiria umetumia milioni zako kazaa kuinua mjengo, halafu baada ya kuhamia na kuanza kupigwa na jua, huku ‘ventilation’ ikiwa mbaya yani upepo ukipiga upande usio na vyumba, ndio unagundua kwa ‘proper zoning’ chumba chako kilitakiwa kikae mahali ilipo public toilet, au dining au store+jiko.

Pia unagundua kuwa unakosa faragha (privacy) kwa wageni na changamoto nyingine nyingi.

Ni rahisi sana kulitambua hilo ukianza na ramani yako kwa kuleta wataalamu kwenye kiwanja chako, ili utengenezewe ramani kulingana na kiwanja chako na mahitaji yako.

Ungeweza kujenga kwa ramani ileile ulioipenda lakini ikahitaji mabadiliko kidogo sana iendane na kiwanja chako, na kukufanya ufurahie uwekezaji wako.

Unaweza kutucheki kwa namba 0717682856 tuje kufanya 'site analysis' upate kilicho bora kwa uwekezaji wako
Tatizo mnakuwaga na akili za ki kanjanja za kutaka kuwapiga watu hela kwanvitu ambavyo mngeomba hata hela ya maji.

Me kuna jamaa nilimuona online, ana biashara ya maswala ya ujenzi. Nikasema ngoja nimuungishe biashara. Nikawasiliana nae twende eneo langu akalicheki tujadili kujenga nyumba ya vyumba vitatu.

Jamaa akafanya ramli zake then baada ya dakika chake anjijia na upuuzi wake wa kunambia kunipa tu ushauri ni 1.2 milioni. Nikamuuliza tena, hiyo ina include nini maana ramani ninayo tayari. Akanambia hiyo ni procedure katika kampuni. Nikacheka sana kimoyo moyo. Nikamwambia mkuu poa. Ngoja niweke mambo sawa nitakupigia.
 
Kama wewe ni mkristo jitahidi kwenda jumuiya utaona ramani nyingi na unamwita fundi unaweka mambo sawa, mpate fundi anajua kujenga
 
Tatizo watu tunapenda vya bei chee sana, lakini lazima tukubali kutumia wataalamu katika issue yoyote ile inaleta tija sana!!

Naona kuna mdau mmoja anakosea kazo ya mwenzake pasipo ku-point out technical reasons!! Mfano mm ningemuliza shida ni muonekano au kuna kitu kingine?

As for me appearance is subjective from one another but when it comes to functionality shida inaanzia hapo!! Unakuja jengo lina muonekano mzuri sana kwa nje lakni ukija kwenye mpangilio wa rooms ni ovyo sana!!

Hii inatokana na ukweli kwamba vijana wengi wamemaliza vyuo hawana uzoefu wowote katika designing lakn wameamua kujiajili ili wamapete ridhiki na bahati mbaya gharama zao ni nafuu kiasi ukilinganisha na gharama ambazo ungepewa na registered Architectural firms !

Hivyo, kwakuwa sisi watanzania tunapenda vya bure, basi wengi watu tunakuwa hatuna jinsi zaidi ya kukumbilia kule kwenye unafuu wa bei na that's why baadhi yetu wanadai ni mara mia watumie mafundi kubuni ramani na ujenzi!!

Kwa kuhitimisha ningependa kusema, tupende kutumia watalaamu hususan ni registered firms zinazotambuliwa na bodi ya wasanifu na wakadiriaji majenzi (AQRB) mtapata vitu vizuri na haya malalamiko yatapungua!!
 
Kuna jamaa anauza boma ila ameambatanisha ramani ya boma sasa ile ramani ni ya ajabu, ramani haioneshi ukubwa wa jengo upanaxurefu afu vyumba havina uwiano wa size na mpangilio usio ridhisha, kuna idle space kubwa hasa corridor yaani corridor za ndani kubwa kama public building. Sasa hii ndio shida ya kutumia vijana wa VETA

Niliwahi kudesign mchoro nikampa jamaa basi kamchukua fundi wake wakabadili vipimo siku anasema nikupeleke site ukaone nikakuta wamejenga vituko yaani sitting inakuwa na mita 3x3 na dining mita 1 nilicheka Sana bahati nzuri walikuwa hawajafika mbali ikabidi niwashauri waue dining iwe sitting kubwa na marekebisho mengine .

