GOSSO MZEKEZEKE
Senior Member
- Dec 13, 2013
- 180
- 204
Habari wanaJF.
Naomba kwa yeyote anayejua sababu zilizopelekea mamlaka ya mapato Tanzania yaani TRA kuajiri wenyewe aniambie?
Kusema ukweli ajira zinazopita utumishi ziko fair sana. Nimeshuhudia watoto wa maskini kabisa wakipata ajira TRA tena bila connection yoyote. Utumishi japo wana mapungufu yao mengi lakini wanakwenda angalau kwa haki. Sina maana kwamba hakuna ukiritimba au ajira za kujuana, naamini zitakuwepo ila kwa asilimia chache sana.
Sasa kitendo cha kurudisha ajira kwa TRA kuna lengo gani? Mimi naamini TRA kujuana kutakuwa kwingi sana, watu watakaokuwa wakiajiriwa watakuwa wa vigogo tu. Labda Utumishi wangetuambia sababu za kurudisha kibali kwa TRA ni zipi maana mamlaka ya kisheria ya kuajiri ni yao.
Mwenye kujua sababu za TRA kurudishiwa kibali cha kuajiri aniambie, na je unadhani kutakuwa na fairness kama ilivyo utumishi?