Ni sababu zipi zinazomfanya Rais Samia ashindwe kushusha bei ya umeme?

Maswa Yetu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2023
Posts
1,398
Reaction score
2,619
Rais Samia kipindi inatangazwa kwamba bwawa la Mwl Nyerere litakapokamilika bei ya umeme itashuka chini wewe ulikuwa makamu wa rais na bila shaka mlikubaliana hivyo kwenye vikao, sasa bwawa la umeme limekamilika na mashine zote zinafanya kazi lakini kuna kila dalili serikali yako ya awamu ya sita haitaki kushusha bei ya umeme!, ina maana umesahau kama mliahidi kushusha bei ya umeme au haujui faida za umeme wa nchi kuwa bei ndogo?

Umeme ukiwa wa bei ndogo viwanda vingi vitajengwa, ajira zitapatikana , bidhaa za viwandani zitakuwa bei ndogo hivyo maisha yatakuwa bora kwa wananchi wote. Watu wataacha kupikia kuni na kuokoa misitu yetu, nchi jirani watafurika Tanzania kufuata bidhaa maana zitakuwa za bei ndogo.

Rais Samia tunataka umeme ushuke bei na hatutasikiliza kisingizio chochote.
 
Mtu aliye zungukwa na mafusadi na ameyakubatia na kunywa nayo mvinyo kama ndio ngao na wasaidizi wake usitegemee atageuka kutazama wananchi wanatabu gani.
 
Ngoja nikamuulize kwanini inakuwa ngumu kushusha bei za unit za umeme,, nitarudia kuwapa mrejesho!
 
Nchi hii Hata kila Mkoa ukawa na Stiglers yake ya Umeme, kama ccm bado ipo hakuna nafuu yoyote Wananchi watapata
 
ROSTAM AZIZ NA GENGE LAKE
 
Lita moja ya petroli ina kodi na tozo zaidi ya 150.
Umeme utakuwa na tozo na kodi 160
 
Ulishaambiwa kama hutaki kulipa tozo hama tena ulishaelekezwa wapi kwa kuhamia ili usiumize kichwa chako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…