Ushauri wa bure hata kama unataka kufanya marekebisho kwenye ramani ambazo ziko scalled Rudi kwa wataalam watakusaidia kuliko kujenga kituko kwa gharama kubwa. Cheap is expensive
 
Kuna jamaa anauza boma ila ameambatanisha ramani ya boma sasa ile ramani ni ya ajabu ,ramani haioneshi ukubwa wa jengo upanaxurefu afu vyumba havina uwiano wa size na mpangilio usio ridhisha,kuna idle space kubwa hasa corridor yaani corridor za ndani kubwa kama public building,,
Sasa hii ndio shida ya kutumia vijana wa VETA

Niliwah kudesign mchoro nikampa jamaa basi kamchukua fundi wake wakabadili vipimo siku anasema nikupeleke site ukaone nikakuta wamejenga vituko yaani sitting inakuwa na mita 3x3 na dining mita 1 nilicheka Sana bahati nzuri walikuwa hawajafika mbali ikabidi niwashauri waue dining iwe sitting kubwa na marekebisho mengine .

Ushauri wa bure hata kama unataka kufanya marekebisho kwenye ramani ambazo ziko scalled Rudi kwa wataalam watakusaidia kuliko kujenga kituko kwa gharama kubwa. Cheap is expensive
Na vipi ukigundua kuwa aliyemchorea ramani hiyo huyo muuza boma ni mtaalam utarud kuishutumu VETA ile ni taasisi makini sana tofauti na mnavyoidhania halaf mnabaguana katika industry moja kisa tu source of knowledge while you serve same society, same consumers kwann? Je sisi ambao hatukusoma mtatufanyaje sisi? Mungu Ibariki Africa Bariki Tanzania, Bariki Tarime, Amina..
 
Tatizo mnakuwaga na akili za ki kanjanja za kutaka kuwapiga watu hela kwanvitu ambavyo mngeomba hata hela ya maji.

Me kuna jamaa nilimuona online, ana biashara ya maswala ya ujenzi. Nikasema ngoja nimuungishe biashara. Nikawasiliana nae twende eneo langu akalicheki tujadili kujenga nyumba ya vyumba vitatu.

Jamaa akafanya ramli zake then baada ya dakika chake anjijia na upuuzi wake wa kunambia kunipa tu ushauri ni 1.2 milioni. Nikamuuliza tena, hiyo ina include nini maana ramani ninayo tayari. Akanambia hiyo ni procedure katika kampuni. Nikacheka sana kimoyo moyo. Nikamwambia mkuu poa. Ngoja niweke mambo sawa nitakupigia.
 
Duh!! Aisee mkuu hiyo 1.2mln kwa consultation tu, au hamkuelewana vizuri.
Niseme tu hakuna sababu ya kuDevalue watu wengine kwa sababu ya mtu mmoja.
 
Habarini wakuu.

Hivi ni kwanini watu hujenga kwa ramani za kufikirika tu zisizokuwa na mpangilio wa kitaalamu. Yani umejibana kukusanya milioni zako flani, unamtafuta fundi na kumtajia idadi ya vyumba tu ajenge, au unampa mfano wa ramani uliyoipata kwenye mtandao.

Hebu fikiria umetumia milioni zako kazaa kuinua mjengo, halafu baada ya kuhamia na kuanza kupigwa na jua, huku ‘ventilation’ ikiwa mbaya yani upepo ukipiga upande usio na vyumba, ndio unagundua kwa ‘proper zoning’ chumba chako kilitakiwa kikae mahali ilipo public toilet, au dining au store+jiko.

