Ni sahihi kuomba maombi yako ya kawaida kwa sauti kubwa?

Ni sahihi kuomba maombi yako ya kawaida kwa sauti kubwa?

Lanlady

JF-Expert Member
Joined
Feb 27, 2019
Posts
1,836
Reaction score
6,303
Kwa nijuavyo kuna aina tofauti za maombi. Maombi binafsi yanayohusu haja zako binafsi. Kuna maombi ya jumla kuombea watu wengine mfano uponyaji na kuna maombi ya vita kama vile kukemea hali fulani.

Swali langu kwa waombaji, je ni sahihi kutumia kipaza sauti wakati wa kuomba maombi binafsi?
 
Halafu hiyo ni moja ya Sababu naenda kanisani kwa kuhesabu...kelele
Yaan unafanya maombi, uwepo wa Mungu unakuwa haupo baina yenu .. kelele
Yaan kelele jaman ..sidhani kama roho mtakatifu anakaa mahali penye fujo .🙌
 
IPO - hakuna maombi ya VITA
Ila ukijiona unakuwa na misfortunes, haufanikiwi n.k jaribu kuifuta hiyo hali na sio kukemea.

Kuhusu maombi binafsi na kuombea WATU , kinacholeta nguvu ni ile kuombea WATU mema na sio kujiombea wewe binafsi . hapa itakurudia hiyo karma kwa haraka .

So hamna maombi ya VITA na ukifanya hivi utakuwa unakosea kuomba ukipiga positive usiweke na negative.

Kuhusu kutoa sauti au kimya - hii haina madhara yoyote .
 
...Sifa au kigezo kikuu Cha kuomba/mombi Ni unyenyekevu au kunyenyekea.

Mtoto anapomuomba Baba yake kitu , anaomba kwa makelele? Si lazima aonyeshe utulivu?

Ndivyo maombi kwa Mungu nayavyohitaji, lazima uwe katika utulivu wa Hali ya juu Sana maana unayozungumza nae Ni mkuu Sana tofauti na wengi wanavyomfikiria Mungu .

Maombi kwa makelele/maombi kwa kujionyesha Ni sawa na kupiga makelele kwenye Kiko chako.
Mungu mwenyewe alisema , Unapotaka kusali nenda katika chumba chako Cha Siri unapoishi na ufanye maombi humo.

Kila la kheri.
 
Kwa nijuavyo kuna aina tofauti za maombi. Maombi binafsi yanayohusu haja zako binafsi. Kuna maombi ya jumla kuombea watu wengine mfano uponyaji na kuna maombi ya vita kama vile kukemea hali fulani.

Swali langu kwa waombaji, je ni sahihi kutumia kipaza sauti wakati wa kuomba maombi binafsi?
Maombi yenye nguvu na uvuvio wa kiroho hayana na hayataki kelele
 
IPO - hakuna maombi ya VITA
Ila ukijiona unakuwa na misfortunes, haufanikiwi n.k jaribu kuifuta hiyo hali na sio kukemea.

Kuhusu maombi binafsi na kuombea WATU , kinacholeta nguvu ni ile kuombea WATU mema na sio kujiombea wewe binafsi . hapa itakurudia hiyo karma kwa haraka .

So hamna maombi ya VITA na ukifanya hivi utakuwa unakosea kuomba ukipiga positive usiweke na negative.

Kuhusu kutoa sauti au kimya - hii haina madhara yoyote .
Umeandika kisomi mnoo!Uwe unaturahisishia na kwa mifano muheshimiwa.
 
Kwa nijuavyo kuna aina tofauti za maombi. Maombi binafsi yanayohusu haja zako binafsi. Kuna maombi ya jumla kuombea watu wengine mfano uponyaji na kuna maombi ya vita kama vile kukemea hali fulani.

Swali langu kwa waombaji, je ni sahihi kutumia kipaza sauti wakati wa kuomba maombi binafsi?

Hakuna formula ya namna ya kuomba...

Mathalani, Biblia kupitia chuo cha Isaya imeandikwa, "njooni tusemezane...", sasa kuna kusemezana kusiko na sauti?

Isaya 1:18
Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.

Ukisoma zaidi, Biblia kupitia chuo hicho hicho cha Isaya kimeandika kuhusu namna ya kupeleka hoja zako kwa Mungu kwa namna ya maneno, sasa je kuna namna ya kutoa hoja kwa maneno kimya kimya?...

Isaya 41:21
Haya, leteni maneno yenu, asema BWANA; toeni hoja zenu zenye nguvu, asema mfalme wa Yakobo.

Isaya 43:26
Unikumbushe, na tuhojiane; eleza mambo yako, upate kupewa haki yako.

Zaidi Biblia kupitia chuo cha Mathayo inataja namna nyingine ya kusali kwa ukimya...

Mathayo 6:6
Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
 
Back
Top Bottom