Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Kupigwa makwenzi, makofi, ngwara, ngumi au mateke na mwenzi wako wa kike, hadharani au faragha ni sahihi hata kama umekosea?
Jamaa, jirani mwenye ndoa yake mtaani, na ana nafasi kubwa tu miongoni mwa mashirika ya kutoa huduma za kifedha mjini, ameamua kwenda kuripoti kwa mjumbe baada ya kuchoshwa na kipigo cha makwenzi, makofi, ngumi na mateke vya mara kwa mara kutoka kwa mkewe. Lakini kama haitoshi, akuamua pia kwenda kuripoti polisi kwa msisitizo na msaada zaidi.
Hii imekuja baada ya muungwana huyu kushindwa kuvumilia hali hiyo inayojirudia mara kwa mara kutoka kwa mkewe, na kuamua kuvunja ukimya na kutafuta usaidizi huko alikoenda kuripoti..
Jamaa atasaidika au atafedhehheka kwenye jamii?
Kama mwanaume kamili, unadhani jamaa amekosea ama yuko sahihi?
Na je, unadhani hali hiyo itaimarisha na kuchochea afya na uhai wa ndoa yao, au itadhoofisha na pengine kusambaratisha kabisa ndoa yenyewe?
Nani wa kulaumiwa baina yao..
NDOA SI LELEMAMA NDRUGO ZANGO, YAHITAJI HEKIMA, UVUMILIVU, USTAHIMILIVU NA SUBRA YA KIPEKEE SANA.