Ni sahihi kujinunulia majeneza na kujijengea kaburi?

Ni sahihi kujinunulia majeneza na kujijengea kaburi?

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Hii dhana ya kujinunulia majenezo au kujijengea makaburi kabla ya kifo chako, kwa kisingizio eti ukifa usije kusumbua watu katika michango.

Hii imekaaje wakuu? Ni sawa kufanya hivyo?
 
Huu mtindo wa kujiandalia vifaa vya mazishi unaanza kushika kasi, kuna mama mmoja hapa tayari kajinunulia sanda, pamba na pafyumu kitu ambacho kimeleta kizaazaa kwenye familia yake akionekana anajichuria kifo na kuzusha minong'ono kwa familia yake wakihoji kwani ameona familia yake haitanunua hivyo vifaa atakapofariki dunia? Ajabu ni pale mtu atakapojinunulia sanduku la kuzikiwa halafu lije lipitwe na fasheni na ubora
 
Sio Sahihi kuwapangia watu maisha; Kwahio watu wakiamua kufanya hayo its all good...;

Tena nashauri watu waanze kufanya kabisa funeral preparations (costs-wise) kama wana uwezo; Death is inevitable

Na wale wenye mpango wa kujiua waende wakajiue kabisa huko watakapozikwa na ikibidi waache wameandaa kila kitu na kama wanasafirishwa wajisafirishe kabisa mpaka sehemu husika (na kama wana wategemezi waache costs za malezi) kama wakishindwa kufanya hayo basi waendelee kuishi....
 
Huu mtindo wa kujiandalia vifaa vya mazishi unaanza kushika kasi, kuna mama mmoja hapa tayari kajinunulia sanda, pamba na pafyumu kitu ambacho kimeleta kizaazaa kwenye familia yake akionekana anajichuria kifo na kuzusha minong'ono kwa familia yake wakihoji kwani ameona familia yake haitanunua hivyo vifaa atakapofariki dunia? Ajabu ni pale mtu atakapojinunulia sanduku la kuzikiwa halafu lije lipitwe na fasheni na ubora
Sasa wewe ndio una mawazo ya Kipekee kabisa... (Duh Fashion hadi Sanduku)?!!!

Anyway to each his/her own....
 
Hii dhana ya kujinunulia majenezo au kujijengea makaburi kabla ya kifo chako, kwa kisingizio eti ukifa usije kusumbua watu katika michango.

Hii imekaaje wakuu? Ni sawa kufanya hivyo?

Kama kuandaa wosia ni sawa, basi hata kujinunulia hayo majeneza na kujijengea makaburi mazuri na ya kisasa, pia ni sawa.
Maana kufa kupo tu. Yaani kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke siku yake ya kifa ikifika, basi atakufa tu.

Kwa hiyo kama una hela, ni bora na wewe ukaanza maandalizi mapema! Ili kutupunguzia michango ya kukuchangia.
 
Kwa upande Wangu mm,,, naona si-sahihi,,, na kama yeye ataona Ni sahihi kufanya ivyoo,,, Ingekuwa vizuriii hata siku hakifa akajizike mwenyewe,,, asitupotezeee MDA WETU,,,,,
 
Angalia huyu hapa Equation x alichofanya 👇🏿.
 
Hata Yesu alizikwa kwenye kaburi lililoandaliwa in advance japo halikuwa lake
 
Back
Top Bottom