Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Ni sahihi kumkaribisha Muislamu nyama ambayo haikuchinjwa kidini?

Ila mara nyingi wakati wa kugonga menyu/kumkaribisha mtu msosi hakuna kuuliza mtu hapo ni mwendo wa kula tu

Ova
 
Sasa Wakristo wanakula wanyama waliokufa wenyewe au wanachinja? Kwanini Wafia dini wa kiislam hawali nyama ya mnyama aliyechinjwa na Mkristo ilihali sio kibudu?
Sasa mbona huelewi umeambiwa wapi wakristo wanakula ? Nionyeshe wapi waislamu wamekatazwa kula nyma iliyochinjwa na mkristo kama sio kukosa elimu.

Nimekuambia nyama ambao haweza kula muislamu hata mkristo kakatazwa.
 
Si Bora huyo aliyechinjwa na mkristu.
Kuna mmama mmoja hapa jirani akitoa kuku kwenye Banda anamshika miguu na kugonga kichwa ukutani kisha anatupa kule. Baadaye anachukua vile vibudu na kuondoa vichwa manyoya na miguu na vya ndani. Kisha sokoni.
 
Kuna shida Gani?

Kuchinja sio kuua?

Unajua logic za Dini sometimes ni ujinga sana😂😂😂 so ua Lakini ua kistaarabu
Kuchinja sio kuuwa kwa kistaarabu, hekima ya kuchinja ni kukata kuruhusu damu itoke kwenye mshipa mkuu ule
 
Muislam anaruhusiwa kula alichochinja asiyekuwa Muislam. Ila tu mchinjaji awe amechinja kweli. Wasio waislam wana tabia ya kuwapiga wanyama au kuku wanamtumbukiza kwenye maji moto anakufa kisha wanaanza kumkata kata. Muislam hali kibudu tu, kitu ambacho hakikuchinjwa. Kama umechinja vizuri kabisa yafaa kula.
Heee yaani nimtupie tu kuku kwenye maji moto bila kuchinja
 
Kuchinja sio kuuwa kwa kistaarabu, hekima ya kuchinja ni kukata kuruhusu damu itoke kwenye mshipa mkuu ule
🤣 🤣 🤣

But ukichinja unakuwa umetoa Maisha ya kiumbe mwingine.

You guys mnahangaika sana kutetea kitu ambacho hakuna tofauti ya kimantiki inayoletwa na kitendo Cha muislam au asiye muislam kuchinja.

Kuchinja ni kuua, na wanyama wote tuna wachinja kwa ajili ya chakula huwa tunawanunua kutoka kwa wafugaji ambao main purpose ni kutoa Maisha yako whenever tukitaka
 
Kuna mmoja alikuja kwangu akatengewa ugali na nyama ya Bata halafu akaanza kuhoji ooh samahani bro kwani nani kachinja huyu Bata nikamwambia Mimi akasema basi Mimi nimeshiba naomba maji tu ninawe nikamwambia jaba lile pale na kikombe kipo hapo nawa tu maana alishafinyanga tongue mbili halafu nikamsindikizia na Aya moja ya suratul qaafiroon
LAKUM DEENUKUM WALIYA DEENI.
😂😂😂😂
Sielewi upumbavu mimi
Jamani jamani........😅😅😅😅😅😅
 
🤣 🤣 🤣

But ukichinja unakuwa umetoa Maisha ya kiumbe mwingine.

You guys mnahangaika sana kutetea kitu ambacho hakuna tofauti ya kimantiki inayoletwa na kitendo Cha muislam au asiye muislam kuchinja.

Kuchinja ni kuua, na wanyama wote tuna wachinja kwa ajili ya chakula huwa tunawanunua kutoka kwa wafugaji ambao main purpose ni kutoa Maisha yako whenever tukitaka
Mada hapa ni kuchinja, kuuwa kwingine kusikokuwa kuchinja sio hoja husika.
 
Back
Top Bottom