Ni sahihi kuomba maombi yako ya kawaida kwa sauti kubwa?

Ni sahihi kuomba maombi yako ya kawaida kwa sauti kubwa?

Unatakiwa upige maombi ya kuwehuka namna hii...👇🤣
FB_IMG_1732610045410.jpg
 
H
Huna roho mtakatifu wewe!Fumba macho uombewe.Pokeaaaa hata kama ni maji ya kunywa.
Huko nilishatoka mkuu, mtu akijizatiti kuomba hewa anajenga kwenye akili tumaini hewa na kujisahaulisha changamoto , ndio anaona tayari huyo roho mtakatifu ameshamshukia , matatizo yapo pale pale , magonjwa na kifo kipo pale pale, omba usiombe hakuna utakachobadilisha, nanyi farijianeni kwa maneno hayo tu, 1wathethalonike 4-18.
 
Kuna dada yetu,tunapokutana kifamilia na familia zetu,hakuna anayetaka ku share nae room ya karibu yake ...maana asub anamkemea shetani kwa sauti aisee ni sauti ya juu.

Watu hawamjui shet, shet hata malaika wanamgwaya halafu wewe unamkemea.Mwombe Mungu akulinde tu ,shetani anahudhulia mbele za Mungu
 
Kwa nijuavyo kuna aina tofauti za maombi. Maombi binafsi yanayohusu haja zako binafsi. Kuna maombi ya jumla kuombea watu wengine mfano uponyaji na kuna maombi ya vita kama vile kukemea hali fulani.

Swali langu kwa waombaji, je ni sahihi kutumia kipaza sauti wakati wa kuomba maombi binafsi?
Sio Lazima, soma Mathayo 6
 
Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
7 Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
 
IPO - hakuna maombi ya VITA
Ila ukijiona unakuwa na misfortunes, haufanikiwi n.k jaribu kuifuta hiyo hali na sio kukemea.



Kuhusu maombi binafsi na kuombea WATU , kinacholeta nguvu ni ile kuombea WATU mema na sio kujiombea wewe binafsi . hapa itakurudia hiyo karma kwa haraka .


So hamna maombi ya VITA na ukifanya hivi utakuwa unakosea kuomba ukipiga positive usiweke na negative.


Kuhusu kutoa sauti au kimya - hii haina madhara yoyote .
Maombi ya vita yapo. Mfano kama unasoma biblia kuna mahali Petro alipiga kelele kuomba msaada ili asizame. Na pia kuna kipofu alipiga kelele kuomba uponyaji.

Unaweza kuwa umelala usiku, ghafla unashtuka hupati hewa ya kutosha ilihali madirisha yapo wazi. Hapo sidhani kama utaomba kawaida maana hiyo ni vita.
 
Maombi ya vita yapo. Mfano kama unasoma biblia kuna mahali Petro alipiga kelele kuomba msaada ili asizame. Na pia kuna kipofu alipiga kelele kuomba uponyaji.

Unaweza kuwa umelala usiku, ghafla unashtuka hupati hewa ya kutosha ilihali madirisha yapo wazi. Hapo sidhani kama utaomba kawaida maana hiyo ni vita.


Ndo maana watu wa dini nyie mapepo, mikosi, umaskini , magonjwa , huwa havikauki kwenu .

Ukiamka ukakuta Pumzi imebana fatilia Afya yako na omba Mungu akupatie Utulivu calmness .


Usimuombee MTU mabaya wala usihangaike na kumkemea shetani
 
Unaweza kuomba kwa sauti.
Halafu ukichoka kuomba kwa sauti unaweza kuomba kwa kunong'ona( whisper)
Ukichoka kunong'ona unaweza kuomba kimoyomoyo( mental ).
Ni kama kusoma, unaweza kusoma kwa sauti
Au kusoma kwa kunong'ona
Au kusoma mentally.
Au kusoma bila verbal or mental recitation.
 
Back
Top Bottom