Kwa % kubwa upo sahihi. Ila pia sababu haya mambo hayana Fomula, unaweza pata mmepishana miaka michache na mambo yakaenda. Tena wapo watu wameoa mwanamke mwenye umri mkubwa na wapo vizuri tu. Ila ni exception za maisha, kwa % kubwa unalosema ni sahihi.
Sasa ujue ni nini mkuu?
Kwasasa wanaostahili ndoa hawataki ndoa.
Wasiostahili ndoa wanazitaka ndoa.
Umeiona dunia tuliyo nayo sasa hivi?
Kuna binti mmoja ni singo maza hapa nilipo,,
Kakitembeza hadi father house akamuachia usimamizi kwenye mijengo yake huku
So kifupi kana mamlaka juu yangu
On top of that kana mzee mmoja hivi ana ndinga yake huwa anakuja hapa anabandua anapita hivi..
Sasa haka kamtu bana kanatamani sana kaolewe lakini ukiangalia circle yake hakastahili ndoa japo kanaitaka sana.
Sasa wewe waza kijana wako ndie atumbukie kwa haka kabinti ghafla kitamkuta nini?
Na haka ndio sababu ya mpaka wife kuachika kwangu..
Maana ni kasimbe hakashindwi kumlengesha wife kibra huku kakimuaminisha kuwa kenyewe kanainjoi sana mwisho nilishangaa mwanamke anasepa na kusema anaenda kufanya maisha yake.
Baada ya wife kusepa haka kabinti kakaanza kuniambia ujue mimi sina gharama kabisa.
Ukipata mtu huko anataka mke wa kuoa mwambie nipo hapa nina mtoto mmoja na sina gharama.
Nikamcheki tu nikampa pesa ya umeme nikaishia town.
Kamekuwa kakifuatilia kujua kama nitamrudisha wife nakaambia noo.
Mtu akisaliti kambi akakaa zaidi ya miezi sita hastahili msamaha..
Kanakazia yaani kabisa usije ukamsamehe maana ameshakuwa paka pori tayari..
Nawaza tu sijui katajisikiaje siku naingiza mwanamke mwingine ndani
Huku kakiwa kanatarajia kuwa kama sio mimi kumrudisha wife basi nakaingiza ndani kenyewe..
Unaweza kuona ni changamoto kiasi gani inatukabili kwenye huu ulimwengu wa sasa..
Yaani ikitokea ukajitoa ufahamu ukatangaza nafasi ya kuolewa utashangaa wanaleta barua za maombi hata wale unaowaona wanadanga na wazee wenye pesa zao mjini.
Wenyewe wanakwambia hakuna kitu kitamu kama kumiliki mume ambae hata ukikuta kasimama na Aisha unamfumua Aisha na jamii yote inakusapoti..