Takwimu za sasa ukifuatilia zinapotosha sana kusema mwanaume ndie anaonekana kuwa mnyanyasaji wa kijinsia katika matukio.
Ukweli ni kwamba, initiators au wasababishaji wa kwanza domestic Violence eneo la mahusiano kwa asilimia kubwa ni wanawake. Hii ni kwasababu jamii inatazama zaidi physical abuse and violence kuwa ndio ushahidi ila wanaacha Emotional abuse and violence ambayo ndiyo hatari na kubwa sana kufanyika katika mahusiano.
Wanawake wanakauli ambazo ukizitazama kwa uzito huwa zinachokoza au kuamsha tabia za ubabe kutoka kwa wanaume aidha kwa makusudi au bila wao kujua.
Kwa mfano, mwanamke anaweza kuwa na kauli za dharau kwa mwanaume wake ambaye hana kazi au kipato kizuri ila ni mwanaume ambaye anampenda mwanamke wake na kumjali ila ni kukosa kipato kuna mfanya ashindwe kumpatia baadhi ya vitu.
Mwanamke atakuwa na kauli za kukatisha tamaa, kufedhesha,kushusha heshima na kudhalilisha mfano, "Mbona wenzako wanafanikiwa wewe una shida gani", "me sioni kama humu ndani kuna mwanaume ", " Mwanaume utakuwa wewe","Kama hauhudumii wapo watakaoweza kuhudumia", "unavyokula chakula kwa kujiachia utadhani umetoa hela" na kadhalika.
Hizi kauli zinapomfikia mwanaume huamsha hisia za kisasi, chuki dhidi ya wanawake, hasira, jazba, na huamsha akili ya kutaka kumdominate mwanamke kwa nguvu ili kudhibiti hizo kelele na kujiprotect psychologically.
Matokeo yake ni mwanaume kubadilika na kuanza kuwa mkorofi nakuanza kumtreat mwanamke wake kwa jazba na hasira. Hapo ndipo jamii sasa huanza kufuatilia na kusema wanaume ni chanzo cha kunyanyaswa wanawake bila kufahamu kuwa mwanaume alipitia mengi ambayo hayakuzungumzwa popote na yalifanyika vyumbani.
Abuse zipo nyingi sana wanawake huwafanyia wanaume zao na kusababisha wanaume kuanza kuwachukia. Imagine mwanaume umerudi nyumbani umedhurumiwa huko, ulikamatwa na traffic ukatolewa pesa, una madeni unarejea nyumbani ukiwa haupo sawa, mwanamke uliyeoa ambaye jukumu lake ni kukusaidia wewe nyakati kama hizi kwa kuwa mfariji, rafiki, sikio la malalamiko yako ndie anageuka kuwa adui wa ndani.
Unafika home kwanza hajali ile facial expressions ya uso wako kuwa haupo sawa, una wasiwasi, una huzuni na haupo sawa anakupuuza hata hakuulizi una tataizo gani au kutaka kukutoa kwenye hiyo hali, hapa unampa ujumbe mwanaume kuwa haujali afya yake ya akili.
Mwanaume anaingia ndani mwanamke humfwati hadi akuite akiwa na shida ya kitu. Unamjengea fikra kuwa sisi sio marafiki. Unaandaa chakula tena pengine ambacho hakipendi,au hauandai kabisa aende kukijuta jikoni saa nne za usiku akitafuta chakula sababu ya njaa.
Usiku analala na mawazo mwanamke anapiga kimya haulizi wala kujali mwanaume analala na msongo wa mawazo. Asubuhi unaamka na mawazo ya siku itakavyokuwa mbaya, mwanamke amelala hadi ule muda ambao angekuwa anakuandalia chai kwa upendo yeye kalala kama mamba kwenye kingo ya mto. Unajiandaa kwa hasira usepe, anakuongelesha kwa sauti ya lawama huku amelala kitandani kuwa unaondokaje kimya kimya yeye anahitaji pesa ya hiki na hiki na kile ukitazama vitu anakulistia vingi ni madeni yake personal.
Mtu wa hivi kwann siku akikupandisha mori usimzibue kwa kipigo kama unaua nyoka?
Wanawake mjifunze sana, kuwa mke sio kazi kubwa kama mnavyodhania. Mke ni rafiki sio mtumwa wala mfanyakazi. Rafiki huwa ni msaidizi na partner.