Pia unagundua kuwa unakosa faragha (privacy) kwa wageni na changamoto nyingine nyingi.

Ni rahisi sana kulitambua hilo ukianza na ramani yako kwa kuleta wataalamu kwenye kiwanja chako, ili utengenezewe ramani kulingana na kiwanja chako na mahitaji yako.

Ungeweza kujenga kwa ramani ileile ulioipenda lakini ikahitaji mabadiliko kidogo sana iendane na kiwanja chako, na kukufanya ufurahie uwekezaji wako.

Unaweza kutucheki kwa namba 0717682856 tuje kufanya 'site analysis' upate kilicho bora kwa uwekezaji wako
Hatuna hela...
 
Tatizo watu tunapenda vya bei chee sana, lakini lazima tukubali kutumia wataalamu katika issue yoyote ile inaleta tija sana!!

Naona kuna mdau mmoja anakosea kazo ya mwenzake pasipo ku-point out technical reasons!! Mfano mm ningemuliza shida ni muonekano au kuna kitu kingine?

As for me appearance is subjective from one another but when it comes to functionality shida inaanzia hapo!! Unakuja jengo lina muonekano mzuri sana kwa nje lakni ukija kwenye mpangilio wa rooms ni ovyo sana!!

Hii inatokana na ukweli kwamba vijana wengi wamemaliza vyuo hawana uzoefu wowote katika designing lakn wameamua kujiajili ili wamapete ridhiki na bahati mbaya gharama zao ni nafuu kiasi ukilinganisha na gharama ambazo ungepewa na registered Architectural firms !

Hivyo, kwakuwa sisi watanzania tunapenda vya bure, basi wengi watu tunakuwa hatuna jinsi zaidi ya kukumbilia kule kwenye unafuu wa bei na that's why baadhi yetu wanadai ni mara mia watumie mafundi kubuni ramani na ujenzi!!

Kwa kuhitimisha ningependa kusema, tupende kutumia watalaamu hususan ni registered firms zinazotambuliwa na bodi ya wasanifu na wakadiriaji majenzi (AQRB) mtapata vitu vizuri na haya malalamiko yatapungua!!
Mkuu kukosoa haikua shida ni kawaida tatizo ni kama ulivyosema hakutoa technical reason. Isitoshe kakosoa kutumia picha aliyoamua kuipost yeye. Post kama post imewekwa bila picha yoyote coz haikufanywa kuwa Tangazo. Sasa yeye kachukua avatar picha ya kitambo sana Ila binafsi ninakazi zangu za maana tu, ila sikuzote huwa naamini katika kutohusisha emotions kwenye arguments hasa zinazohusisha taaluma.
Naungana nawewe mkuu watu tuache kupenda shortcuts, In most cases cheap is more expensive
 
Hatuna hela...
Hela kiasi gani mkuu na unajenga nyumba ya pesa nyingi. Kwanini usihakikishe kile kinachojengwa ni kile hasa unakihitaji, kuanzia mpangilio wa vyumba, muonekano hadi ubora.
Ujue sio kila design inaweza kujengwa mahali popote kwa mtindo/ubora uleule. Kuna umuhimu wa kuhusisha wataalamu eneo lako la kiwanja, Ndio sababu nyumba nyingi unajenga unamwaga million zako kibao kisha unaanza kusumbuliwa na vitu kama cracks na effloresce

Na mnashindwa hata kuzingatia vitu kama uelekeo wa jua wala upepo so hata nyumba yenyewe huifurahii. Yaani ushaanza/ushamaliza kujenga ndio unaona chumba hiki kilitakiwa kikae kule na hiki kikae huku, au tulitakiwa kutumia material flani kwa tahadhari, unajikuta unakuja kupoteza pesa nyingi sana baadae kuliko hata uliyojaribu kuiokoa
 
