Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Unapompiga Risasi hafi moja kwa moja.. una msogeleaaa/unamuwah unachinja.. hakikisha anakuwa bado hajafa..
Hata kama alikufa ila muwindaji muislamu kama alipiga Bismillah kabla basi Hana shida huyo
 
Mimi nachinja mwenyewe ukija nakwambia ukitaka kula ukitaka acha......nikija kwako nakula vizuri tu sana mno na sitakufa.....complication nyingine hazifai .....
 
Hilo liko wazi kwa hapa Tanzania. Ninachojiuliza tu ni huwa wanafanyaje pindi wawapo kwenye nchi zisizo na huo utaratibu?

Je, bidhaa imported zilizotokana na nyama kama soseji wanafanyaje?
Ukienda huko unakuwa vegetarian au unakomaa na seafood tu au unatafuta maduka ya halal food
 
Pombe wanakunywa sembuse nyama tena ya kuku. Wengine hata kitimoto wanakula.
 
Sasa Wakristo wanakula wanyama waliokufa wenyewe au wanachinja? Kwanini Wafia dini wa kiislam hawali nyama ya mnyama aliyechinjwa na Mkristo ilihali sio kibudu?
 
Sasa Wakristo wanakula wanyama waliokufa wenyewe au wanachinja? Kwanini Wafia dini wa kiislam hawali nyama ya mnyama aliyechinjwa na Mkristo?
Uislamu ni mfumo mzima wa maisha ya mwanadamu,una taratibu zake na sheria zake

Ili kichinjo kiwe halal hakina budi kuchinjwa na muislamu ambaye anamwamini Allah mmoja asiyeshirikishwa na yoyoye katika ufalme wake

Kuchinja ni ibada na inataratibu zake,ikiwa ni pamoja na kuelekea kibla wakati wa kuchinja na kutaja jina la Mwenyezi Mungu

Kwakuwa wasio waislamu hawana taratibu hizi basi ni haramu kula mnyama aliyechinjwa nje ya taratibu za kiislamu
 
Hatakufa, lakini unafikiri atakuchukuliaje siku akigundua kuwa ulimlisha "haramu" kwa makusudi?

Masuala ya imani yapo very complicated. Si ya kuyachukulia kirahisi.
Haramu kwa maana kwamba umemlisha nguruwe kwa makusudi au ulikuwa na maana nyengine?

Na kwanini kwanza mimi Mkristo nimlishe kwa makusudi mwenzangu kitu asichokitumia?unadhani sitakuwa na busara ya kuamuru kipikwe chakula kingine kwa ajili yake au iwepo option anywe maji au juice maisha yaende?
 
Sawa, sio vibaya wasipokula
 
Karibu sana. Huyu kuku nimemchinja mwenyewe. Pole sana ngoja nikuandalie mabamia
 
Kuna shida Gani?

Kuchinja sio kuua?

Unajua logic za Dini sometimes ni ujinga sana😂😂😂 so ua Lakini ua kistaarabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…