Kuna maswali mawili ndani ya swali moja:
1: Kunywa dawa na baadaye kunywa maziwa.
2: Kunywa dawa kwa kutumia maziwa.
Jibu ni:
Inategemea aina ya dawa:
1: Kuna dawa kulingana na zilivyotengezwa na vilivyomo, zinayeyuka vyema kwenye maziwa. Hivyo, hurahisisha dawa kufyonzwa na kuingia mwili.
2: Kuna dawa kwa jinsi zilivyotengenezwa na vilivyomo, vikikutana na maziwa hutengeneza mchanganyiko ambao mwili hauwezi kufyonza dawa husika. Hivyo, dawa nyingi hupitiliza na kufanya lengo la dawa kutofikiwa.
Mtoa huduma ya afya huweza kushauri, dawa hii ukitumia kunywa maziwa ni jambi jema au usinyewe maziwa unapotumia dawa hii.
Kwa msingi huo, usimpe mtu maziwa kama amekunywa sumu iwapo hujui SUMU husika INAYEYUKA vyema kwenye maziwa. Maana badala ya kumuokoa unaweza KURAHISISHA KIFO kwa kusababisha sumu kufyonzwa vyema.