Ni sahihi kabisa kusema kuwa CCM ya sasa ni "CCM ya Magufuli"

Ni sahihi kabisa kusema kuwa CCM ya sasa ni "CCM ya Magufuli"

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
12,505
Reaction score
40,002
Hatimaye Magufuli amefanikiwa kuiweka CCM mfukoni mwake, tena mfuko wa shati huku akiibeba na kutembea nayo kwa bashasha na makeke mwake.

CCM ya sasa inaulizwa kilichopendekezwa na mwenyekiti tena kwa maneno "Si ndivyo jamani?" Kuwarahisishia wapwa na wakulungwa waliojazana humo kwa lengo la kuinuliwa, kutawanywa na kukusanywa ikitegemea mood kabambe ya mwenyekiti. Hakuna tena mwenye ubunifu wala uhojifu chamani bali kwa mtukufu aliyetanda kama mkufu.

CCM imekuwa kama watoto wa kindagateni na mwalimu wao huku wakifwatisha maneno ya mwalimu bila kuyumba wala kunyumbua. Ukijifanya kuhoji unaambiwa haukubaliki kama dobi kwa kaniki na unaishia kuufyata kama kiazi mbatata kwa JIWE!

Poleni wanaccm, hatimaye kimekuwa chama cha Magufuli bila mtutu wala tofali na wote waliomo ni wake, anawapanga na kuwapangua atakavyo ili mradi mapenzi yake yatimizwe kuanzia Kisiwandui mpaka Burigi.
 
Yaani upo sahihi kabisa ccm imekuwa ni ya mtu binafsi,akina mzee Makamba,Kinana,Membe wametukanwa na Msiba lkn wameishia wao kuomba msamaha,Membe ndio kaishia kufukuzwa kisa kuwa mkweli,leo ccm imekuwa ni watu ndio tu,tumsameahe Kinana ndio,tumpe azabuu ndio,hakuna wakupinga.
 
Chama amekikamata kisawasawa lakini pia naona vikao vyenyewe havina mvuto jana nilifuatilia nilivyowaona wajumbe ukumbini wengi walijawa na huzuni
 
[emoji23][emoji23][emoji23]umenikumbusha dogo wangu wa nursery school, kwamba wanachama wako kama dogo wangu, hawezi kuhoji bali kumeza tu
 
Ni kawaida kuwa hivo chama kinapompata kiongozi sahihi mwenye maono ya kuivusha nchi kutoka tulikokuwa kwenye enzi za UFISADI, Vyeti feki, wafanyakazi hewa maESCROW nk nk hadi kufika enzi za kujenga nidhamu, uwajibikaji na maendeleo hadi kuifikisha nchi ilipo na World Bank kukiri TZ tunsonga mbeleeee!
Na ATAKE ASITAKE 2025 tutam-"putin" tu. Tusije tukaletewa akina FARU JOHN tukajuta.
 
Yaani upo sahihi kabisa ccm imekuwa ni ya mtu binafsi,akina mzee Makamba,Kinana,Membe wametukanwa na Msiba lkn wameishia wao kuomba msamaha,Membe ndio kaishia kufukuzwa kisa kuwa mkweli,leo ccm imekuwa ni watu ndio tu,tumsameahe Kinana ndio,tumpe azabuu ndio,hakuna wakupinga.
Walionywa awakusikia kwamba katiba yao ni kitanzi Chao wakaweka pamba,waliambiwa waondoe kofia mbili wakaweka pamba leo wametukanwa,wamedhalilishwa,wamefukuzwa na mfumo ule ule walioweza ubadili walipokuwa na nafasi hawakusikia, makamba's wamesomeshwa namba wamebatizwa kwa moto wa makaa ya mawe wamepotea.
Leo chama ni Mali binafsi mmiliki wake ndie mwenye maamuzi Nani agombee Nani asugue benchi.
 
Ni kawaida kuwa hivo chama kinapompata kiongozi sahihi mwenye maono ya kuivusha nchi kutoka tulikokuwa kwenye enzi za UFISADI, Vyeti feki, wafanyakazi hewa maESCROW nk nk hadi kufika enzi za kujenga nidhamu, uwajibikaji na maendeleo hadi kuifikisha nchi ilipo na World Bank kukiri TZ tunsonga mbeleeee!
Na ATAKE ASITAKE 2025 tutam-"putin" tu. Tusije tukaletewa akina FARU JOHN tukajuta.
Mnufaika
 
Mtu makini au mmebanwa zamu yenu kusomeshwa namba mlifurahi Sana wapinzani kushughulikiwa hili bado trela
 
The fate of CCM is similar to the fate of the Republican Party under Donald Trump!!! Hopefully, Donald loses in November and God willing the similarity will not end there!!!
Trump hakustahili walimpa tu sababu alisimamishwa na Clinton.
Arudi tena kipindi cha pili.
 
Mtu makini au mmebanwa zamu yenu kusomeshwa namba mlifurahi Sana wapinzani kushughulikiwa hili bado trela
Mkuu tatizo la nchi yetu haikuwa Upinzani. Tatizo ilikuwa ni CCM ya KIFISADI. Ndio maana 2015 mabango yaliandikwa chagua MAGUFULI na sio chagua CCM.
Huyu jamaa kaja kufanya kazi ambayo upinzani ilikuwa inaulalamikia CCM. Ni kweli waathirika wakubwa wa serikali ya Magufuli ni wanaCCM ile ya KIFISADI. - Wapinzani wanapapaswa tu! sema wana makelele kuwashinda akina Kinana walioshughulikiwa HASA!
 
Back
Top Bottom