Ni sahihi kumuheshimu boss wako/ Mchungaji/Sheikh /Padre kuliko Mumeo/Mkeo?

Ni sahihi kumuheshimu boss wako/ Mchungaji/Sheikh /Padre kuliko Mumeo/Mkeo?

Hahaha pastor anahudumiwa kuliko mwenye mali 🤣🤣🤣
Mungu atusaidie kwakweli, wake za wachungaji mioyo wanayo!! Maana kila kondoo anavyomchangamkia mchungaji utaskia "yes, dady "
 
Maisha ni haya ukae kujua ukiwa nyumbani kama wewe ni mwanaume heshimu mke wako , kama ni mwanamke muheshimu mume wako, kama upo kanisani halijiendeshi lenyewe Lina wafanyakazi wake basi weka heshima ili uheshimiwe, hata mbwa wako home muheshimu, ili asije akaacha kuhudumia , kila mahali heshimu watu. Vitu wanyama wanyumbani hata paka mweshimu.
Amina
 
Respect is earned, mzee. Watu watakuchukulia namna unavyowaruhusu wakuchukulie. So basically, shida iko kwako.
 
kutana naye ofisini /sehemu ya ibada
Utasema mwanamke ndiye huyu! Anavyomnyenyekea boss wake, utasema ana heshima Sana. Boss ataulizwa nikupe chai au kahawa? Kuna kitu unahitaji, tabasamu Kama lote. Ushawahi kukutana na wadada wa customer care? Utasema hapa ndiyo penyewe [emoji16]

Kanisani nako unyenyekevu upo sana, tena usiombe umkute kwenye "ibada ya kukanyaga mafuta [emoji3]" akiambiwa vua viatu,anavua Hakuna maswali anatii. Kuna lugha huwezi kuzisikia mwanamke akizitoa kwa pastor wake. Ukikutana naye hapo utasema umepata dodo kwenye mchongoma

WAKIJA NYUMBANI SASA! LORD HAVE MERCY.
ukisikia jinsi mtu anamjibu mme wake utauliza hivi, huyu ndiye fulani wa pale kanisani? Ni unafiki au kitu gani ndugu zangu kwanini heshima mnayoitoa huko msizidishe nyumbani?

Nawasubiri hapa na Fanta pineapple ya Baridi

Alafu mnaowaheshimu sana sio wote baadhi ni WAOVU NYUMA YA PAZIA. Kwenye uhusika wao ndio mnawaona watu. Tena wengine WARUKA NA UNGO USIKU.
 
Respect is earned, mzee. Watu watakuchukulia namna unavyowaruhusu wakuchukulie. So basically, shida iko kwako.
Tujifunze basi kwa wachungaji kuearn respect, maana hili ni janga la taifa!! Mpaka unajiuliza au kaolewa na kanisa?
 
Alafu mnaowaheshimu sana sio wote baadhi ni WAOVU NYUMA YA PAZIA. Kwenye uhusika wao ndio mnawaona watu. Tena wengine WARUKA NA UNGO USIKU.
Watu wanafiki Sana mkuu
 
Tujifunze basi kwa wachungaji kuearn respect, maana hili ni janga la taifa!! Mpaka unajiuliza au kaolewa na kanisa?

Huitaji kujifunza kwa mtu. Jiheshimu mwenyewe, na hiyo inatosha. Kujiheshimu ni kujitoa katika mazingira unayodhani huheshimiki.
 
Kutosimama kama mwanaume kwa wengi means kutokuwa na pesa.
Wanawake wachache sana uwaheshimu waume zao wasio na kitu.
Heshima ni matokeo ya malezi.Kama hakufunzwa heshima kwao huwezi mbadilisha
Usije ukadhani wenye hela hawadharauliwi na wake zao..!!
 
Back
Top Bottom