Bro usikate tamaa na hizi negative comments zitumie kama changamoto za kukufanya upige hatua katika kazi yako na kile unachojishughulisha nacho. Keep it up Mkuu
Aisee mkuu unakatishwaje tamaa kwa maneno yasiyo na logic, just personal opinion za mtu.
Isitoshe watu tuko bize na kazi ni nyingi na mimi huwa sina emotions kwa mawazo ya mtu, ndiomaana sikutaka hata kupost kazi yangu moja kuJustify my work
 
Ikiwa umesoma technical school ukachagua civil engineering kiukweli unaweza kubuni ramani yako nzuri tu
Namuunga mkono Countrywide kuwa wachoraji wengi wanafanya kurubuni na muonekano wa nje/rangi lakini mambo mengi ni yale yale tu na mara nyingi nao pia hutoa ramani kwenye mitandao
Ndio maana huwezi kukuta ubunifu tofauti kwenye hizi nyumba zetu za makazi sie wa kipato cha chini
Sasa mkuu huyo unaemuunga mkono nayeye ndio anataka huo muonekano wa nje. Wakati kiuhalisia hata ungetaka kibali cha ujenzi kwenye mamlaka husika wala hawahitaji hizo 3D views. Wanazingatia spacial arrangement ya jengo, setbacks na standards zao walizoweka kulingana na maeneo ya ujenzi kwa muonekano wao huzongatia elevations tu.
Istoshe kwakawaida unatakiwa kulizishwa na kazi ilivyosanifiwa ndio kisha ufanye malipo.
 
Tatizo kubwa ni umaskini! Watu wengi wanaona kuweka Architect ni gharama lakini gharama kubwa zaidi ni kutengeneza jengo bovu lisiloendana na kiwanja na hali mahalia( micro climate).

Kingine ni kuwa wengi hawakuzoea vitu vizuri. Mtu anaona nyumba ni kuta na sakafu na dari bila kuangalia uzuri ( aesthetics)

Lakini kingine ni ushauri mbaya kutoka kwa marafiki na ndugu
👏🏿👏🏿Nakubaliana nawewe boss
 
Tatizo watu tunapenda vya bei chee sana, lakini lazima tukubali kutumia wataalamu katika issue yoyote ile inaleta tija sana!!

Naona kuna mdau mmoja anakosea kazo ya mwenzake pasipo ku-point out technical reasons!! Mfano mm ningemuliza shida ni muonekano au kuna kitu kingine?

As for me appearance is subjective from one another but when it comes to functionality shida inaanzia hapo!! Unakuja jengo lina muonekano mzuri sana kwa nje lakni ukija kwenye mpangilio wa rooms ni ovyo sana!!

Hii inatokana na ukweli kwamba vijana wengi wamemaliza vyuo hawana uzoefu wowote katika designing lakn wameamua kujiajili ili wamapete ridhiki na bahati mbaya gharama zao ni nafuu kiasi ukilinganisha na gharama ambazo ungepewa na registered Architectural firms !

Hivyo, kwakuwa sisi watanzania tunapenda vya bure, basi wengi watu tunakuwa hatuna jinsi zaidi ya kukumbilia kule kwenye unafuu wa bei na that's why baadhi yetu wanadai ni mara mia watumie mafundi kubuni ramani na ujenzi!!

Kwa kuhitimisha ningependa kusema, tupende kutumia watalaamu hususan ni registered firms zinazotambuliwa na bodi ya wasanifu na wakadiriaji majenzi (AQRB) mtapata vitu vizuri na haya malalamiko yatapungua!!
In shirt wachora ramani wa bongo hawana maajabu.

Wengi uwezo mdogo, wanajilazimisha kufanya kazi kwasababu ya njaa tu.

Kama kweli watu wangeona kuna jipya la tofauti kati ya waliochorewa ramani au waungaji, hakuna namna ramani zingekosa soko.
 
Kuna architect nilimwambia anichoree ramani daah akawa anadai dau kubwa mno basi nikaona ishu nikamtafuta mwingine nikampa kazi ya kuchora ramani nyumba ya vyumba vitatu na picha nilikuwa nayo nikampa na alidai hela ndefu pia nikaona poa, nilikuwa nahitaji vitatu tu foundation planning, elevation planning na roof planning asubuhi namwambia atumie alipofikia anatuma vipicha vya ajabu ajabu na vitu simple tu.

