Maswa Yetu
JF-Expert Member
- Mar 18, 2023
- 1,398
- 2,619
Rais Samia kipindi inatangazwa kwamba bwawa la Mwl Nyerere litakapokamilika bei ya umeme itashuka chini wewe ulikuwa makamu wa rais na bila shaka mlikubaliana hivyo kwenye vikao, sasa bwawa la umeme limekamilika na mashine zote zinafanya kazi lakini kuna kila dalili serikali yako ya awamu ya sita haitaki kushusha bei ya umeme!, ina maana umesahau kama mliahidi kushusha bei ya umeme au haujui faida za umeme wa nchi kuwa bei ndogo?
Umeme ukiwa wa bei ndogo viwanda vingi vitajengwa, ajira zitapatikana , bidhaa za viwandani zitakuwa bei ndogo hivyo maisha yatakuwa bora kwa wananchi wote. Watu wataacha kupikia kuni na kuokoa misitu yetu, nchi jirani watafurika Tanzania kufuata bidhaa maana zitakuwa za bei ndogo.
Rais Samia tunataka umeme ushuke bei na hatutasikiliza kisingizio chochote.