Ni sahihi kuomba maombi yako ya kawaida kwa sauti kubwa?

H
Huna roho mtakatifu wewe!Fumba macho uombewe.Pokeaaaa hata kama ni maji ya kunywa.
Huko nilishatoka mkuu, mtu akijizatiti kuomba hewa anajenga kwenye akili tumaini hewa na kujisahaulisha changamoto , ndio anaona tayari huyo roho mtakatifu ameshamshukia , matatizo yapo pale pale , magonjwa na kifo kipo pale pale, omba usiombe hakuna utakachobadilisha, nanyi farijianeni kwa maneno hayo tu, 1wathethalonike 4-18.
 
Kuna dada yetu,tunapokutana kifamilia na familia zetu,hakuna anayetaka ku share nae room ya karibu yake ...maana asub anamkemea shetani kwa sauti aisee ni sauti ya juu.

Watu hawamjui shet, shet hata malaika wanamgwaya halafu wewe unamkemea.Mwombe Mungu akulinde tu ,shetani anahudhulia mbele za Mungu
 
Sio Lazima, soma Mathayo 6
 
 
Maombi ya vita yapo. Mfano kama unasoma biblia kuna mahali Petro alipiga kelele kuomba msaada ili asizame. Na pia kuna kipofu alipiga kelele kuomba uponyaji.

Unaweza kuwa umelala usiku, ghafla unashtuka hupati hewa ya kutosha ilihali madirisha yapo wazi. Hapo sidhani kama utaomba kawaida maana hiyo ni vita.
 


Ndo maana watu wa dini nyie mapepo, mikosi, umaskini , magonjwa , huwa havikauki kwenu .

Ukiamka ukakuta Pumzi imebana fatilia Afya yako na omba Mungu akupatie Utulivu calmness .


Usimuombee MTU mabaya wala usihangaike na kumkemea shetani
 
Unaweza kuomba kwa sauti.
Halafu ukichoka kuomba kwa sauti unaweza kuomba kwa kunong'ona( whisper)
Ukichoka kunong'ona unaweza kuomba kimoyomoyo( mental ).
Ni kama kusoma, unaweza kusoma kwa sauti
Au kusoma kwa kunong'ona
Au kusoma mentally.
Au kusoma bila verbal or mental recitation.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…