Nikampiga fundi akasema napoteza pesa, nikaona kweli mimi ni IT nikaona hakuna kitu kipya nikakaa na fundi tukachora ramani tena nzuri sana nikasave pesa...niligundua architecture wengi wababaishi na kazi ukikaa na fundi mzoefu unachora ramani nzuri bila gharama.
Ndicho kilichonitokea,nilipata mkopo wa nyumba moja ya shart lilikuwa ni kibali cha ujenzi ambacho ili kipatikane ni lazima uwe na ramani na plot yenye hati.(kama ingezingatiwa hii kusingekuwa na makazi holela nchini)
Basi nikamtafuta fundi nikampa idea yangu akawa anataka afike site nikamuonesha hati yangu yeye aingize tu vipimo basi ukawa ni ugomvi,nikamkomalia achore tu,basi draft zikawa nyingi halafu ni mlalamishi madeko yaani anajiona kafika.wakati mimi nimekulia kotazi za aina tatu tofauti,ndugu zangu wanaishi NHC na miramani yao ni mazuri tu.basi nikamuomba niwekee gebo hapo mbele au we boss unapenda vitu vya kizamani yaani huna nzuri hata moja la kunisifia we ni mikasoro tu.hapa unajua inapendeza halafu ramani yako nimemaliza siku nyingi ila we ni makasoro tu.nikaibeba
Kila siku nikiangalia nabaki najiuliza hivi alishindwa nini kutoa kabati za ukutani kama zile nyumba za NHC.? YAANI KABaTi ununue au ujengee.
Basi siku hizi najicholea tu mwenyewe na mpauji huangalia ramani ya chini biashara imeisha
 
Habarini wakuu.

Hivi ni kwanini watu hujenga kwa ramani za kufikirika tu zisizokuwa na mpangilio wa kitaalamu. Yaani umejibana kukusanya milioni zako flani, unamtafuta fundi na kumtajia idadi ya vyumba tu ajenge au unampa mfano wa ramani uliyoipata kwenye mtandao.

Hebu fikiria umetumia milioni zako kadhaa kuinua mjengo, halafu baada ya kuhamia na kuanza kupigwa na jua, huku ‘ventilation’ ikiwa mbaya yaani upepo ukipiga upande usio na vyumba, ndio unagundua kwa ‘proper zoning’ chumba chako kilitakiwa kikae mahali ilipo public toilet, au dining au store+jiko.

Pia unagundua kuwa unakosa faragha (privacy) kwa wageni na changamoto nyingine nyingi.

Ni rahisi sana kulitambua hilo ukianza na ramani yako kwa kuleta wataalamu kwenye kiwanja chako, ili utengenezewe ramani kulingana na kiwanja chako na mahitaji yako.

Ungeweza kujenga kwa ramani ileile ulioipenda lakini ikahitaji mabadiliko kidogo sana iendane na kiwanja chako na kukufanya ufurahie uwekezaji wako.

Unaweza kutucheki kwa namba 0717682856 tuje kufanya 'site analysis' upate kilicho bora kwa uwekezaji wako
Tatizo wengi hawana uelewa wa ramani raia wengi wanategemea mafundi wafanye draft kwenye karatasi na wanajua hiyo ndiyo ramani.
Kama mtu amejipanga kuanza ujenzi hawezi kushindwa kumtafuta mtaalamu amchoree ramani ya nyumba tatizo ni ufahamu mdogo wa mambo ndio hupelekea sehemu kubwa kutohitaji wataalamu na ramani!
 
Tangazo lako umeingia nalo vibaya kwa kuanza kuponda..wewe mwenyewe hizo ramani unacopy na kuzimodoa halafu unasema zako.
Ungeenda moja kwa moja kwa kutangaza bidhaa yako.
 
Back
Top Bottom